Upondaji kokoto
Na mwandishi wetu.
Vijana wametakiwa kujishughulisha katika shunguli halali na salama ambazo zitawawezesha kujipatia kipato cha kutosha badala ya kukaa vijiweni na kupiga soga.
Ushauri huo umetolewa na wakulima wa bonde la Umwagiliaji kata ya Igawilo jijini Mbeya kufuatiwa kuwepo kwa malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vijana kuhusu ajira.
Aidha wameziomba halmashauri nchini kuandaa mpango utakao wawezesha vijana kujituma katika shughuli za kilimo ili kujenga uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao vijana wa eneo hilo wamesema uhaba wa mitaji na riba kubwa inayotozwa na taasisis za kifedha nchini mara baada ya kurejesha mikopo ni moja ya sababu zinazochangia vijana wengi kukimbilia katika shughuli za upondaji kokoto.
Mwandishi wetu ameshuhudia idadi kubwa ya vijana wanaoishi pembezoni mwa bonde hilo wakijishughulisha na upondaji wa kokoto huku wazee wakijishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.
0 comments:
Post a Comment