Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu
Baadhi ya washiriki wa mdahalo wa miaka 50 ya Uhuru uliofanyika jana katika ukumbi wa Mkapa wameiomba serikali kuangali upya sera ya soko huria kutoka na sera iliyopo sasa kuwakandamiza watu wachache.
Akiongelea maendeleo ya kiuchumi hapa nchini dakta Gwamaka Mwankenja kutoka chuo cha kikuu cha Neema amesema licha ya utandawazi wa soko huria kuleta mabadiliko ya kiuchumi bado wananchi wa chini wameshindwa kufanikiwa kutoka na kutokuwa na mtaji wa kutosha.
Awali akifungua mdahalo huo mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amesema katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru Tanzania imewawezesha wananchi wake kujikomboa dhidi ya ujinga, umasikini, Afya, Maji, Mawasiliano na Kilimo ambapo hivi sasa mkulima amewezesha mbinu za kutumia kilimo cha kisasa.
0 comments:
Post a Comment