Pages


Home » » UBOVU WA MIUNDOMBINU NI CHANZO KIKUBWA KWA WAFANYABIASHARA NA WATEJA KUKIMBIA SOKO + MBEYA

UBOVU WA MIUNDOMBINU NI CHANZO KIKUBWA KWA WAFANYABIASHARA NA WATEJA KUKIMBIA SOKO + MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:33 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Uongozi wa soko la Isanga jijini Mbeya umesema ubovu wa miundombinu ya soko pamoja na barabara inayoingia sokoni hapo ni moja ya sababu inayochangia soko hilo kukosa huduma za bidhaa muhimu zinazohitajika na wateja.

Mwenyekiti wa soko hilo Bwana Aidani Mwashigaire amesema kutokana na ubovu wa barabara wafanyabiashara wa soko hilowamekuwa wakilazimika kulihama soko hilo na kwenda soko la Darajani ambalo ni rahisi kufikisha bidhaa sokoni.

Aidha ameuomba uongozi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kuangalia upya maamuzi yao kwa kulipitisha soko la darajani na badala yake, ameuomba uongozi huo kuwaunganisha wafanyabiashara wa darajani na wale wa Isanga.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger