Wananchi wa mtaa wa Ivumwe kata ya Mwakibete jijini Mbeya wakiwa kwenye mazishi ya kijana Ayoub Shoti mwenye umri wa miaka 13, ambaye alifikwa na mahuti siku ya jumamosi baada ya kung'atwa na mbwa wenye kichaa. Lakini mpaka sasa jumla ya wananchi watatu wamefariki akiwemo Venance Samson umri wa miaka 13, na tisa kujeruhiwa na mbwa huyo. Marehemu amehitimu shule ya msingi mwaka huu katika shule ya msingi Ivumwe.
Mbwa anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa ambaye kasababibisha maafa ya kifo cha watu wa tatu na tisa kujeruhiwa katika mtaa wa Ivumwe kata ya mwakibete jijini Mbeya. Na uongozi wa mtaa kwa kushirikiana na Idara ya mifugo haujaweza kuchukua njia madhubuti ya kuweza kumteketeza mbwa huyo kwani mmiliki wa mbwa huyo hafahamiki.
Baadhi ya wananchi wakifukia kaburi la Marehemu Ayoub Shoti mkazi wa Mtaa wa Ivumwe kata ya Mwakibete aliyefariki baada ya kung'atwa na mbwa mwenye kichaa ambaye mpaka sasa hajateketezwa kutokana na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine tisa kujeruhiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Ivumwe Bwana Moris Nkurungu amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba wiki la kesho utaanza mchakato wa kuwasaka mbwa wote wenye kichaa na kuwateketeza.
0 comments:
Post a Comment