Pages


Home » » MGOMO WA WANAFUNZI WAPELEKEA CHUO CHA UUGUZI IFISI MKOANI MBEYA CHAFUNGWA KWA MUDA WA WIKI MOJA

MGOMO WA WANAFUNZI WAPELEKEA CHUO CHA UUGUZI IFISI MKOANI MBEYA CHAFUNGWA KWA MUDA WA WIKI MOJA

Kamanga na Matukio | 06:14 | 0 comments
 Bweni la Wanawake katika Chuo cha uuguzi cha Ifisi
 Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa katika harakati za kuondoka chuoni hapo.
Na mwandishi wetu.
Chuo cha uuguzi na maabara kinachomilikiwa na Kanisa la uinjilisti kilichopo ndani ya hospitali Teule ya Ifisi kimefungwa kwa muda wa wiki moja kuanzi hapo jana Septemba 30, Mwaka huu, kutokana na madai ya wanafunzi kuwa wamekuwa wakilishwa chakula kibovu.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanafunzi hao kwa sharti la kutotanjwa majina yao wamesema wamekuwa wakilishwa mikate inayotengenezwa kwa ngano na uji wa ulenzi ambao umekuwa na michanga.
Wameongeza kutokana na wao kwenda kusimamia afya hali hiyo ni hatari kwa afya zao hali iliyopelekea kutoingia madarasani na Uongozi wa chuo hicho kuchukua jukumu la kukifunga chuo hicho.

Kwa upande wa mkurugenzi wa maendeleo ya kanisa hilo Mchungaji Marcus Lehner amesema ameyapokea malalamiko yao na kumwagiza makamu wa maendeleo Mchungaji TitoNduka kukaa na uongozi wa wanafunzi hao ili kuondoa tofauti zilizopo.

Ameongeza kuwa walikutana jana majira ya saa saba mchana na kuwaagiza uongozi wa wanafunzi hao kuondoka chuoni mara moja na kurudi baada ya wiki moja na kuwataka kuwataja vinara wa mgomo huo.

Katika harakati za kufunga chuo hicho haraka haraka baadhi ya wanafunzi walifungiwa mabweni kwa muda wa masaa manne, mwandishi wa mtandao huu alibaini kuwakuta wanafunzi wa kike wakiangaika kutoka kwa baadhi ya mabweni na baada ya kupata taarifa hiyo uongozi wa chuo hicho waliagiza wafunguliwe.

Hata hivyo baadhi ya wanafunzi watokao mikoa ya mbali walikutwa wakirandaranda mitaani na wengine kujihifadhi kwa ndugu zao.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger