Wananchi mkoani Mbeya wanaalikwa kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru ambayo kimkoa yatafanyika kwa muda wa siku 3 katika viwanja vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe vilivyopo kata ya Ilomba jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mkuu wa mkoa mkuu wa wilaya ya Mbeya Evansi Balama kwa niaba ya mkuu wa mkoa Abasi Kandoro amesema kuwa maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali na sekta binafsi.
Aidha amewaalika wananchi kushiriki katika mdahalo wa miaka 50 ya uhuru utakao fanyika katika kumbi wa mkapa octoba 19 majira ya asubuhi hadi mchana.
Mida zitakazojadiliwa katika mdahalo huo ni Hali ya Usalama, hali ya huduma za jamii na hali ya Uchumi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ni KUKUZA UCHUMI, KILIMO CHENYE TIJA, MATUMIZI YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO NI SILAHA YA KUPAPAMBANA NA UMASIKINI wakati kauli mbiu ya kitaifa ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
0 comments:
Post a Comment