Usugu huu wa uchafu kukithiri na kutotolewa kwa wakati muafaka ni kero kwa wakazi wa jiji la Mbeya.
Na mwandishi wetu.
Wafanyabiashara jijini Mbeya wametakiwa kuboresha usafi wa mazingira kwa kufanya biashara zao katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa dhumuni la biashara husika.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama wakati wa mahojiano na mwandishi wetu kuhusiana na uchafu uliokithiri katika vituo mbalimbali vya kufanyia biashara.
Ameeleza kuwa kumekuwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wanafanyabiashara zao maeneo ambayo si rasmi hivyo kupelekea uchafunzi wa mazingira hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Aidha Bwana Balama ametahadharisha kwamba ofisi yake haitasita kuwachukulia sheria wafanyabiashara wenye tabia ya kuchafua mazingira hali inayopelekea jiji kuwa katika hali ya uchafu.
0 comments:
Post a Comment