Makao Makuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Na mwandishi wetu.
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imeombwa kuboresha miundombinu ya soko la Tukuyu ilikuweka mazingira bora ya uwekezaji.
Tamko la ombi hilo limetolewa na wafanyabiashara wa soko hilo ambao wamesema kwa muda mrefu soko hilo limekosa mifumo thabiti ya kutililisha maji machafu hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko wakati wa msimu wa mvua.
Aidha uchunguzi uliofanya na mwandishi wetu umebaini kuwa soko hilo halina barabara za ndani sababu inayochangia kushindwa kuokoa bidhaa linapotokea janga la moto na wakati mwingine kushindwa kuingiza bidhaa zinazobebwa kwenye magari.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko hilo Bwana Almas Yazidu amesema uhaba wa umeme wa uhakika pamoja na vyoo visivyo na sifa sitahiki imepelekea wafanyabiashara wengi kutowekeza mitaji yao mikubwa sokoni hapo na hivyo halmashauri hiyo kukosa mapato ya kutosha.
Chanzo chetu kilipojaribu kuwatafuta viongozi wa halmashauri hiyo wanaosimamia soko hilo na kuambiwa kuwa viongozi wapo nje ya ofisi kikazi.
0 comments:
Post a Comment