Pages


Home » » WACHUNGAJI WA KKKT DAYOSISI YA KONDE MBOZI - MBEYA - WAKOSA IMANI NA KAMATI MPYA YA MAADILI

WACHUNGAJI WA KKKT DAYOSISI YA KONDE MBOZI - MBEYA - WAKOSA IMANI NA KAMATI MPYA YA MAADILI

Kamanga na Matukio | 03:58 | 0 comments
MOSHI+NA+MALASUSA.jpg Maaskofu pamoja na wachungaji na viongozi wengine wa usharika wa Vwawa na jimbo la Magharibi Mbozi.
+++++
Na mwandishi wetu.
Baadhi ya wachungaji wa kanisa la kiijili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya Konde wamesema hawana imani na kamati ya utekelezaji wa halmashauri ya kichungaji inayoongozwa na Baba askofu Dakta Peter Mwakyolile ambayo inasimamia maadili na usuluhishi  baina ya wachungaji.

Wakizungumza na chanzo hiki kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutotajwa majina yao wachungaji hao wamesema kujiuzulu kwa Katibu wa kamati hiyo Mchungaji Michael Ambangile kumetokana na mvutano wa muda mrefu kati yake na mkuu wa Jimbo la Magharibi Mchungaji Nyibuko Mwambola ambaye ni mjumbe wa kamati.

''Sababu ya kujiuzulu kwangu ni kutokana na mvutano wa muda mrefu kati yangu na mtumishi mwenzangu'' alisema Mchungaji Ambangile kupitia barua iliyomwandikia Askofu wa dayosisi hiyo.

Nao baadhi ya wachungaji na waumini wamemwomba Askofu wa dayosisi hiyo kuivunja kamati iliyoteuliwakwani baadhi ya wajumbe huendekeza majungu, mabishano na malumbano yasiyokuwa na tija yoyote kwa kanisa.

Kwa upande wake Mwambola amesema hajawahi kuwa na ugomvi na Mchungaji Ambangile na hajapata nakala ya barua iliyoandikwa kuhusu malalamiko yanayo mkabili.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger