Pages


Home » » WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUDAIWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA MTU MMOJA OMEGA BAR JIJINI MBEYA

WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUDAIWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA MTU MMOJA OMEGA BAR JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:24 | 0 comments
 Moto wenye utata umeteketeza chumba kimoja cha Bar inayoitwa Omega inayomilikiwa na Mrs Ngwada iliyopo mtaa wa Ilolo jijini Mbeya, majira ya saa Kumi na mbili jioni na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ansen Mtono wenye umri wa miaka 23 afariki dunia.Marehemu amekaa chumba hicho kwa muda wa siku mbili na alikuwa anadaiwa shilingi elfu hamsini ya bili ya vinywaji.
 Na mwandishi wetu.
Ema Ngwanda mkazi wa RRM mwenye umri wa miaka 36 na Neria Meshaki mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Isanga jijini Mbeya wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumchoma moto hadi kufa Hanseni Mtono wakimtuhumu kusababisha hasara ya shilingi elfu hamsini katika baa ya Omega iliyopo Isanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja za jioni ambapo watuhumiwa walimfungia marehemu kwenye chumba ambacho kilimwagiwa petroli kisha wakawasha moto.

Naye dada wa marehemu Jackline Mtono amesema kuwa septemba 28 mdogo wake alifungiwa kwenye chumba hicho kwa madai kuwa alisababisha hasara ya shilingi elfu 50 ambazo ni mtaji wa bia na kwamba baada ya mama yeke mzazi kwenda kuongea na wahusika waligoma kumtoa hadi hapo watakapo kuwa wamelipwa fedha zote.

Ameongeza kuwa baada ya siku moja kupita walipata taarifa ya ndugu yao kuchomwa moto akiwa ndani ya chumba alichofungiwa.

Hata hivyo majira ya saa kumi na mbili jioni wananchi wenye hasira kali walivamia na kuvunja bar ya Omega na kufanya uharibifu na kuviharibu vitu kadhaa ikiwemo TV na vilivyobaki vilibebwa na ndugu wa mlalamikiwa wakidai kwanini muuaji ameachiwa.


Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger