MAHABUSU MWINGINE ALIYETOROKA BAADA YA KUCHIMBA UKUTA AKAMATWA.

Kamanga na Matukio | 01:51 | 0 comments
 
 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.

Vasco Lwenje (28) mkazi wa Songwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya mmoja wa wahabusu wanne waliotoroka kwa kuchimba ukuta wa Kituo Kuu cha Polisi cha Kati Machi 22 mwaka huu amekamatwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Advocate Nyombi, amesema mtuhumiwa amekamatwa katika nyumba ya Bwana Reuben Sanga mkazi wa Iwindi nje kidogo ya mji mdogo wa Mbalizi, majira ya saa nne usiku Machi 29 mwaka huu alikoomba hifadhi.

Amesema kupatikana kwa Lwenje ni juhudi za jeshi lake pamoja na ushirikiano wa kiintelejinsia baina ya jeshi hilo na wananchi hadi kufanikisha kukamatwa mahabusu watatu kati ya wanne waliotoroka kwa muda wa juma moja tu.

Kamanda Nyombi ameongeza kuwa amesalia mahabusu mmoja aliyemtaja kwa jina la Jonas Jackson (28), mkazi wa Tunduma na mwenyeji wa Mbozi ambapo pamoja na Lwenje walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.

Aidha amesema kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa Jonas Jackson, jeshi lake litatoa zawadi nono kwani pamoja na wengine waliorejeshwa mahabusu ni watu hatari sana.

Lwenje alikuwa kwenye nyumba ya Mzee Sanga ambako alipewa hifadhi na mzee huyo ambapo waliwahi kukutana gerezani, alipokuwa kifungoni kabla ya kuachiwa.

Hata hivyo Kamanda Nyombi amebainisha kuwa kukamatwa kwa Lwenje kunafanya jumla ya waliokamatwa kufikia watu watatu na kwamba mbali ya makosa ya mauaji watakabiliwa na kosa la kutoroka chini ya ulinzi wa dola.

AIBA KUKU NA KUAMRISHWA KULA KINYESI CHABINADAMU NA KUACHIWA HURU.

Kamanga na Matukio | 01:46 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mkazi mmoja wa Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini Bwana Musa Mwambapa (25), amelazimishwa kula kinyesi cha binadamu baada ya kukamatwa ameiba kuku katika Kijiji cha Sisitila, Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea jana Machi 30 mwaka huu, majira ya saa nne asubuhi katika kijiji hicho pale mtuhumiwa alipoiba kuku mali ya Bwana Vedastus Jerome (45).

Baada ya mtuhumiwa kukamatwa wananchi wenye hasira kali walimtaka achague adhabu moja kati ya mbili, ambazo ni kumwagiwa mafuta ya petroli kisha kuchomwa moto au kula kinyesi cha binadamu ambapo bila kinyaa alichagua kula kinyesi cha binadamu kisha akaachiwa.

Hata hivyo juhudi kuwatafuta viongozi wa Kijiji hicho akiwemo balozi na Mwenyekiti wa kijiji hicho kugonga mwamba kwa vile walikuwa wamekwenda msibani eneo la Mbalizi na hazikuweza kupatikana hewa.

SOLAR POWER ILIYOZINDULIWA NA RAIS KIKWETE YAIBIWA.

Kamanga na Matukio | 01:44 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Halungu, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina moja la Mkoma, ametoroka baada ya Solar ya umeme wa jua iliyotolewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kutengenezea hati za kimila kwa ajili ya kumiliki ardhi kijijini.

Mradi huo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2010, umejikuta ukikwama kutokana na kuibiwa kwa solar hiyo ambayo ilikuwa na uwezo wa kuendesha kompyuta iliyokuwa ikitunza nyaraka za hati za kijiji cha Halungu na Ipunga wilaya ya Mbozi, ambavyo vilikuwa mfano Mkoani hapa na chini kwa ujumla.

Naye, Diwani wa Kata ya Halungu Mheshimiwa Samson Simkoko amesema kupotea kwa solar hiyo ni pigo kubwa kwa Kijiji na Kata yake kwa ujumla kutokana na masjala hiyo kusaidia wananchi kupata hati za ardhi kijijini hapo badala ya kufuatilia Mkoani na Wizarani.

Ameongeza kuwa dada ya solar hiyo kuibiwa Halmashauri ya Wilaya hiyo iliamua kuchukua kompyuta iliyokuwepo kijijini hapo na kuipeleka katika ofisi za Halmashauri na hivyo kwa sasa hakutakuwa na shughuli za upimaji na umilikishwaji wa ardhi kwa njia ya kimila hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi.

Diwani Simkoko amesema baadhi ya wananchi walianza kupata manufaa kwenye Asasi za fedha ambazo zimekuwa zikizikubali hati hizo kwa ajili ya mikopo.

WANANCHI WAIKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA KIJIJI CHAO - MBOZI.

Kamanga na Matukio | 01:43 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Wananchi wa Kijiji cha Hampangala, Wilayani ya Mbozi, Mkoani Mbeya wameikataa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji, iliyosomwa na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Saston Mkondya Februari 24 mwaka huu.

Hata hivyo pamoja na kukataliwa kwa taarifa hiyo Mtendaji huyo aliamua kutengeneza muhtasari wa kugushi na kuupeleka katika ofisi mbalimbali zikiwemo ya diwani na halmashauri ya mji, ambapo alihalalisha mkutano huo ambao ulimalizika kutokana na kukosekana kwa amani.

Aidha baadhi ya wananchi wamesikitishwa na tabia ya Afisa utumishi wa wilaya, baada ya kuendelea kumkingia maovu mtumishi wake, ambaye amekiri kugushi muhtasari hali iliyopelekea wananchi hao kuifunga ofisi hiyo Machi 16 mwaka huu, kufuatia kuchoka na kuchoishwa na vitendo vya mtendaji huyo.

Katika uchunguzi umebaini kuwa kutokana na sakata hilo Mkuu wa wilaya ya hiyo Bwana Gabriel Kimoro, atafanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

WAHAMIAJI HARAMU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

Kamanga na Matukio | 01:40 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Raia 7 wa nchi ya Somalia na mmoja wa nchi ya Kenya wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Rahim Mushi, kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi Staff Sajent Amin Rajab, ameiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Machi 25 mwaka huu raia hao walikamatwa Mji mdogo wa Tunduma na kufikishwa mahakamani Machi 26 mwaka huu.
 
Ameongeza kuwa kesi hiyo namba 56, raia hao wamefanya kosa hilo kinyume cha sheria kifungu cha 31:1(i) na kifungu cha 2 cha sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995, ambapo amewataja wahamiaji hao kuwa ni pamoja na Salad Yusuph(20), Abdillah Abdi(20), Mohammed Idd Hussein(20), Mohammed Ahmed Abdi(13) na Ahmed Athuman(22).

Wengine ni Abdirizack Abdlahaman(19), Nuru Yusuph Ally (35) wote ni wakazi wa Mogadishu nchini Somalia na Ibrahim Ally(30), mkazi wa Nairobi nchini Kenya.

Hata hivyo kesi hiyo itatajwa tena April 10 mwaka huu na washtakiwa wapo mahabusu .

RC MBEYA AWATAKA MAAFISA ELIMU, KUHAKIKISHA WALIMU KWENDA MASOMONI KWA AWAMU.

Kamanga na Matukio | 01:38 | 0 comments

Habari na mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka maafisa elimu wa shule za msingi na Sekondari kuhakikisha wanaandaa mpangilio maalumu utakao wawezesha walimu kwenda masomoni kwa awamu.

Ametoa agizo hilo baada ya kuwepo kwa upungufu mkubwa ya waalimu waalimu katika shule za msingi na sekondari ambao unachangiwa na idadi kubwa ya waalimu kwenda masomo bila ya mpangilio.

Amesema taarifa ya waalim 6 kati ya kumi wa shule moja kupewa ruhusu ya kwenda masomoni imechangia kwa kiasi kikibwa kuongeza upungufu wa waalimu.

Wakati huohuo amewataka viongozi wa kisiasa na wazazi kushirikiana kujenga nyumba za waalimu na kuongeza kuwa uwepo wa waalimu jirani na maeneo ya shule husaidia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya shule elimu kwa wanafunzi.

WALIMU WAANDAMANA WAKIDAI MALIMBIKIZO YA MISHAHARA NA POSHO JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 01:34 | 0 comments

Habari na mwandishi wetu.
Waalimu wa ajira mpya wa shule za msingi na Sekondari jijini Mbeya hivi karibuni wameandamana hadi Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji, wakidai madai ya malimbikizo ya mshahara wa mwezi wa pili na watatu.

Wakiowa nje ya Ofisi hiyo waalimu hao wameyataja madai yao kuwa ni Mshahara, fedha za usafiri, fedha za kujikimu na huduma za msingi.

Aidha wameomba kuondolewa kwenye chama cha waalimu Tanzania kutokana na wao kuandikishwa uanachama na kukatwa mshahara wao pasipo ridhaa yao.

Hata hivyo mkurugenzi hukuweza kukutana nao kwa kuwa alikuwa katika kikao cha wadau wa elimu mkoani mbeya.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote kuhakikisha wanaandaa mipango madhibuti itakayowezesha kumaliza tatizo la madai ya waalimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila mwajiliwa mpya analipwa stahiki zake mapema.

UJENZI WA SOKO LA KISASA MKOANI MBEYA WASUA SUA.

Kamanga na Matukio | 01:30 | 0 comments
Habari na Bomba FM, Mbeya.
Umoja wa wafanyabiashara katika soko la mwanjelwa jijini mbeya wamelalamikia kutokamilika kwa soko hilo.

mwenyekiti wa umoja huo Charles Syonga amesema muda ulioongozezwa wa miezi sita umekamilika mwezi Februari mwaka huu lakini hakuna dalili za kukamilika kwa soko hilo.

aidha amesema kumekuwepo kwa taarifa za ugawaji wa siri wa vyumba vya biashara ndani ya soko hilo na kuzua kwa malamiko kutoka kwa wafanyabiashara wengine.

Naye katibu wa umoja huo Janson Mtupwa amesema kutokana na hali hiyo wafanyabiashara hao wanalazimika kulipa riba za mikopo bila ya kuwa na uzalishaji unaofaa.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dokta Samweli Lazaro amesema hakuna ugawaji wa vyumba vya biashara ndani ya soko hilo na kuongeza kuwa taarifa za ugawaji wa vyumba hivyo itatolewa kupitia matangazo.

WALIMU 50 WALALA CHUMBA KIMOJA WAKIDAI MAFAO YAO WILAYANI MBOZI – MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:30 | 0 comments

 Mmoja wa walimu waliokuwa na watoto wao na hivyo kulazimika kulala wima huku wakiwa wamewapakata, wakati wa madai ya mafao yao ya pesa za nauli, posho na mishahara yao ya miezi miwili, na katika hali isiyoyakawaida mtumishi mmoja wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi alimtamkia kuwa mtoto hana baba yake mpaka anaenda naye katika Ofisi za halmashauri hiyo..
Baadhi ya walimu kutoka katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari wilayani Mbozi, wakiwa nje ya Ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo wakisubiria pesa za nauli, mishahara na posho ambazo hawajalipwa kwa takribani miezi miwili mpaka sasa.
 Walimu tuna hali ngumu maisha yetu yamewekwa rehani kwenye maduka na Maafisa watendaji wa Kijiji, ambao wamekuwa wakitukopesha pesa za kujikimu.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Zaidi ya walimu 50 waliopata ajira mpya hivi karibuni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya wamejikuta wakilala chumba kimoja baada ya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya hiyo kufungwa huku walimu hao hawajapata sitahili zao.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea kwa siku mbili mfululizo, baada ya walimu hao waliotokea maeneo tofauti tofauti wilayani humo na baada ya kufika katika Ofisi hizo za Halmashauri hawakuweza kupata stahili zao kama vile pesa za kujikimu, nauli na mishahara kwa muda wa miezi miwili mpaka sasa.

Mnamo Machi 6 mwaka huu, walimu hao walimuona Mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Gabriel Kimoro ambapo walilipwa posho ya shilingi laki moja (100,000) kwa kila mmoja kwa ahadi ya kuwa mwishoni mwa mwezi stahili zao zote zingelipwa, lakini mambo yalikuwa tofauti Machi 27 na 28 kwani madai yao yalikuwa hayajashughulikiwa.

Kiongozi wa walimu hao Mwalimu Carlos Magoyo amesema baada ya maafisa wa halmashauri kutawanyika waliamua kulala katika ofisi hizo za Mkuu wa wilaya kwani walikuwa hawana pesa za nauli na kujikimu, kabla ya kutokea msamaria mwema aliyewapa chumba hicho kimoja na kuchanganyika jinsi zote huku wakiimba pambio na kutafuna mahindi ya kuchoma.

Aidha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bwana Levson Chilewa amesema madai yao ya posho yanaanza kushugulikiwa mara moja na Ofisi ya fedha ya halmashauri hiyo lakini kuhusiana na mishahara yao ipo nje ya uwezo wake kwani suala hilo linashughulikiwa na Serikali kuu yaani Hazina kuu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Bwana Kimoro ameahidi kufuatilia madai hayo kwa ukaribu zaidi na amesikitishwa kwa kitendo hicho cha kucheleweshwa mishahara kwani baadhi ya walimu wanatoka mbali na mji wa Vwawa na asingependa kuona walimu wakiishi maisha ya kuombaomba.

Naye, Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bwana Juma Kaponda amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba atawasiliana na Mkurugenzi wa wilaya hiyo ili walimu hao walipwe mapema iwezekanavyo, ingawa kwa sasa yupo safarini kikazi nje ya mkoa.

Baadhi ya walimu walionekana wakiwa na watoto wadogo na baadhi yao wamekesha wakiwa wamewapakata watoto wao kutokana na kukosa eneo la malazi sambamba na kukosa hata chakula cha watoto ambao wapo chini ya umri wa miaka miwili.

SERE MBOVU ZA CCM ZIMECHANGIA KUONGEZEKA KWA UMASIKINI ULIOKITHIRI KWA WANANCHI VIJIJINI - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:06 | 0 comments

Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zuberi Zitto Kabwe amesema sera mbovu za Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechangia kuongezeka kwa umasikini uliokithiri kwa wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini. 

Zitto amesema hayo jana wakati wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani kupitia CHADEMA, Laurent Mwakalebule katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kiwira uliofanyika katika mji wa Kiwira Rungwe.

Amesema kuwa licha ya Serikali kutangaza kukua kwa  uchumi wa nchi kila mwaka, idadi ya watu masikini inazidi ongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na taarifa ya Serikali ya maendeleo ya uchumi inaonyesha kuwa mwaka 2007 watanzania milioni 11 walikuwa masikini wa kutupwa na kuwa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia milioni 14 kwa mwaka jana.

Amesema kuwa iwapo Watanzania hawataamka sasa kwa kukiondoa Chama Cha Mapinduzi(CCM) madarakani,basi idadi ya masikini itaongezeka mara dufu katika miaka michache ijayo kwa kuwa umasiki wa watanzania unasababishwa na sera mbovu za chama hicho.

Zitto amewataka wakazi wa Kata ya Kiwira kuanza kuleta mabadiliko hayo kwa kumchagua mgombea wa Chadema, ili akasimamie na kutetea maslahi ya wananchi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

BREAKING NEWS:- WALIMU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MBOZI WAANDAMANA KUDAI MAFAO YAO & MTOTO AZIKWA KISIMANI.

Kamanga na Matukio | 05:01 | 0 comments
1. *Walimu wakesha chumba kimoja wakifuatilia mafao yao Wilayani Mbozi.
* DC, Mkurugenzi na Afisa Utumishi wawakimbia.
 *Walimu wasema hawaondoki mpaka kieleweke.

2 *Mtoto azikwa kisimani baada ya kushindikana kwa juhudi za kumwokoa Wilayani Kyela.

*****Kwa habari zaidi usikose kutembelea mtandao huu*****

 

YALIYOJILI KATIKA SIKU YA MAADHIMISHO YA KIFUA KIKUU DUNIANI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:33 | 0 comments
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, akihutubia katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu duniani yaliyofanyika kiwilaya Kata ya Iwindi Mbeya Vijijini.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama,akikagua moja ya mabanda ambayo huduma ya vipimo vya ugonjwa wa Kifua Kikuu ilikuwa ikitolewa.
Bwana Weston Asisya wa Asasi ya MMRP akisisitiza moja ya ujumbe wa mwaka huu.
Wananchi wa Kata ya Iwindi na vitongoji jirani wakisubiri kupatiwa huduma ya vipimo vya ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Dr Erica Sanga wa MMRP na Weston Asisya wakieleza jinsi taasisi hiyo ya utafiti wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu na mafanikio yaliyopatikana kutokana miezi 8 ya awali katika tiba na sasa ni miezi minne na kutaka wananchi wajitokeze kwa wingi katika Ofisi za taasisi hiyo kwani wanaboresha tiba siku hadi siku.
Kitokomeza ugonjwa wa Kifua kikuu.
Burudani safi zilitolewa na vikundi mbalimbali, lakini pichani ni Kikundi cha Nyota Mbalizi kikitoa burudani ya Sarakasi.
 Wanafunzi nao walikuwa mstari wa mbele wakisubiri kupewa huduma ya vipimo vya Ugonjwa wa Kifua kikuu. (Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)

ASHITAKIWA KWA WIZI - MBOZI

Kamanga na Matukio | 04:29 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Mwananchi mmoja Enn Sichone (22) mkazi wa Old Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya, amefikishwa mbele ya mahakama ya mwanzo kujibu shtaka la wizi.

Akisoma shtaka hilo mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo PC Lugano Mwampulule, mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Ismael Karuta amesema mshtakiwa ametenda kosa hilo Machi 13 mwaka huu majira ya saa 12 kamili jioni.

Mtuhumiwa aliiba starter moja ya gari, radiator 2 za gari zinazomilikiwa na Bwana Said Salum wa Vwawa vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki nane(800,000/=).

Hata hivyo mshtakiwa Enn amekana kutenda kosa hilo na keshi hiyo imeahirishwa hadi April 10 mwaka huu na hivyo kurejeshwa mahabusu kutokana na kukosa wadhamini.

AUAWA KWA WIZI WA PIKIPIKI - MBEYA VIJIJINI

Kamanga na Matukio | 04:28 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya Vijijini.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ford Mwakambonja (41) mkulima na mkazi wa Nyalwela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kuiba pikipiki.

Tukio hilo lemetokea majira ya saa tisa alasiri katika Kijiji cha Kimondo wilayani humo, ambapo kundi la wananchi walimkamata marehemu akiwa na pikipiki aliyoiiba mali ya Bwana Pius Jonas, kisha kumpika na kumuua papo hapo.

Wananchi hao hawakuishia hapo baada ya kumuua Ford na mwili wake kuuteketeza kwa kuuchoma moto na pikipiki aliyoiiba ikihifadhiwa katika Ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Kimondo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Hata hivyo wimbi la wizi wa pikipiki limekithiri Mkoani Mbeya, ambapo baadhi ya madereva wameporwa na kuuawa hali inayowatia hasira wananchi pindi wanapowakamata wahalifu wa wizi huo.

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUYARUSU MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA ZAO LA PARETO ILI KULETA USHINDANI WA BEI - MAKETE

Kamanga na Matukio | 04:27 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi, Njombe.
Wakulima Wilayani Makete Mkoani Njombe wameiomba Serikali wilayani humo kuyaruhusu makampuni mbalimbali ya ununuzi wa zao la Pareto yaliyopata vibali ili kuleta ushindani wa bei ya zao hilo kwa manufaa ya mkulima.

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Kata za Ipelele na Iniho wamesema kuwa miaka miwili iliyopita kulikuwa na mnunuzi mmoja ambaye ni Kapuni ya Pareto Tanzania(PCT) yenye makao yake makuu mjini Mafinga,mkoani Iringa.

Wamesema kuwa bei ya pareto kwa kilo moja walikuwa wakiuza kati ya shilingi 1200 hadi 1600 kabla ya kupanda bei ambapo kwa sasa wanauza shilingi 1800 kwa kilo moja katika kapuni ya PCT.

Augustino Fungo mkazi wa Kijiji cha Ipelele amesema kuwa katika msimu wa mwaka huu wamefurahishwa sana baada ya kuona kampuni nyingine imejitokeza kwenda kununua pareto katika kijiji hicho.

Amesema kuwa kampuni hiyo aliyoitaja kwa jina la KATI Enteprises Ltd. imekuwa ikimlipa mkulima shilingi 2,000 kwa kilo moja jambo ambalo hapo awali lisingewezekana kutokana na kutokuwepo kwa kampuni mshindani wa PCT ambao walikuwa wakipanga bei wanayoitaka wao kwa lengo la kujinufaisha wao na si mkulima.

Aidha,ameiomba serikali kuweka mfumo mzuri wa upatikanaji wa mbegu za pareto sambamba na pembejeo nyingine za kilimo ambazo hazimfikii mkulima kwa wakati.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ipelele Anna Sanga amesema kuwa kuwapo kwa makampuni mengi kunasaidia kupanda kwa bei ya pareto kwa kilo ambapo alitolea mfano wa shilingi 1800 kwa kilo bei iliyokuwepo hapoa awali ambapo baada ya kampuni nyingine kujitokeza na kununua shilingi 2000 kwa kilo kumekuwa na ushindani hivyo wale wa awali kupandisha bei hadi shilingi 2050.

Ameshauri serikali kutengeneza miundombinu ya barabara ambayo hivi sasa ni chakavu sana hali inayosababisha wakulima hao kukosa soko la uhakika kutokana na barabara hizo kutopitika kwa urahisi na magari hivyo kujikuta mazao yao yakiozea mashambani ama majumbani.

Awali Mkuu wa Wilaya hiyo, Zainabu Kukwega amewaambia waandishi wa habari kuwa kampuni ya PCT imeingia mkataba na wakulima Wilayani hapo hivyo hakuna kampuni nyingine iliyoruhusiwa kununua pareto wilayani humo na wale ambao wamejaribu kufanya hivyo tayari wamekwisha andikiwa barua ya kusimamishwa kununua Pareto wilayani humo licha ya kuwa na vibali halali vya kununulia zao hilo.

WIMBI LA UBAKAJI LABEBA SURA MPYA, ABAKA MTOTO WA MIAKA MIWILI – MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:04 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi la ubakaji kwa watoto mkoani Mbeya limechukua sura mpya baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Ikukwa, Wilaya ya Mbeya Vijijini kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka miwili bila huruma.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana Machi 24 mwaka huu, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Manase (30) kumbaka mtoto baada ya kumrubuni mtoto na kwenda naye nyumbani kwake na kisha kufanyia ukatili huo.

Baada ya kusikika kwa kelele chumbani kwa Manase, wananchi walifuatilia na kukuta mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya , ambapo walimkamata mbakaji huyo na kumpeleka Kituo cha Polisi Kati kilichopo Jijini Mbeya .

Hata hivyo mtuhumiwa anashikiliwa Kituoni hapo na Jeshi la Polisi na wakati wowote atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika..

Wakati huohuo mtoto aliyebakwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini hapa, akipatiwa na matibabu na uchunguzi wa kitendo hicho umebaini kuwa ni imani za kishirikiana.

KITUKO:- ALISHWA KINYESI MBELE YA MKEWE.

Kamanga na Matukio | 05:03 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wawili wakazi wa Kijiji cha Isansu, Kata ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya wanakabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru kwa kumlisha vinyesi vyao mkazi mmoja wa mtaa hao mbele ya mkewe.

Washtakiwa hao ni pamoja na Joseph Kalinga na Ephrem Chisunga wakazi wa kijiji hicho na kosa hilo walimtendea Bwana Musa Kilalawima (42).

Mwendesha mashtaka wa Polisi PC Lugano Alfred Mwampulule amesema watuhumiwa walitenda kosa hili majira ya saa nane mchana kwenye bustani ya mlalamikaji.

Mlalamikaji wa kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi wilayani humo Bwana ilisomwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Vwawa Martha Malimi, ambapo mlalamikaji Bwana Musa aliiambia mahakama kuwa mnamo Machi 10 mwaka huu akiwa shambani na mkewe, watuhumiwa Joseph Kalinga na Ephrem Chisunga walimkamata na kisha kujisaidia vinyesi vyao.

Watuhumiwa wakiwa wameshika mapanga walimchukua mlalamikaji na kumpeleka mtoni na kumtaka asali sala ya mwisho kabla ya kuuawa huku mkewe akilia kwa uchungu, ndipo wakaanza kumlisha vinyesi hivyo kila mmoja kwa wakati wake na vingine wakimsiliba kichwani na sehemu mbalimbali, huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa chuma na kamba.

Huku wakiendelea na ukatili huo mkewe wa mlalamikaji alifanikiwa kuwatoroka na kuendelea kupiga kelele, ndipo walimchukua Mussa hadi kijijini na kumtembeza mtaani hapo huku mwili mzima ukiwa umetapakaa kinyesi.

Mlalamikaji huyo amedai mahakamani hapo kuwa baada ya kuachiwa na watesaji haoa alitoa taarifa kwa Mjumbe wa mtaa aitwaye Julius Nyingi, ambaye naye alimtaarifa Mwenyekiti wa mtaa huo Rais Mwampashi, ambaye alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Vwawa na kufanikiwa kumkamata Joseph ambapo Ephrem alifanikiwa kutoroka.

Kwa upande wake mwendesha mashtaka PC Mwampulule amesema kosa hilo ni kosa la jinai kifungu cha 21 sura ya 16, cha kanuni ya adhabu cha mwaka 2002.

Hata hivyo mahakama hiyo ilikataa ombi la dhamana kwa mshtakiwa ambapo imedaiwa kuwa mtuhumiwa ana makosa mengine ya kujibu.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka April 10 mwaka huu, mlalamikaji atakapo leta mashahidi wake huku sheria ikiangalia ni kifungu gani sahihi cha sheria ya mtu kulishwa kinyesi, ambapo jalada la kesi hiyo limepelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili ajaribu kuchambua.

Wakati huohuo watoto wawili John Mtawa (16) na Daniel Mwandingo (14), wamefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kuvunja na kuiba bidhaa kibandani kwa Tizo Mwasonga majira ya saa 5:00 usiku,  na kuiba tray 10 za mayai na viazi mviringo vyote vinathamani ya shilingi 91,000.

Mwendesha mashtaka wa Polisi PC Mwampulule, ameiambia mahakama hiyo chini ya hakimu Halima Malimi kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 256 cha kanuni ya adhabu.

Watuhumiwa walitenda kosa hilo Machi 24 mwaka huukatika mtaa wa Ilembo wilaya ya Mbozi, ambapo watuhumiwa hao wamekana kutenda kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa mpaka April 11 mwaka huu na watuhumiwa wamepewa dhamana.

MTUHUMIWA ALIYETOROKA MAHABUSU AKAMATWA

Kamanga na Matukio | 04:59 | 0 comments

Kituo cha Polisi Kati kilichopo Jijini Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Maneno Wiwa Kalinga mmoja wa mahabusu waliotoroka wiki iliyopita katika Kituo cha Polisi Kati, Mkoani Mbeya amekamatwa akiwa mafichoni Wilayani Mbozi.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa majira ya saa 10 alfajiri katika kijiji cha Ruanda wilayani humo.

Kukamatwa kwake kumetokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi la polisi  mkoani hapa, mara baada ya kutoroka kwa kuchimba ukuta wa Kituo hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kukamatwa kwa mahabusu huyo na kufanya jumla ya waliokamatwa kufikia wawili, huku mwenzake  Fadhili Mwaitebele (27) makazi wa Ilomba jijini Mbeya alikamatwa muda mfupi baada ya kutoroka.

Hata hivyo Kamanda Nyombi ametoa wito kwa wananchi kuwa popote watakapo waona wahalifu hao watoe taarifa kituo chochote cha Polisi kwani watu hao ni hatari katika jamii.

MTOTO ABAKWA NA ASKALI KISHA AFUNGIWA NDANI KWA MUDA WA SIKU TATU - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 06:11 | 1comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Askali mmoja aliyefahamika kwa jina la utani Zungu ,mkazi yake mji mdogo wa Mbalizi jirani na Shule ya Sekondari Samaritan amembaka mtoto mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya msingi Swaya Ntokela wilaya ya Rungwe.

Tukio hilo limetokea Machi 16 hadi 19 mwaka huu, ambapo mwanafunzi huyo amekatizwa masomo Machi 14, alipoenda kuchukuliwa na mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Bi. Maida Ngulo ambaye ni mke wa askali huyo kwa nia ya kuwa mfanyakazi wa ndani.

Bi Maida alisafiri Machi 16 mwaka huu kuelekea Tukuyu na kumuacha mtoto huyo akiwa na Askali huyo(mumewe), ndipo usiku baada ya mtoto huyo kumaliza kumuandalia chakula askali huyo akitokea ulevini alimkamata binti(mtoto) huyo na kumbaka na kumjeruhi vibaya na kumfungia ndani kwa muda wa siku mbili, ambapo alijisahau kufunga mlango na mtoto huyo kutumia fursa ya kutoroka.

Lakini kutokana na ugeni mtoto huyo alikosa mahali kwa kwenda na kutokana na kitendo cha kubakwa alikuwa akishindwa kutembea na kuokotwa na msamalia mwema aitwaye Bi Lilian Costa na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbalizi, ambapo alichukuliwa PF3 na kukimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya kupima na mtoto huyo kugunduliwa amebakwa.

Aidha, Bi Lilian alirudisha taarifa Kituo cha Polisi  kuwa mtoto huyo kabakwa, ndipo juhudi za kumtafuta askali huyo kazini kwake kutokana na kitendo cha ukatili alioufanya hakuweza kufika kazini kwake na ametoweka nyumbani kwake pamoja na mkewe na simu ya mkewe imekua ikiita bila kupokelewa.

Hata hivyo mtandao huu unafuatilia kumrejesha mtoto huyo Shule ya Ntokela, ambapo pia inadaiwa jina lake limeuzwa kwa mtu mwingine na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, kutokana na mtoto huyo kutoonekana shuleni kwa muda baada ya mama yake kuumwa na ndipo walipotumia mwanya wa kumtorosha na kuja kufanya kazi za ndani.

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA, MAHABUSU WACHIMBA UKUTA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KISHA KUTOROKA.

Kamanga na Matukio | 05:44 | 0 comments
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi, akiwa ameketi ofisini kwake.
 **********
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira kali katika Kijiji cha Myunga, Wilaya ya Momba (Jimbo la Mbozi Magharibi) mkoani Mbeya.

Majambazi hayo yameuawa usiku wa manane yalipokwenda katika kijiji hicho kwa nia ya kutekeleza mauaji kwa diwani wa Kata ya Myunga (CHADEMA) mheshimiwa Godfrey Siame, ambapo waliahidiwa kupewa milioni mbili.

Majambazi hayo yakiwa na silaha mbili aina ya shortgan na bastola walipofika kijijini hapo na kisha kumrubuni Diwani huyo kuwa wanataka kudanya naye biashara, ndipo aliwashitukia kuwa ni majambazi wakati  yeye akiwa Tunduma baada ya mtego  wakati wakitoka katika nyumba moja ya kulala wageni kwa ajili ya kutekeleza azma yao walikamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuanza kupingwa hadi kuuawa.

Wakati huohuo usiku wa kuamia jana mahabusu wanne waliokuwa katika mahabusu ya polisi Kituo Kikuu cha Kati Mbeya wametoroka baada ya kufanikiwa kuchimba ukuta wa vyumba vya mahabusu bila Askari waliokuwa zamu kujua.

Askari hao walifanya ukaguzi majira ya saa nane usiku saa tisa usiku wakabaini mahabusu hao hawapo baada ya kuchimba moja ya ukuta kisha kutokomea gizani na kuwaacha Polisi wakiwa katika lindo.

Mbinu iliyotumika ni kuloanisha ukuta kwa kutumia maji yaliyopo bafuni na vipande viwili vya nondo ambavyo walivitumia kuuchimba ukuta huo kwa urahisi licha ya kujengwa kwa matofari ya saruji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio yote wawili na kwamba mahabusu watatu walikuwa wanakabilisha na kesi za mauaji na mmoja kesi ya wizi.

Hata hivyo amesema Jeshi lake limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye ni Fadhili Mwaitebele (27), mkazi wa Ilomba jijini Mbeya ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa wizi.

MAJERUHI WA TUKIO LA MAPIGANO YA CHILULUMO, WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:43 | 0 comments
 Mmoja wa wananchi waliojeruhiwa kwa kipigo kufuatia mapigano yaliyozuka katika Kijiji cha Chilulumo Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Bwana Daudi Sikali.
Mabinti waliodhalirishwa kijinsia baada ya kubakwa na watu saba walionadaiwa kushinikizwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilulumo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Bwana Bruno Chipungu, huku wakishikiwa mashoka kutenda ukatili huo wa ubakaji kwa mambinti.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilulumo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Bwana Bruno Chipungu amefikishwa mahakamani kujibu kosa la kutishia kuua Machi 12 na 15 mwaka huu kijijini hapo.

Mtuhumiwa huyo alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Rahim Mushi, ana mwendesha mashtaka mkaguzi wa Polisi (PP) John Mazwile March 21 mwaka huu.

Akisoma shtaka mwendesha mashtaka huyo amesema mtuhumiwa aliteka kosa hilo la kutishia kuua kinyume cha sheria, kifungu cha 89 sura ya 16 cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.

Mwenyekiti huyo (mtuhumiwa) na uongozi wa kijiji hicho wanatuhumiwa kuwa vinara katika mgogoro kijijini hapo na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa na mabinti watatunkubakwa, kuharibiwa mali na wengine kuchomewa nyumba zao hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kuishi uhamishoni kwa hofu ya kuawa.

Aidha, PP Mazwile alizuia dhamana kwa mtuhumiwa na hivyo kwenda mahabusu hadi, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo mwenzi ujao na mpaka sasa watuhumiwa wanne wamefikishwa mahakamani hapao kutokana na vurugu zilizozuka kijijini hapo.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi mkoani hapa, linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mariam mkazi wa Mwanjelwa jijini Mbeya, baada ya kummwagia maji ya moto Joseph Simfukwe (35).

Tukio hilo limetokea Machi 21 majira ya saa 2;30 usiku ambapo, Bwana Simfukwe alikwenda kwa Mariam kufuatilia sahani zake alizokuwa akizitumia katika biashara yake ya kuuza chipsi ndipo binto alimdai deni lake la shilingi mia nne, alipomwambia atampatia baadae ndipo aligadhibika kisha kuchukua maji ya moto na kummwagia Josephat, mwilini huku akiporomosha matusi mazito huku Josephat akianguka chini chini kwa maumivu makali.

Josephat amejeruhiwa vibaya mwilini na amelazwa katika Hospitali ya  Rufaa jijini Mbeya wadi namba 1 akipatiwa matibabu.

Aidha Julius Mkela mkazi wa Ifumbo Chunya amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa kisha kuporwa dhahabu na pesa taslimu ambazo idadi yake haijafahamika usiku wa Machi 18 mwaka huu, ambpo majambazi walivamia nyumbani kwake na kumlewesha kwa madawa na kuanza kupekua kila eneo na kufanikiwa kuchukua dhahabu kiasi kikubwa na pesa taslimu kisha kutokomea na kumwacha Julius Mkea akiwa hajitambui.

Diwani wa Kata ya Ifumbo Michael Zanzi amethibitisha kutokea kwa tukio hili na kwamba wameripoti kituo cha Polisi na mpaka sasa Mkea amelazwa.

RC MBEYA AOMBWA KUINGILIA KATI MGOGORO ULIOPO KATI WANANCHI NA SHULE YA SEKONDARI NDEMBELA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:42 | 0 comments


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), baada ya kumaliza mbio zake mkoani Rukwa.
****** 
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Wananchi wa kijiji cha Ndembela, Kata ya Makandana Wilayani Rungwe wamemwomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kuingilia kati mgogoro uliopo kati ya wananchi wa Kijiji hicho na shule ya sekondari Ndembela inayoendeshwa na Kanisa la Waandiventista Wasabato(SDA) iliyopo kijijini hapo,uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 sasa.

Katika malalamiko yao waliyoyatoa juzi mbele ya Mkuu wa Mkoa, wananchi hao wamedai kuwa Kanisa hilo la Wasabato limewapora ardhi na majengo ya shule ya Sekondari Ndembera kinyume na matakwa yao, hivyo wamemwomba kandoro kuwasaidia kuirejesha mikononi mwao.

Baadhi ya wananchi waliopata nafasi ya kueleza wamesema kuwa katika miaka ya 1980 wakati shule hiyo ikiwa inatoa elimu ya msingi pekee, kulionekana kuwepo na mahitaji ya shule za sekondari na ndipo wakaamua kuibadilisha kuwa shule ya sekondari.

Aidha,baada ya uamuzi huo kupitishwa, Kanisa la Wasabato liliomba kuiendesha shule hiyo kwa ufanisi na Serikali kupitia Kamati ya Maendeleo ya Elimu ya Wilaya ya Rungwe (Rudet) iliikabidhi shule hiyo kwa uongozi wa kanisa hilo.

Wamesema kuwa katika makabidhiano hayo, walikubaliana kuwa kanisa hilo litaiendesha shule hiyo chini ya Halamshauri ambapo ilitakiwa kila mwaka kusomesha wanafunzi wawili bure kutoka vijiji vinavyoizunguka shule hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya kufuatilia madai ya wananchi hao, Solomon Mwakafyaga amesema kuwa baada ya miaka michache kanisa la SDA lilivunja makubaliano hayo na likaanza kufanya utaratibu wa kumiliki shule na majengo ya shule hiyo kinyemela bila wananchi kujua.

Ameyataja baadhi ya mambo yaliyobadilishwa kuwa ni pamoja na vibao vilivyokuwa vimeandikwa awali ‘Shule ya Wananchi’ na kuandikwa ‘Shule ya Waandiventista Wasabato’ ikionyesha kuwa kanisa ndilo wamiliki wa shule, pia kusitisha kusomesha wanafunzi wa kijiji hicho na kuzuia wananchi kupata taarifa za shule kinyume na makubaliano ya awali.

Hivyo wamefikisha madai yao kwa Mkuu wa Wilaya na uongozi wa Halmashauri ambao uliiandikia shule hiyo barua pamoja na kufungua kesi ya madai katika mahakama Kuu kitego cha  ardhi Jijini Dar es Salaam.

Mwafyaga amesema tangu mwaka 1996 wananchi wamekuwa wakitakiwa kusubiri kwa maelezo kuwa kesi ipo mahakamani, lakini wanashangaa kila mwaka shule inaendelea kusajili wanafunzi wa kidato cha kwanza na kidato cha sita, huku wananchi wakiwa hawajui hata tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Akijibu hoja hizo toka kwa wananchi, Kandoro amesema kuwa tatizo lao amelichukua na kuomba muda ili alifanyie kazi hivyo kuwataka wananchi hao kuwa na subira na kutousumbua uongozi wa shule hiyo wakati akiendelea kushughulikia tatizo lao.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger