Na mwandishi wetu
Walanguzi wa zao la Ufuta wilayani Chunya mkoani Mbeya wamegundua mbinu mpya ya kuwaibia wakulima wa zao hilo kwa kuwalazimisha wakulima hao kuuza ufuta ambao utapimwa kupitia madebe yao ambayo yanaukubwa tofauti na madebe mengine.
Uchunguzi wa mwandishi wetu wilayani humo umebaini kuwa madebe hayo yametanuliwa ili kuyafanya kuwa na ukubwa zaidi wa kuweza kubeba kiasi kikubwa cha mazao.
Wakiongelea kuhusu ushuru na wizi unaofanywa na walanguzi wa zao la ufuta wakazi hao wa Mbuyuni wanasema bei za ufuta zimekuwa mbaya sana ambapo ni shilingi 13,000/= hadi 15,000/= ambapo kwa debe ambalo ni kubwa kuliko debe la kawaida maarufu kama “debe la biashara” ambalo huwa na ujazo wa lita ishirini na mbili dadala ya lita ishirini na kwamba ukipima debe 5 moja huongezeka.
Wameongeza kuwa mara nyingi wafanyabiashara kutoka Mbeya mjini hutumia debe hilo ambalo huchemshwa na kupanuliwa na kuwa na ujazo mkubwa kuliko debe la kawaida ambapo wakuliwa huumia na kuwasababishia hasara kutokana na kuibiwa kutokana na vipimo vya debe hilo.
Pamoja na hayo wameuomba uongozi wa halmashauri kuangali upya utaratibu wa kuchukua fedha za ushuru na faini wanazotozwa wafugaji na wakulima kwa kuiomba kutenga baadhi ya fedha ili ziweze kusaidia maendeleo ya kata badala ya wao kila mwaka kuendelea kuchangia zaidi ya shilingi elfu hamsini.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Mbuyuni Bwana Daudi Mpakasi anasema kuwa mchango halali wa ujenzi wa shule ya sekondari ni shilingi elfu ishirini na zote hulipwa katika halmashauri ya wilaya ya chunya na kwamba elfu hamsini inayozungumzwa na wananchi labda wanajumuisha na michango mingine ya shughuli za maendeleo.
0 comments:
Post a Comment