Ufugaji wa Ng'ombe kiholela pasipo kuzingatia njia za kitaalamu.
*****
Na mwandishi wetu
Wakazi wa kata ya Mbuyuni wilayani Chunya mkoani Mbeya wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara na gharama kubwa ya ushuru unaotozwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa wafugaji na wakulima.
Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wakulima na wafugaji wa kijiji cha Chang’ombe kata ya Mbuyuni wamesema katika kipindi cha masika wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi kutokana na barabara kutowekewa miundombinu bora ya kupitisha maji wakati wa mvua
Akiongelea tatizo hilo mmoja wa wakazi hao Kasimu Shabani anasema kiangazi maji hakuna katika sehemu za malishio Kipembao na Mbangala walizotengewa na baadhi ya Maafisa mifugo wamekuwa wakinufaika na ushuru kama fursa ya kujitajirika kutokana na kuishi na kujenga nyumba nzuri.
Aidha kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo za ushuru wakulima na wafugaji hao wanasema gunia la bebe kumi hulipiwa nauli kutoka eneo la kuzalishia mazao mpaka Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini na ushuru wa kila debe hulipiwa ushuru shilini elfu moja na wakala katika mauzo ya mazao hayo huitaji malipo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya mbuyuni Daudi Mpakasi anasema kuwa wafugaji wamekuwa wakitumia mto Songwe ambao haukauki na unakuwa na maji muda wote kiangazi na masika na baadhi yao wamekuwa wakiona ni mbali na kuamua kuchimba visima jirani na maeneo yano na kuhamishia mifugo.
Ameongeza kuwa ushuru wa mfugaji anapozidisha idadi ya ng’ombe hulazimika kulipa faini ya shilingi elfu ishirini kwa kila ng’ombe.
Hata hivyo wamemuomba mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro kufanya ziara maalumu ya kufanya mkutano wa hadhara na wakulima na wafugaji ili kuondoa tofauti zao ambazo zimekuwa zikisababisha mgogoro baina yao mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment