Baadhi ya vibaka wakiwa wameng'oa Mashine za kutengeneza sahani na vikombe vya udongo katika Soko la Sido Mwanjelwa ambazo hazikuharibiwa na moto lakini wameziuza kama Vyuma chakavu, Je huu ni uungwana na tabia hii ya kutamani fedha kwa kuuza kitu cha thamani kubwa kwa bei ndogo hali kodi za wananchi zikinufaisha watu wachache.
Polisi walifika eneo hilo na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi
Mashine hii nazo iling'olewa
Vipuli ambavyo viling'olewa kwenye mashine
Hizi ni baadhi ya mashine ambazo polisi walifanikiwa kuziokoa, baada ya kufika na kuwatawanya vibaka hao kwa mabomu ya machozi
Mashine ikiwa imeondolewa swichi kubwa/Main switch na vibaka bila kujua thamani ya mashine hiyo.
Pia na hii ni mashine ambayo imeokolewa
Gari ambayo ilipinduliwa na kujaribu kung'olewa Injini ambapo vibaka hao hawakufanikiwa.
Watoto bila kujali moto walikuwa wakijitafutia chochote.
Bila aibu yoyote na hawa wakifika katika soko hilo lililoungua wakiwa na vitendea kazi au dhana za kukatia vyuma, kama msemeno
Mzee huyu kwa uchungu baada ya kuunguliwa kwa banda lake akiwazuia watu wasiingie katika eneo lake, kutokana na kuwa na baadhi ya masalia ya bidhaa zake.
Dada huyu mwenye asili ya China akishangaa baada ya kuvunjwa kwa chumba chake cha biashara licha ya kuwa Moto haukuweza kufika eneo lake.
Kushoto Mama huyu akilia kwa huzuni baada ya kukuta kila kitu kimeteketea, na moto kwani alikuwa safarini..
0 comments:
Post a Comment