Pages


Home » » RAIA MMOJA WA CHINA AMEFARIKI DUNIA NA WATATU KUJERUHIWA BAADA YA GARI KUACHA NJIA NA KUPINDUKA ENEO LA MSWISWI - MBARALI - MBEYA

RAIA MMOJA WA CHINA AMEFARIKI DUNIA NA WATATU KUJERUHIWA BAADA YA GARI KUACHA NJIA NA KUPINDUKA ENEO LA MSWISWI - MBARALI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:44 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Mkazi mmoja Kongolo Kyiyu Owoju mwenye umri wa miaka 45 Raia wa China amefariki dunia ka ajali ya gari juzi, maeneo ya Mswizi wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na watu watatu kujeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T 625 ANH aina ya Honda CRV kuacha njia na kupinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Anacletus Malindisa amesema dereva wa gari hilo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu pamoja na majeruhi watatu ambao ni Housh Youni mwenye umri wa miaka 15, Peong Fongwi mwenye umri wa miaka 58,na Hong Weiy mwenye umri wa miaka 56  wote ni raia wa CHINA.  
                                                                
Aidha Malindisa amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi  majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Chimala na gari lipo kituoni Chimala.

Aidha amesema Jeshi Polisi limemshikilia Veronica George mkazi wa Isansa Wilayani Mbozi kwa kosa la kumtumbukiza mtoto wake  wa kike mwenye umri wa siku tatu.

Veronica amemtumbikiza mtoto huyo baada ya mumewe aitwaye Majaliwa Mwampashi kukataa kwamba mtoto  huyo si wake.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger