BABA MZAZI ATUMIA SIRAHA ZA ULINZI KUMWADHIBU MTOTO WAKE WA MIAKA 10 KWA KOSA LA KUTOKWENDA SHULE JIJINI MBEYA

Chimbuko Letu | 01:55 | 0 comments
 Victoria Mukama (10) akiwa hospitali ya rufaa mbeya baada ya kupigwa na baba yake mzazi  sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa  vya ulinzi likiwemo Lungu.
Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.
 Victoria Mukama (10) baada ya matibabu


KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama  mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.
Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.
Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.
Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.
Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.
Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.
Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.
Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.
Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.
Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.
Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.
Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.
Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya. 

WATU watano wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuharibika, Mkoani Mbeya

Chimbuko Letu | 01:44 | 0 comments
Kondakta wa basi hilo, Ulimboka Noah (26) alisema sababu ya kutokea kwa ajali hiyo ni kutokana na gari kugoma kubalisha gia ambapo dereva alivyojaribu kubadili ilishindikana ndipo alipojaribu kushuka nalo hivyo hivyo lakini kabla ya kufika darajani ilikuwa kama kitu kimelichota gari na kupinduka.
Muuguzi mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi ambako majeruhi wote walipelekwa, Sikitu Mbilinyi alikiri kupokea majeruhi 22 na kusema kati yao Wanaume 8 ambao hali zao zinaendelea vizuri kutokana na kutoumia sana ingawa wanamichubuko usoni na sehemu za mikono na miguu.WATU watano wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuharibika, baada ya dereva kushindwa kulimudu kutokana na mwendokasi.
Ajali hiyo ilitokea  majira ya saa sita mchana katika Mtelemko wa Mlima Senjele katika Mpaka wa Halmashauri ya Mbeya na Wilaya ya Mbozi eneo la Songwe Mkoani hapa, wakati gari hilo likitokea Tunduma kwenda Jijini Mbeya.
Gari hilo lenye namba za usajili T 378 ADR aina ya Toyota Costa  lilikuwa likiendeshwa na Dereva Semu Mwakajwanga anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 60 na 70 ambaye alitoweka baada ya tukio.
Muuguzi mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi ambako majeruhi wote walipelekwa, Sikitu Mbilinyi alikiri kupokea majeruhi 22 na kusema kati yao Wanaume 8 ambao hali zao zinaendelea vizuri kutokana na kutoumia sana ingawa wanamichubuko usoni na sehemu za mikono na miguu.
Aliongeza kuwa kati ya majeruhi hao wanawake 10 walipokelewa wakiwa katika hali ya kuumia sana na kupatiwa matibabu ambapo kati yao Wanne walipewa Rufaa kutokana na hali zao kutokuwa katika hali nzuri, wengi wao wakiwa wameumia vichwa na kuvunjika miguu.
Alisema pia kati ya majeruhi hao watoto ni wanne ambao hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na kuongeza kuwa taarifa za eneo la tukio kwamba watu wanne walikufa papo hapo na mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano.
Kwa upande wake Kondakta wa basi hilo, Ulimboka Noah (26) alisema sababu ya kutokea kwa ajali hiyo ni kutokana na gari kugoma kubalisha gia ambapo dereva alivyojaribui kubadili ilishindikana ndipo alipojaribu kushuka nalo hivyo hivyo lakini kabla ya kufika darajani ilikuwa kama kitu kimelichota gari na kupinduka.
Alisema kutokana na jinsi lilivyopinduka gari hilo inasemekana ni kutokana na kukatika kwa Propela Shafti ambayo ilijikita chini kasha kupindua gari au U- Bolt inaweza ikawa imeachia kwa kile alichosema eneo lilikuwa zuri na hukuna kitu kilicholigusa gari hadi likapinduka.
Bado miili ya marehemu haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mbeya Ifisi. 
Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.

Mgombea nafasi ya uraisi wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi hii jana amezindua rasmi.

Chimbuko Letu | 04:16 | 0 comments

Mgombea nafasi ya uraisi wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi hii jana amezindua rasmi kampeni za kuwani nafasi hiyo huku akitoa ahadi ambazo ana hakika atazitekeleza endapo atapewa nafasi  na wajumbe wa mkutano mkuu mwishoni mwa juma hili.


Jamali Malinzi ambae anaiwani nafasi hiyo kwa mara ya pili, baada ya mwaka 2008 kushindwa na raisi anaemaliza muda wake Leodger Chilla Tenga, amesema soka la Tanzania linahitaji msaada mkubwa ili liweze kufikia malengo yake pamoja na kuwafurahisha watanzania ambao wana uchu wa mafanikio.


Malinzi amesema mzizi mkubwa wa maendeleo ya soka nchini unatakia kujikita katika idara ya ufundi ya shirikisho la soka nchini na kama atapata nafasi ya kuwa raisi wa TFF atahakikisha idara hiyo inaboreshwa kwa lengo la kuufufua upya mkakati wa soka kuanzia kwa vijana wenye umri mdogo.

Katika hatua nyingine Jamali Malinzi akaguzia suala la mikataba kwa kusema endapo atapewa fursa ya kuliongoza shirikisho la soka nchini kwa ridhaa ya wapiga kura, atahakikisha kuwa muwazi katika hatua za kuingia mikataba na makampuni ambayo kwa sasa yanatumia kivuli cha soka kujinufaisha binafsi pamoja na baadhi ya watu wasiolitakia mema soka la Tanzania.

Webb amekanusha tetesi kuwa anataka kuchukua kugombea nafasi ya rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.

Chimbuko Letu | 04:15 | 0 comments


 FIFA-logo-300
Raisi wa Shirikisho la Vyama vya Soka vya Nchi za Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf, Jeffrey Webb amekanusha tetesi kuwa anataka kuchukua kugombea nafasi ya rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA inayoshikiliwa na Sepp Blatter.

Webb amehusishwa kugombea nafasi hiyo mwaka 2015, huku Blatter akipendekeza katika mkutano uliofanyika Caribbean Jumatatu iliyopita kuwa Webb anaweza kuchukua nafasi kuchukua nafasi yake siku zijazo.

Lakini Webb mwenyewe alikanusha suala hilo akidai kuwa hana mpango wa kugombea nafasi hiyo katika siku za karibuni.

Blatter ambaye aiongoza FIFA toka mwaka 1998 alikuwa akizungumza kufungua mkutano wa mwaka wa Concacaf.

Mwaka 2011 Blatter aliwaambia viongozi wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kwamba kipindi hiki kitakuwa cha mwisho kwake kukalia ofisi hiyo lakini mwaka huu ameonekana kubadili uamuzi baada ya kuonyesha ishara kama anaweza kugombea kwa kipindi kingine.

Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu ya Manchester United.

Chimbuko Letu | 03:42 | 0 commentsMeneja wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu hiyo kwasababu nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza alidhani yeye ni mkubwa kuliko meneja.
Katika kitabu chake kipya kinachoelezea maisha yake ya ukocha, Ferguson amesema aligombana na Beckham baada ya kumkosoa kwa kiwango chake alichokionyesha katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Arsenal ambao walipoteza.
Katika kitabu hicho Ferguson ameandika kuwa dakika ambayo mchezaji wa United atakapodhani yeye ni mkubwa kuliko meneja ni lazima aondoke na Beckham alidhani yeye ni mkubwa kuliko Ferguson ndio maana akamuuza.
Ferguson pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu mtindo wa maisha ya watu mashuhuri kufuatia nyota huyo kumuoa Victoria Adams aliyekuwa nyota wa kundi la muziki la Spice Girls nchini humo.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Beckham ndiye mchezaji pekee kati ya aliyowafundisha kuchagua maisha ya umaarufu na kitendo hicho hakikumfurahisha ndio maana akamuacha aondoke.
Lakini Ferguson alimpongeza nyota huyo kwa mchango wake uliochangia mafanikio mengi ya United na kumtaja kama kioo cha watoto wote duniani.
Katika kipindi chote cha miaka 26 aliyofundisha United, Ferguson alishinda mataji 38 na kufanikiwa kuwafundisha nyota kadhaa wakiwemo Beckham, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo, Peter Schmeichel, Bryan Robson, Roy Kean, Jaap Stam na Ruud Van Nistelrooy.

HATARIIII RELI YA TAZARA YAZIDI KUHUJUMIWA NAWAUZA VYUMA CHAKAVU MKOANI MBEYA

Chimbuko Letu | 00:44 | 0 comments
WAKATI SERIKALI IKIWEKA MIKAKATI YA KUNUNUA VICHWA VYA TRENI  YA TAZARA HUKU WENGINE WANAFANYA KAZI YA KULIHUJUMU SHIRIKA HILO KWA KUFUNGUA NA KUIBA MATALUMA YA RELI HIYO KUPELEKA KUUZA KAMA VYUMA CHAKAVU.


HII HATARI SANA HAPA TAYARI WAMEFUNGUA NATI ZOTE.
WAHUSIKA MPOOOOO?

JAMAA WASHAMALIZA KABISA KUIBA VYUMA VYAKINGO ZA DARAJA LA TRENI MAENEO YA MBALIZI MBEYA.TRENI HIYOOOOO INAPITA  MLEMLE KULIKOFUNGULIWA BOLT  JE WAHUSIKA MNALIONA HILI?.
Picha Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

BABA AUZA NYUMBA MTOTO AKIWEMO NDANI NA KUTOKOMEA

Chimbuko Letu | 00:36 | 0 comments
“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  


Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.

Hii ndiyo nyumba iliyouzwa mtoto akiwa ndani


Mwandishi wa Mbeya yetu  akizungumza na mwenyekiti wa kijiji cha Hatwelo Ibrahim Mponzi katikati akiwa  na barozi juu ya uuzwaji nyumba hiyoMwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.
VITENDO vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hususani vijijini, licha ya Serikali na asasi mbali mbali kulipigia kelele ambapo hivi karibuni Baba mmoja aliamua kuuza nyumba ikiwa na watoto ndani na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wasijue la kufanya.

Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.

Akizungumzia sakata hilo kijijini hapo, Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.

Alisema baada ya kumfungulia mtoto huyo ndipo ilipobainika kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeshauzwa huku mtoto akiwa ndani na ndipo mnunuzi alipofunga na kufuli bila kujua kama kuna mtoto ndani huku watoto wengine wakiwa kwa ndugu zao ambao pia hawakuelezwa kama nyumba imeuzwa.

Nyumba hiyo iliuzwa kwa Dati Nsagaje kwa gharama ya shilingi 750,000/= ikiwa ni nyumba mbili pamoja na kiwanja ambapo mnunuzi huyo alilipa kianzio cha shilingi laki nne biashara iliyofanyika tangu April 26 mwaka huu  na kiasi kilichobaki wakiwa wameahidiana kulipana Mwezi Mei 15, Mwaka huu.

Wahanga wa tukio hilo ambao ni watoto walisema hawakuwa na taarifa zozote za kuuzwa kwa nyumba wanayokaa ambapo walisikia kuwa baba yao ameenda Sumbawanga kumfuata  mke wake ambaye inasemekana aliolewa na mwanaume mwingine.

“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  

Mtoto mwingine aliyetelekezwa ambaye siku ya tukio alikuwa ameenda kulala kwa bibi yake Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuonesha kukosa uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walishiriki moja kwa moja zoezi hilo huku wakiwa wamesaini kama mashahidi na kugonga mhuri wa Serikali ya Kijiji walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo hawakuwa na majibu ya kuridhisha.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Hatwelo, Ibrahimu Mponzi, alisema kitendo alichokifanya muuzaji ni cha kawaida kwa sababu ameuza mali yake mwenyewe na kwamba wao kama majirani na serikali ya kijiji hawawezi kuhoji atakako waacha watoto kwa sababu ni mipangilio ya maisha ya kila mtu.

Mbali na mwenyekiti wa Kijiji kuwa shahidi wa upande wa mnunuaji akiwa sambamba na watu wengine wanne akiwepo Mkewe ambaye pia ni Balozi wa nyumba kumi pia waliosaini wengine ni ndugu wa mnunuaji ili hali muuzaji akiwa hana shahidi hata mmoja.

Na Ezekiel Kamanga
Mbeya Yetu

Inasemekana mama mzazi wa muuza nyumba amerudisha pesa kwa mnunuzi habari kamili za kurudishwa pesa hizo na hao wajukuu walipo sasa tutawaletea kesho 

BABA AUZA NYUMBA MTOTO AKIWEMO NDANI NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.

Kamanga na Matukio | 04:56 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hususani vijijini, licha ya Serikali na asasi mbali mbali kulipigia kelele ambapo hivi karibuni Baba mmoja aliamua kuuza nyumba ikiwa na watoto ndani na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wasijue la kufanya.


Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.


Akizungumzia sakata hilo kijijini hapo, Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku saba.


Alisema baada ya kumfungulia mtoto huyo ndipo ilipobainika kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeshauzwa huku mtoto akiwa ndani na ndipo mnunuzi alipofunga na kufuli bila kujua kama kuna mtoto ndani huku watoto wengine wakiwa kwa ndugu zao ambao pia hawakuelezwa kama nyumba imeuzwa.


Nyumba hiyo iliuzwa kwa Dati Nsagaje kwa gharama ya shilingi 750,000/= ikiwa ni nyumba mbili pamoja na kiwanja ambapo mnunuzi huyo alilipa kianzio cha shilingi laki nne biashara iliyofanyika tangu April 26 mwaka huu  na kiasi kilichobaki wakiwa wameahidiana kulipana Mwezi Mei 15, Mwaka huu.


Wahanga wa tukio hilo ambao ni watoto walisema hawakuwa na taarifa zozote za kuuzwa kwa nyumba wanayokaa ambapo walisikia kuwa baba yao ameenda Sumbawanga kumfuata  mke wake ambaye inasemekana aliolewa na mwanaume mwingine.


“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  


Mtoto mwingine aliyetelekezwa ambaye siku ya tukio alikuwa ameenda kulala kwa bibi yake Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.


Kutokana na kitendo hicho kutokubalika, baadhi ya Majirani baadhi ya majirani walisema ni kitendo cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho ambapo waliamua kuchanga fedha ili kuikomboa nyumba ili irudi mikononi mwa watoto.


Majirani hao walifanikiwa kuchanga shilingi 410,000/= alizokuwa amedai mnunuaji ili aweze kurejesha nyumba ikiwa ni fedha alizokuwa ametoa awali hivyo kukubaliana kuicha nyumba hiyo ambayo kwa mujibu wa majirani na baadhi ya ndugu wamesema itakuwa ni mali ya watoto.


Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuonesha kukosa uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walishiriki moja kwa moja zoezi hilo huku wakiwa wamesaini kama mashahidi na kugonga mhuri wa Serikali ya Kijiji walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo hawakuwa na majibu ya kuridhisha.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Hawelo, Ibrahimu Mponzi, alisema kitendo alichokifanya muuzaji ni cha kawaida kwa sababu ameuza mali yake mwenyewe na kwamba wao kama majirani na serikali ya kijiji hawawezi kuhoji atakako waacha watoto kwa sababu ni mipangilio ya maisha ya kila mtu.


Mbali na mwenyekiti wa Kijiji kuwa shahidi wa upande wa mnunuaji akiwa sambamba na watu wengine wanne akiwepo Mkewe ambaye pia ni Balozi wa nyumba kumi pia waliosaini wengine ni ndugu wa mnunuaji ili hali muuzaji akiwa hana shahidi hata mmoja.


Aidha juhudi za majirani kuikomboa nyumba hiyo na kuwa mali ya watoto zilifanikiwa ambapo mnunuzi Datistani Mwanshinga alibatilisha ununuzi wa nyumba hiyo Mei 9, Mwaka huu baada ya kukiri kurejeshewa fedha zake.

HATIMAYE BABA ALIYETELEKEZA WATOTO AKAMATWA.

Kamanga na Matukio | 04:54 | 0 comments
Watoto  Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakifanya usafi katika nyumba wanayoishi 

Hapa ndipo wanapopikia chakula wakati wa usiku  kwakweli ni hali ya hatari sana

Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akiwa na watoto hao alipowatembelea nyumbani mara baada ya kuwakosa shuleni mwandishi wetu alipowauliza kwanini hamjaenda shule leo? wakamjibu tulijua leo ni sikukuu ndiyo maana hatujaenda shule,


Hapa wakinawa kutokana na hali ya uchafu waliokuwanayo baada ya kumaliza kufanya usafi nyumba yao


Wakiwa na waalimu wao

Hapa mwandishi wetu Joseph Mwaisango akiwarudisha nyumbani watoto hao mara baada ya maongezi mafupi na waalimu waoJESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Steven Julias mkazi wa Jakaranda kata ya Iyela Jijini Mbeya akituhumiwa kutelekeza familia kwa miezi mitano bila huduma za msingi ikiwemo chakula na sare za shule.

Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumethibitishwa na mwenyekiti wa dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Mary Gumbo ambaye alisema walimkamata Oktoba 11, mwaka huu eneo la nyumbani kwake alikokuwa amewatelekeza watoto hao.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa anafanya maandalizi ya kuwatorosha watoto hao ili kukwepa mkono wa sheria dhidi yake baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa anatafutwa kukabili kesi iliyombele yake.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa uchunguzi unafanyika ili kesi iweze kufunguliwa na hatimaye kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vikomeshwe.

Wakati huo huo maisha wanayoishi kwa sasa watoto hao  Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza  shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya maisha ya kujipikia bila huduma za msingi wasamaria wema wameombwa msaada wao wa hali na mali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema hivi sasa wanaishi kwa misaada kutoka kwa walimu na baadhi ya watu ambao huwapa unga na maharage na wao hulazimika kutafuta fedha za kununulia mahitaji mengine kama mafuta ya kula na taa.

Wametaja baadhi ya mahitaji yao muhimu kwa sasa kuwa ni pamoja na Sare za shule kutokana na kuchakaa kwa sare wanazotumia ikiwemo Madaftari, kalamu,Masweta, Viatu, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, sabuni, chumvi, mkaa, Unga, Mchele na maharage.

Aidha imeshauriwa kuwa kutokana na mazingira wanayoishi watoto hao kutokuwa mazuri kwa utunzaji wa vyakula ambapo nyumba wanayoishi kutokuwa na mlango vitu hivyo vihifadhiwe Ofisini Kwa Mwalim Mkuu kama vitapatikana.

Kwa yeyote atakayekuwa ameguswa na hali ya watoto hao awasiliane na Mbeya Yetu kupitia namba 0754 374 408
 au Bomba Fm redio kupitia 0754 490 752.

Na Mbeya yetu
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger