Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo cha Teofilo kisanji kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Mkoani Mbeya Bwana Ambukege Imani akizungumzia na waandishi wa habari namna walivyokataliwa kupewa kibali cha kufanya maandamano na Jeshi la polisi baada ya wanachuo hao kushitushwa na taarifa iliyotoka bodi ya mikopo kuwa hawataweza kuwapa mikopo yao mpaka ifikapo mwezi Desemba 12, mwaka huu.
Maandamano hayo ya zaidi ya wanafunzi 4,500 wa chuo cha TEKU yalianza majira ya saa sita za mchana wakitokea katika chuo chao kilichopo eneo la Block T kata ya Iyela jijini Mbeya na kwa mujibu wa Waziri wa mikopo wa chuo hicho Mwilenga Lucas amedai kuwa kutokana na kucheleweshewa mikopo hiyo wana hali mbaya ya kimaisha hivyo majibu yasiyoridhisha kutoka bodi ya mikopo ndiyo yanawalazimisha wanachuo hao kufikia hatua hiyo.
Wanafunzi wa chuo cha TEKU jijini Mbeya wakiwa wameketishwa chini baada ya kuzuiwa na askari wa kuzuia ghasia kuingia katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakati wa maandamano yao ya kutaka kutafutiwa ufumbuzi juu ya taarifa iliyotoka bodi ya mikopo kuwa hawataweza kuwapa mikopo yao mpaka ifikapo mwezi Desemba 12, mwaka huu.
Askari wa kuzuia Ghasia walifika mapema kwa usafiri wa magari mawili yenye nambari za usajili PT 2079 na PT 0796, nje ya Jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika maandamano yaliyofanywa na wanafunzi wa chuo cha TEKU jijini Mbeya ya kutaka kutafutiwa ufumbuzi juu ya taarifa iliyotoka bodi ya mikopo kuwa hawataweza kuwapa mikopo yao mpaka ifikapo mwezi Desemba 12, mwaka huu.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Teku(kulia) na Waziri mkuu wake(kushoto) wakiwa hawana la kufanya baada ya wanafunzi hao kuzuiwa na askari wa kutuliza ghasia kuingia katika ofisi ya mkuu wa mkoa Mbeya.
Baada ya askari wa kuzuia ghasia kufanikiwa kuwadhibiti wanafunzi kuendelea na mgomo, wanafunzi hao walifanya maandamano ya Amani na kueleza sababu yao ya kufika kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ni juu ya kukwama kwa jitihada zao za kufuatilia mikopo hiyo.
0 comments:
Post a Comment