Pages


Home » » NAIBU WAZIRI WA ELIMU PHILP MULLUGO AKABIDHI MISAADA MASHULENI WILAYANI CHUNYA.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU PHILP MULLUGO AKABIDHI MISAADA MASHULENI WILAYANI CHUNYA.

Kamanga na Matukio | 06:05 | 0 comments

Naibu Waziri wa elimu na mbunge wa jimbo la Songwe mkoani Mbeya Philip Mullugo ametoa vitabu 6,000 vya Sekondari na Msingi, Compyuta 40 (Laptop) kwa walimu, Madawati 80 ya kisasa ya katika Sekondari za kata wilayani Chunya.

Akizungumza na mwandishi wetu Naibu Waziri Mullugo amesema kuwa ametoa vifaa hivyo ili kuiwezesha wilaya hiyo kuendelea kielimu.

Aidha ameahidi kutoa shilingi milioni 70 kwa ajili ya kuchimba visima 17 vitakavyosaidia kupunguza tatizo la maji wilayani humo hasa kwa shule za sekondari za kata.

Wakati huohuo amewataka wananchi wilayani humo kuunga mkono mfuko wa Elimu wa jimbo la Songwe unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni ambayo yeye kama mbunge atatoa shilingi milioni 5.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger