Pages


Home » » WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI

WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI

Kamanga na Matukio | 05:57 | 0 comments


Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde
 *****
Watu wa tatu wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya katika kijiji cha Ivuna kata ya Kamsamba wilayani Mbozi, kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule ya sekondari ya Ivuna vikiwemo saruji, rangi na chokaa.

Amewataja watu hao kuwa ni Mkuu wa shule ya sekondari ya Ivuna Bwana Danford Mwakaswaja, Erick Mkamba ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya shule na Magazeti Simfukwe ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Ivuna.

Kwa pamoja watu hawa wanadaiwa Oktoba 18, mwaka huu majira ya saa 11 jioni walikamatwa na wananchi wa kijiji hicho cha Ivuna wakiwa wamebeba katika gari, wakidai wanavipeleka katika shule ya Msingi Itumbula kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi hali iliyopelekea wananchi hao kupinga taarifa hizo na kuamua kuita Jeshi la polisi.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi magharibi Mheshimiwa David Silinde amesema kwamba watu hao walikuwa na nia ya kuiba na sababu ya kuwa vinatumika katika ujenzi wa shule ya msingi si sahihi.

Naye Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa amesema watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha Polisi Vwawa na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger