Jamii imeshauri kutunza mazingira kwa kutumia njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kudhibiti uharibifu wa tabaka la ozoni.
Ushauri huo umetolewa na afisa mazingira ofisi ya makamu wa Rais Japhet Kaniziusi wakati wa warsha ya siku mbili iliyofanyika kwenye ukumbi wa Paradise Mbeya na kuwakutanisha wadau wa mazingira kutoka mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini.
Amesema warsha hiyo imelenga kuondoa hatari ya kutokea kwa maafa makubwa kutokana na uharibifu wa tabaka la ozoni linalochangiwa na matumizi mabaya ya jokofu na viyoyozi.
Akifunga warsha hiyo mkuu wa chuo cha Veta Mbeya Bitubi Makongoro amezitaja faida za umuhimu wa tabaka la hewa ya ozoni kuwa ni kulinda afya ya binadamu na mazingira ambapo ameitaka jamii kwa pamoja kulilinda tabaka hilo kwa kuangali a matumizi bora ya jokofu na viyoyozi
0 comments:
Post a Comment