Na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Chama cha
wachimba madini mkoani Mbeya tawi la Chunya(Mberema)wametakiwa kuachana na
kuchimba madini kwa mazoea badala yake watumie Teknolojia za kisasa ili
kuepukana na hasara wanazozipata katika uzalishaji.
Haya
yameelezwa na mawakala wa Jiolojia
Tanzania(GST) kutoka Dodoma katika kikao
cha chama cha wahimba madini tawi la Chunya (mberema) Kilichokuwa kikiongozwa
na mwenyekiti wa wachimba madini mkoa wa Mbeya Leonard Manyesha,wakati wataalamu
hao wakitoa elimu juu utafiti wa miamba kwa
kutumia vifaa vya kisasa ili kubaini uwepo wa madini wanayoyatafuta.
Wakitoa mada
kwa wachimbaji madini kwa njia ya kisansi mjiolojia Alphoncce Michael na mjiofizikia Octavian
Minja walisema utafutaji wa madini kwa njia ya jiolojia hutumika kuanisha
miamba na madini kwenye eneo husika na
kupata taarifa kwa haraka zaidi na hupunguza gharama za uendeshaji kwa
kuokoa muda na kujua uwepo wa madini au laa.
Walisema
baada ya kufanya tafiti mchimbaji anaweza kujua ni nini afanye ili aweze kupata
kile anachokihitaji kwani wamedai kuwa njia za asili za kutazama kwa macho kwa
kuangalia aina ya udongo zinachua muda mrefu na hutumia nguvu nyingi na gharama
huwa kubwa bila kujua kama anchokitafuta atakipa ipasavyo.
Aidha
wachimbaji waliohudhulia kikao hicho walisema waliwashukuru mawakala hao wa
jiolijia kwa kuwaletea elimu hiyo ya
uchimbaji wa kisasa na kuomba ofisi ya madini kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya chunya ieweze
kuwasaidia kuhakikisha mitambo hiyo ya kufanyiwa utafiti inawafikia wachimbaji kwenye
maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa manufaa.
0 comments:
Post a Comment