WANAFUNZI WAWILI WA KIDATO CHA KWANZA WAACHA MASOMO NA KUAMUA KUOANA.

Kamanga na Matukio | 01:13 | 0 comments


Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. Abbas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu.
Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Sange iliyopo kata ya Sange wilayani Ileje wameacha masomo na kuamua kuoana ambapo hadi sasa wanaishi kama mume na mke.

Hayo yamebainika baada ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kufanya ziara maalumu ya kujitambulisha wilayani humo ambapo pia alitembelea kujionea hali ya ujenzi wa shule ya msingi Sange.

Akiwa shuleni hapo Kandoro alielezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Lugano Mwambuja kuwa wanafunzi Joshua Kijalo na Acheni Tete waliacha masomo mwezi Julai mwaka huu na kuamua kuishi maisha ya ndoa.

Mratibu Elimu wa kata hiyo, Joseph Mwanzela amesema wanafunzi wameacha masomo kwa sababu za kiuchumi, ambapo watoto wa kike huamua kuacha shule na kwenda kufanya kazi za ndani mijini wakati wavulana hukimbilia kufanya kazi za mashambani.

Kutokana na taarifa hizo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro ametoa agizo kwa viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha watoto hao wanapatikana na kurejeshwa masomo pamoja na wazazi wa watoto hao kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kushindwa kuwadhibiti watoto wao kufuata masomo.

WATOTO ZAIDI YA MILIONI MOJA WENYE CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO MKOANI MBEYA KUPEWA CHANJO

Kamanga na Matukio | 01:12 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Watoto zaidi ya 1,886,226 mkoani Mbeya wenye umri chini ya miaka mitano wanatarajia kupewa chanzo ya surua, homa ya kupooza (polio), matone ya vitamin ‘A’ na dawa ya minyoo. 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk.Seif Mhina, akizungumza na mwandishi wetu amesema kampeni ya kutoa chanjo hizo itaanza Novemba 12 hadi 15 mwaka huu katika Halmashauri zote za mkoa huu. 

Alisema kampeni hii inalenga kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa hatari ya surua na homa ya kupooza na kuzuia mlipuko wa magonjwa hayo na kuimarisha kinga kwa watoto hao. 

Dk.,Mhina alitoa mchanganuo kuwa watoto 453,127 watapewa chanjo ya surua,polio watoto 535,995, matone ya vitamin ‘A’ 477,770,na dawa za minyoo watoto 419,404. 

Kwamujibu wa Dk.Mhina, chanjo ya Surua itatolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka mitano, polio wenye umri wa kuanzia siku moja hadi miaka mitano,matone ya vitamin ‘A’ wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka mitano wakati dawa ya minyoo watapewa watoto wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano. 

Alisema chanjo hizo zitatolewa kwa watoto wote bila kujali kama alishawahi kupata chanjo nyingine katika utaratibu wa kawaida unaojulikana kitaalam kama Routine Immunization. 

Dk.Mhina alitoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao katika vituo vya kupatia chanzo vilivyopo katika maeneo yao kwa tarehe hiyo ili kuwezesha kufanikisha zoezi hilo ambalo ni muhimu sana.

MELI YA MV SONGEA YASIMAMISHA SAFARI ZAKE BAADA KUHARIBIKA ILI IFANYIWE MATENGENEZO.

Kamanga na Matukio | 01:11 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Meli ya MV Songea inayosafirisha abiria na mizigo katika maeneo mbalimbali ndani ya ziwa Nyasa, imesimamisha safari zake baada ya kuharibika ili ifanyiwe matengenezo.

Kwa sasa meli hiyo imeegeshwa katika bandari mpya ya Kiwira wilayani Kyela ikisubiri kwenda kufanyiwa matengenezo katika bandari ya Drydock nchini Malawi.

Meneja wa kampuni ya Marine Services inayomiliki meli hiyo, Baraka Bigambo amesema meli hiyo imetoboka sakafu na imeanza kuingiza maji halki inayohatarisha usalama wa abiria na mali zao.

MV Songea inao uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 50 za mizigo na inatoa huduma katika ukanda mzima wa pwani ya upande wa Tanzania na nchi jirani ya Malawi.

Meli ya Mv Iringa ndiyo inayoendelea kutoa huduma za usafirishaji ambapo meli hiyo inauwezo wa kubeba abiria 138 na tani 15 za mizigo.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Bandari wilayani Kyela, Absalum Bohela amesema kuharibika kwa meli hiyo kumeathiri Mamlaka ya Bandari kutokana na kukosa mapato yatokanayo na shughuli zinazofanywa na meli hiyo.

RADI YASABABISHA KIFO NA KUJERUHI - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:16 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Bi Magdalena Mlaga mwenye umri wa miaka 28 amefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kupingwa na radi akiwa ndani ya nyumba yake, radi hiyo ambayo ilisababishwa na mvua iliyokuwa ikinyesha juzi katika kijiji cha Iyenga, kata ya Isansa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Chanzo chetu kutoka eneo la tukio kimeeleza kuwa mvua hiyo ilianza kunyeesha majira ya saa saba za mchana na ilimalizima majira ya saa nane unusu mchanaambapo marehemu akiwa na mwanae Happy Mwakanyonga mwenye umri wa miaka mitatu pamoja na mdogo wake Gift Yona mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Mpito walipingwa na radi hiyo.

 Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo bwana Efraimu Mwampanda amesema kuwa baada ya tukio hilo kutokea walimkuta Bi.Madawa Malaga akiwa amelala na ndipo walipomfikisha hospitali ya Vwawa Mbozi na kuambiwa kuwa amefariki dunia na kwamba mdogo wake aliendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Hata hiyo Mtoto Happy Mwakanyonga hakukutwa na tatizo lolote.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema kuwa hana taarifa ya tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi baada ya kulifuatilia.

SAKATA LA HUNDI ZA MIRATHI KUTOWAFIKIA WAHUSIKA.

Kamanga na Matukio | 04:15 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Imedaiwa kuwa hundi nyingi za mirathi zimekuwa haziwafikii warithi na kubaki mahakamani kutokana na mawasiliano duni kati ya msimamizi wa mirathi na mahakama za mwanzo

Aidha warithi kutochukuwa hundi kutokana na kukata tama inayosababishwa na kutokuwa na taarifa ya kukamilika kwa malipo, gharama za kufuata malipo kuwa kubwa na urasimu wa watendaji wa mahakama.

Hayo yamebainishwa na afisa mirathi kutoa hazina bwana Wiliamu Kesi wakati akitoa mafunzo ya kukabilia na changamoto hizo kwa watendaji na mahakimu wa mahakama za mwanzo kwa mikoa ya Iringa na Ruvuma.

Wakati huohuo amezitaka familia kumteua msimamizi anayeaminika na familia kwa ujumla ili kuondoa tofauti zinazoweza kujitokeza wakati wa kufuatilia mirathi.

ZAIDI YA WAJASIRIAMALI 40 KUSHIRIKI MAONESHO YA UJASIRIAMALI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:12 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Zaidi ya wajasiliamali 40 kutoka Mbeya, Dar es salaam na Kenya watashiriki maonesho ya ujasiriamali yatakayofanyika kwa siku 3 katika viwanja vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe jijini hapa.

Akiongea na mwandishi wetu meneja masoko wa Mbeya Trade Fair bwana Stephen Msekwa amesema nia ya kuchanganya wajasilia mali wa ndani na nje ya nchi ni kuwaongezea ujuzi wajasilia mali wa ndani katika shughuli zao.

Amezitaja bidhaa zitakazo oneshwa siku hiyo kuwa ni nguo za asili, wine, sabuni za kuongea, sabuni za usafi wa choo na juisi.

Aidha amesema maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa November 4 na mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Idi na kufungwa November 6 na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro.

MKUU WA MKOA WA MBEYA MH KANDORO AWATAKA WANANCHI KUTOKUWA NA JAZBA, CHUKI KATIKA UCHANGIAJI WA MAONI YA KATIBA MPYA WAKATI UTAKAPOFIKA.

Kamanga na Matukio | 05:24 | 0 comments
Mkuu wa mkoa wa Mbeya mheshimiwa Abbas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu
Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya Bw Abbas Kandoro amesema kuwa wakati utakapokuwa umefika  wa kukusanya maoni  ya katiba mpya wananchi wanatakiwa kutotumia jazba, chuki au shinikizo kwani katiba hiyo ni sheria mama inatakiwa kujadiliwa kwa umakini.

 Mkuu huyo wa Mkoa alisema hivi sasa suala la katiba  mpya linazungumzia karibu kila kona hivyo kuna umuhimu likapewa umuhimu wa aina yake na likajadiliwa kwa kina na si kujadili wakati wananchi wakiwa na chuki zao au shinikizo.

Alisema kuwa matatizo yaliyopo hivi sasa mkoani hapo ni ya mpito,kwa kuwa hakuna taifa linalojengwa kwa mara moja isipokuwa ni kwa kuunganisha nguvu kama taifa ili kuona ni namna gani matatizo hayo yatakabiliwa.

Bw. Kandoro alisema kuwa suluhisho la matatizo hayo haliwezi kutatuliwa kwa kufanya fujo wala kupiga watu nondo bali huo ni uhalifu ambao haustahili kushabikiwa kamwe.

  Aidha Bw.Kandoro alitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi wa Mbeya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba mpya utakapoa anza kwa kutoa mawazo yao ili kuboresha katiba hiyo kwa manufaa ya Taifa ni ya Mtu moja mmoja.

WAZIRI NAGU AMEZITAKA TAASISI NA VYOMBO VYA DLA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI.

Kamanga na Matukio | 05:19 | 0 comments


Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu
(katikati).
Na mwandishi wetu.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji  na uwezeshaji Dkt.Mary Nagu (Mb) amezitaka taasisi na vyombo vya dola kuweka mazingira wezeshi  ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wawekezaji katika Tanzania  ili kusiwepo na vikwazo na ucheleweshwaji wa huduma muhimu.

 Dkt. Nagu aliyasema hayo  jana wakati wa ufunguzi wa kituo cha uwekezaji kwa kanda ya  nyanda za juu kusini kilicho ofisi za Bank ya NBC Jijini hapa.

Alisema kuwa  ili wawekezaji  wa kanda ya Mbeya waweze kufanya kazi vizuri hakuna budi vikwazo vyote kuondolewa na upatikanaji wa huduma muhimu kwa wawekezaji urahisishwe.


 Hata hivyo waziri Nagu alihimiza mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kutenga, kupima na kusajili maeneo ya uwekezaji ipasavyo kabla ya kuyagawa pale inapowezekana ili kuondoa usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

 Alisema ikumbukwe kuwa uwekezaji  ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi  kwani  utaongeza pato la Taifa, mitaji na teknolojia na ajira kwa watanzania wengi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kituo cha Uwekezaji cha Tanzania Balozi Elly Mtango alisema kituo hicho kinategemea  kufanya kazi  na mamlaka nyingine za mikoa na serikali za mitaa na vijiji katika kufanikisha upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za uwekezaji na uendelezaji wa miuondo mbinu.

 Aidha alitoa wito kwa wafanyabishara na wawekezaji wote katika kanda ya mbeya  kutumia kituo hicho katika kujipatia huduma mbali mbali ili wajiendeleze kibiashara na kiuwekezaji.

WAKRISTO WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU KWA LENGO LA KUUKABILI UTANDAWAZI

Kamanga na Matukio | 05:14 | 0 comments

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mtume Ayubu Msigwa wa Huduma ya World Alive Ministry (WAM) ya Jijini Mbeya amewataka Wakristo nchini kujiendeleza kielimu ili kwenda na wakati wa utandawazi..

Akihubiri katika huduma hiyo iliyopo Sae Jijini Mbeya, Msigwa maarufu kama “Sauti ya Simba” alisema  wokovu sio ujinga  kama wengine wanavyofikiria.

“Wapendwa wokovu sio ujinga  yaani elimu mnaichukulia kama dhambi?”. Alihoji Mtume Msigwa.

Aliongeza kusema walokole wengi wamekuwa wakifanya shughuli zao bila elimu na kujikuta wakitumbukia katika hasara kubwa na mitaji kufilisika.

Mtume Msigwa alisema chimbuko la wengi kukimbilia kwa waganga wa kienyeji katika biashara zao ni kutokana na ukosefu wa elimu ambayo ni muhimu katika kuendesha biashara, na kwamba wengine wakienda kwa sangoma hao hujikuta wakipewa masharti magumu kwa mfano ya kuua familia zao wakiamini ndio watapata utajiri.

Pia Sauti ya Simba aliwataka wakristo kusoma Biblia kwani katika kitabu hicho ndimo ulimo ukombozi wao na kusisitiza “mshike sana elimu usimwache elimu aende zake kwani ndiye uzima wako”.

Hata hivyo aliwataka wakristo hao kuachana na tabia ya ulegevu pindi wanapokuwa katika masomo kwani wengine hufikiria kuwa ni dhambi wakikazana kusoma huku wakisubiri miujiza katika kila kitu.

Kwa suala la wazazi na watoto wao Mtume msigwa alisema wazazi wamesahau kuweka misingi mizuri kwa kwa watoto wao hasa suala la elimu, na kudai kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiaachia watoto wao vitu ambavyo havitawasaidia maishani mwao na baada ya kufa ugomvi baina ya ndugu na watoto hujitokeza.

Wanafunzi kwa upande wao wametakiwa kusoma kwa  bidii wanapokuwa masomoni  badala ya kujiingiza katika starehe, na kuongeza kuwa wasimsahau Mungu katika masomo yao, na kwamba wao ni vichwa na si mkia.

Aidha Sauti ya Simba katika Ibada hiyo aliihitimisha kwa kufanya maombi kwa wanafunzi waliokuwepo hapo na wengine kufunguliwa baada ya maombi hayo.

Huduma ya WAM imeanzishwa miaka miwili iliyopita ikianza na watu wanane, lakini hivi sasa ikiwa na zaidi ya waamini 400 kutoka mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

MBUNGE MBEYA ASEMA HATOKIHAMA CHAMA CHA MAPINDUZI

Kamanga na Matukio | 04:55 | 0 comments

 Mbunge wa jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi(katikati), akisalimiana na baadhi ya wananchi nje ya mahakama ya Hakimu mfawidhi wa mkoa wa Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Modestus Kilufi kupitia chama cha Mapinduzi amesema kuwa hana mpango wa kukihama chama cha Mapinduzi (CCM) licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizosababishwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho.

Ameyasema nje ya Mahakama ya mkoa wa Mbeya mara baada ya kutoka mahakamani hapo kutoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya kutishia kuuwa.
 
Amesisitiza kwamba  changamoto zilizopo kati yake na wanachama wenzake wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbarali haiwezi kumvunja moyo wa kuwatetea wananchi bali ni njia ya kumwongezea nguvu katika kusimamia masuala muhimu yanayowakabili wananchi wa jimbo lake.

Wakati huohuo ameitaka jamii kutambua kuwa utetezi wa wananchi haufanywi na chama fulani cha siasa bali ni jukumu la kila kiongozi kuwatumikia wananchi wake kuwatetea kwa uongozi wa juu ili kero zao ziweze kutatuliwa.

Hukumu ya Mbunge huyo itatolewa Novemba 9 mwaka huu baada ya pande zote za ushahidi kumaliza kutoa ushahidi wao.

UNYWAJI POMBE KUPINDUKIA UMETAJWA KUWA NI MOJA YA SABABU YA WATOTO KUISHI MAZINGIRA HATARISHI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:53 | 0 comments

Na mwandishi wetu
Unywaji wa pombe kupindukia umetajwa kuwa moja ya sababu inayochangia baadhi ya wazazi na walezi wa kata ya Igawilo jijini Mbeya kushindwa kutoa huduma muhimu kwa watoto wao hali inayopelekea watoto hao kuishi kwenye mazingira hatarishi.

Akiongea na mwandishi wetu mwenyekiti wa mtaa wa Mwanyanji Bwana Elia Jerema amesema watoto wanao onekana kwenye madampo wakiokota vitu mbalimbali kwa kuwa wamekosa malezi kutoka kwa wazazi ambao muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwenye uuzaji na unywaji wa pombe.

Aidha amewataka wakazi wa mtaa huo kutojihusishwa na vitendo vya unywaji wa pombe muda wa kazi na kwamba mtu atakaye kamatwa akinywa pombe muda huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naye mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la JOHN amesema analazimika kuokota vitu kwenye madampo ya taka ili aweze kuuza na kujipatia kipato kitakachomsaidia kununua mahitaji mbalimbali.

MTU MMOJA AFARIKI KWA KUJINYONGA MTAA WA MWAMBENJA - KATA YA IGANZO MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:46 | 0 comments
 Mtu mmoja mkazi wa mtaa wa Mwambenja kata ya Iganzo jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la Anyimike Ambokile mwenye umri wa miaka 25, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya plastiki chumbani kwake, na hakuacha ujumbwe wowote wa kukatiza maisha yake. Marehemu alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza mitumba katika soko la Sido Mwanjelwa lililoteketea kwa moto hivi karibuni.(Picha juu ni sehemu ambayo marehemu alijinyonga)
Kifo cha Anyimike Ambokile kiligunduliwa na mama wa marehemu aitwaye Esther Tujobe mwenye umri wa miaka 60, wakati akijiiandaa kuelekea kanisani ndipo agagundua marehemu hajaamka mapema kwenda kwenye shughuli za kuuza mitumba na kukuta mwanae akiwa amefariki na hivyo kulazimika kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja Bwana Lucas Mwakalonge ambaye nae alitoa taarifa kwa Diwani wa kata ya Iganzo Bwana Uswege Furika ambaye alitoa taarifa kwa Kituo cha Polisi cha Kati jijini Mbeya ambapo walifika na kuuchukua mwili wa marehemu  hadi Hospitali ya RufaaMkoani Mbeya kwa uchunguzi zaidi ambapo jalada lake ni MB/IR/9204/2011

SAKATA LA MBWA MWENYE KICHAA LAISHIA PABAYA WATOTO WAWILI WAFARIKI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:26 | 0 comments
 Wananchi wa mtaa wa Ivumwe kata ya Mwakibete jijini Mbeya  wakiwa kwenye mazishi ya kijana Ayoub Shoti mwenye umri wa miaka 13, ambaye alifikwa na mahuti siku ya jumamosi baada ya kung'atwa na mbwa wenye kichaa. Lakini mpaka sasa jumla ya wananchi watatu wamefariki akiwemo Venance Samson umri wa miaka 13, na tisa kujeruhiwa na mbwa huyo. Marehemu amehitimu shule ya msingi mwaka huu katika shule ya msingi Ivumwe.
 Mbwa anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa ambaye kasababibisha maafa ya kifo cha watu wa tatu na tisa kujeruhiwa katika mtaa wa Ivumwe kata ya mwakibete jijini Mbeya. Na uongozi wa mtaa kwa kushirikiana na Idara ya mifugo haujaweza kuchukua njia madhubuti ya kuweza kumteketeza mbwa huyo kwani mmiliki wa mbwa huyo hafahamiki.
Baadhi ya wananchi wakifukia kaburi la Marehemu Ayoub Shoti mkazi wa Mtaa wa Ivumwe kata ya Mwakibete aliyefariki baada ya kung'atwa na mbwa mwenye kichaa ambaye mpaka sasa hajateketezwa kutokana na kusababisha vifo vya watu  watatu na wengine tisa kujeruhiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Ivumwe Bwana Moris Nkurungu amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba wiki la kesho utaanza mchakato wa kuwasaka mbwa wote wenye kichaa na kuwateketeza.

WANANCHI WATAKIWA KUVITUNZA VYAZO VYA MAJI NYIMBILI WILAYANI MBOZI MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:30 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Wananchi waishio kandokando ya vyanzo vya maji wametakiwa kuvitunza vyanzo hivyo ili kusaidia kupatikana kwa maji katika kipindi chote cha mwaka

Rai hiyo imetolewa na wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Chizumbi lililopo kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Wamesema endapo vyanzo hivyo vitatunzwa kikamilifu vitasaidia kuondokana na tatizo la maji pamoja na kuiwezesha mito kutiririsha maji kwa kipindi chote cha mwaka

Mmoja wa wakulima hao Bi.Sophia Kayombo ametoa ombi kwa serikali kuwatafutia soko la mazao yao ili waweze kunufaika zaidi na kilimo hicho

Bonde la Chizumbi limekuwa chachu ya maendeleo kwa wakulima katika kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mpunga, mahindi na mbogamboga kwa wilaya ya Mbozi na Ileje.

WATENDAJI WA HALMASHAURI NA WILAYA WAMETAKIWA KUONDOA URASIMU WA TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:29 | 0 comments
Waandishi wa habari wakongwe na waliobobea mkoani Mbeya
*****
Na mwandishi wetu
Katibu tawala msaidizi Utumishi na Utawala Bwana Leonald Magacha amewataka watendaji wa halmashauri na wilaya kuondoa urasimu wa taarifa kwa waandishi wa habari ili kuiwezesha jamii kutambua mambo yanayoendelea katika mkoa wao.

Ameyasema hayo kufuatia kuwepo kwa tabia ya baadhi ya wakuu wa idara kutoka halmashauri mbalimbali kutokuwa na ushirikiano na vyombo vya habari katika kutoa taarifa hali inayowalazimu waandishi wa habari kutafuta njia mbadala ya kupata habari hizo.

Naye mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe ameuomba uongozi wa Serikali mkoani hapa kuondoa ubaguzi wa vyombo vya habari katika kutoa taarifa ili kuondoa hisia binafsi za mtu katika utendaji kazi.

SAKATA LA BEI YA UNUNUZI WA GARI ZA KUZOLEA TAKA LA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:28 | 0 comments
 Gari la kuzolea taka la halmashauri ya jiji la Mbeya.(Picha na mtandao huu)
******
Na Gabriel Mbwille.
Mkaguzi mkuu wa Serikali kanda ya nyanda za juu kusini Mohamed Ramadhani amesema kuwa gari la kubeba taka lililonunuliwa na halimashauri ya jiji la Mbeya kwa shilingi milioni 300 linathamani ya shilingi milioni 20.

Akisoma taarifa hiyo ndani ya kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi mwishoni mwa wiki amesema kuwa gari hilo limetumika hivyo fedha stahiki ilitakiwa Jiji hilo litoe ni shilingi Milioni 20 lakini viongozi waliokuwepo waliidhinisha Shilingi Milioni 300.

Aidha katika hadidu rejea za Juni 19 mwaka huu za kikao cha Baraza la Madiwani waliazimia kumrejesha Jijini Mbeya aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji mwaka 2008, mweka   hazina na Afisa ugavi wa kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye alialikwa katika kikao hicho alimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Idd kwa kuendelea kuziba mianya ya ubadhilifu katika Jiji hilo na kwamba Serikali itaendelea kumlinda.

WANANCHI WATAKIWA KUVITUNZA VYAZO VYA MAJI NYIMBILI WILAYANI MBOZI MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:27 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Wananchi waishio kandokando ya vyanzo vya maji wametakiwa kuvitunza vyanzo hivyo ili kusaidia kupatikana kwa maji katika kipindi chote cha mwaka

Rai hiyo imetolewa na wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Chizumbi lililopo kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Wamesema endapo vyanzo hivyo vitatunzwa kikamilifu vitasaidia kuondokana na tatizo la maji pamoja na kuiwezesha mito kutiririsha maji kwa kipindi chote cha mwaka

Mmoja wa wakulima hao Bi.Sophia Kayombo ametoa ombi kwa serikali kuwatafutia soko la mazao yao ili waweze kunufaika zaidi na kilimo hicho

Bonde la Chizumbi limekuwa chachu ya maendeleo kwa wakulima katika kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mpunga, mahindi na mbogamboga kwa wilaya ya Mbozi na Ileje.

MTOTO AJERUHIWA BAADA YA KUPINGWA NA WATU WANAODAIWA KUWA NI MAJAMBAZI

Kamanga na Matukio | 06:26 | 0 comments
 Mtoto Victa Tobia aliyejeruhiwa baada ya kupingwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi
Na mwandishi wetu
Mtoto Victa Tobias mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kamficheni Soweto jijini Mbeya amepigwa na watu wasiofahamika asubuhi ya jana baada ya kudhaniwa kutaka kuiba vyuma chakavu kwenye moja ya gereji jijini hapa.

Kutokana na kipigo hicho mtoto huyo amejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha uvimbe katika maeneo ya mabega, mgongoni na kichwani.

Mwenye wa mtaa Ruanda Sinde bwana Patrik Haule amesema mtoto huyo amepigwa kwa kuhisiwa kuwa ni mwizi wa vyuma chakavu na kwamba amechukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya.

KIJANA MMOJA ALIYEHITAJI MSAADA WA MAZISHI, AFANYA UTAPELI NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA

Kamanga na Matukio | 06:23 | 0 comments
Afisa mtendaji wa mtaa wa Maendeleo kata ya Iyunga jijini Mbeya Bi Tabu Sengo Tabu ambaye ametapeliwa simu yekye thamani ya shilingi 90,000/= kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Geogre Ramsi aliyedai kuwa ametokea jijini Tanga,  alifika katika uongozi wa serikali hiyo kuomba msaada wakumzika ndugu yake aliyedaiwa amejifungua na kufariki katika Hospitali ya Rufaa Meta jijini hapa.
 Bwana Elias Mwakyusa aliyeitwa kusaidia kuzika akiwa amefika kwa fundi seremala kubeba misalaba.
 Dereva akiwa na pikipiki iliyokodiwa na kijana tapeli George Ramsi aliyedai kufiwa na ndugu yake aliyejifungua katika hospitali ya Rufaa Meta kwa njia ya operasheni ambaye naye alitapeliwa simu yenye thamani ya shilingi 80,000/= za kitanzania na fedha zilizokuwa katika akaunti ya MPESA shilingi70,000/=
Fundi seremala Bwana Maiko Mwakalonge aliambiwa  atengeneze misalaba yenye thamani ya shilingi 10.000/= na kijana tapeli George Ramsi ambapo hakuweza kulipwa.
 Gari iliyokodiwa na kijana tapeli George Ramsi kwa shilingi 20,000/= kwa ajili ya kuwabeba wachimbaji wa kaburi wanne(majina yao katika habari inayofuata chini), ambapo umbali hadi kufikia eneo la makaburi ni kilometa 5 kutoka Iyunga.

Vijana wa kutoka kushoto ni Obadia Robert Kyando, Obby Mwakasasagule, Shida Mwasambili na Matatizo Kyando waliokodiwa kwa ajili ya kuchimba kaburi kwa shilingi 110,000/= ambapo waliahidiwa kulibwa na kijana huyo baada ya mazishi lakini hawakuweza kulipwa.
Fundi seremala Maiko Mwakalonge aliyefika katika ofisi ya Afisa mtendaji Bi Tabu Sengo kutoa malalamiko ya kutengeneza misalaba na mteja wake kutoonekana.

Kijana huyo tapeli George Ramsi ametokomea kusikojulikana baada ya kupelekwa kwa Mchungaji wa kanisa la Sabato Nzovwe, majira ya saa saba akiomba taratibu za mazishi kufanyika katika kanisa lake, kitu ambacho si cha kweli na kudai anaomba kwenda kununua vocha ndipo alitokomea moja kwa moja na simu ya afisa mtendaji, dereva wa pikipiki na shilingi elfu mbili ya dereva taksi.

Hata hivyo baada ya kijana huyo kutofika makaburini ndipo kulipopelekea kupatikana kwa taarifa za kuwa kijana George ni tapeli na taarifa zilipelekwa katika Kituo cha polisi cha Iyunga.

WATU 30 WAJERUHIWA NA HAKUNA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSUSHA MAGARI MANNE MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa katika ajali mbaya na hakuna aliyefariki iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Baadhi ya majeruhi kati majeruhi 30 wakiwa wameketi chini, wakiwaweshikwa na butwaa kushindwa kuamini kile kilichotokea baada ya kutoka salama katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo hakuna aliyefariki lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Mashuhuda waliofika eneo la ajali ambapo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Moja kati ya malori matatu yaliyosababisha ajali na kuziba barabara na hali iliyopelekea magari mengine kushindwa kupita  katika ajali mbaya, ambayo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali hiyo iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma.

WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA NA NOTI BANDIA

Kamanga na Matukio | 05:52 | 0 comments

Kamanda wa Jeshila Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi
*****
Na mwandishi wetu
Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili wakazi wa Tunduma na Kyela baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Kokeini na Bangi pamoja noti 3 za bandia za  shilingi elfu kumi.

Akiongea na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema kuwa jana majira ya saa 6 za mchana Imani Chaula mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Mwaka Tunduma alikutwa na kete 50 za bangi akiwa anauza.

Aidha amemtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni Ramadhani Abasi mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Kyela kati ambaye alikuwa na kete kumi za dawa ya kulevya aina ya Kokeini na noti 3 bandia za elfu kumi.

Amesema mtuhumiwa huyo ni muuzaji wa dawa za kulevya na kwamba watuhumiwa wote wamefikishwa leo mahakamani kosomewa mashtaka yao.

WAOMBA MSAADA WA FEDHA ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UFUNGAJI WA MITAMBO YA UMEME NUNGU - MAKETE

Kamanga na Matukio | 05:51 | 0 comments
Wananchi wa kijiji cha Nungu wilaya ya Makete mkoani Iringa wameiomba serikali iweze kuwasaidia kiasi cha fedha ili waweze kufanikisha zoezi la ufungaji wa mitambo ya umeme katika maporomoko ya mto Mbulu.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Bwana Esau Ndaga amesema ili kufanikisha zoezi la ufungaji wa mitambo hiyo msaada mkubwa unahitaji kutoka Serikalini na wadau wengine wa maendeleo.

Naye mwenyekiti wa kijiji hicho Bi.Marieth Malekano amesema wamefanikiwa kumpata mkandarasi wa kufunga mitambo hiyo ambapo gharama inayohitajika ni shilingi milioni 20.

MWALIMU AKUTWA AMEUWAWA NA MWILIWAKE KUACHWA MTUPU NA KUHARIBIKA VIBAYA MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:50 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Mwalimu wa shule ya msingi Wimba iliyopo tarafa ya Igale B. kata ya Utengule Usongwe Bi.Maria Harudo Sanga mwenye umri wa miaka 46 amekutwa ameuawa na mwili wake kuachwa  ukiwa mtupu na kuharibika vibaya.

Akiongea na mwenyekiti wa Kijiji cha wimba Dickson Mlawa amesema October 14 mwaka huu mwalimu huyo aliaga kwenda Iringa baada ya kuibiwa vitu vya thamani kwenye nyumba yake na kwamba hakuonekana kwa zaidi ya siku 4 hadi hapo mwili wake ulipokutwa ukiwa umeharibika

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Wimba Nikubuka Mbwile amesema taarifa za kifo cha mwalimu huyo zilitolewa na wanafunzi baada ya kukuta nguo za mwali huyo kichakani

Nao wanafunzi wa shule hiyo Ayubu Japheti na Erenesi Wile wamesema nguo za mwalimu wao waliziona wakati wakiwa wanaelekea kwenda shule.

Naye kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amekiri kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa uchunguzi zaidi bado unaendelea.

Imeelezwa kuwa wakati wa uhai wake mwalimu huyo alikuwa na kesi 4 katika mahakama ya hakimu mkazi Mbeya akiwadai watu watano fedha ambapo katika kesi hizo mwalimu huyo alishinda na kupewa haki yake.

DIWANI NA AFISA MTENDAJI WA KATA YA RUIWA MKOANI MBEYA WAKACHA MKUTANO.

Kamanga na Matukio | 05:49 | 0 comments
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mheshimiwa Hamad Sharifu awataka Diwani na Afisa mtendaji wa kata ya Ruiwa kuwasikiliza wananchi kero zinazowakabili katika shughuli za maendeleo katika kata hiyo iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Ruiwa. wilayani Mbarali wakitaka kusomewa taarifa za mapato na matumizi ambapo diwani wa kata hiyo ni Bwana Alex Ndamlage na Afisa mtendaji ni Bwana Jordan Masweve ambayo kwa pamoja wanadaiwa kukwepa kukutana na wananchi amabo wanadai kusomewa taarifa za mapato na matumizi licha kukusanya pesa kibao za mifugo.

Kwa pamoja viongozi hao wa kata walimkamata na kumweka mahabusu mmoja wa wananchi hao Bwana Juma Merere kuanzia majira ya saa 10 usiku wa manane hadi saa 4 asubuhi ambaye alikuwa akisambaza taarifa na mkutano huo wa kutaka kusomewa mapato na matumizi, hali iliyopelekea wananchi kutishia kuvunja ofisi ya mifugo ambayo walimfungia mwananchi huyo ndipo walipomuachia Bwana Juma nawao kutokomea.

BAADHI YA MADEREVA NA ABIRIA MKOANI MBEYA NI SUGU KWANI HAWAJIFUNZI KUTOKANA NA MAKOSA, KWA AJALI ZINAZOTOKEA MKOANI HAPA.

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Sakata la kubeba abiria katika magari ya kubebea mizigo bado ni tete mkoani Mbeya, licha ya kuwepo kwa ajali zinazotokea mara kwa mara na kuchinja idadi kubwa ya abiria. 

Mtanado huu umeweza kushuhudia gari hili la mizigo aina ya Canter katika barabara ya Utengule Usangu wilayani Mbarali likiwa limebeba abiria kwa kushonana. Je?, Jeshi la polisi mkoani Mbeya mnaliona hili kwa makini ili kunurusu uhai wa wanajamii?.

MAMIA WAJITOKEZA KATIKA MDAHALO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:22 | 0 comments
Aliyeshika kipaza sauti ni Mchungaji ambaye ni mmoja wa wawezeshaji wa Mdahalo wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ni KUKUZA UCHUMI, KILIMO CHENYE TIJA, MATUMIZI YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO NI SILAHA YA KUPAPAMBANA NA UMASIKINI wakati kauli mbiu ya kitaifa ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
 
Baadhi ya wawezeshaji wa.Mdahalo wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru mkoani Mbeya, uliofanyika katika Ukumbi wa Mkapa uliopo jijini Mbeya, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa chuo cha Mbeya Institute of Science and Technology(MIST) Prof Msambichaka ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ni KUKUZA UCHUMI, KILIMO CHENYE TIJA, MATUMIZI YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO NI SILAHA YA KUPAPAMBANA NA UMASIKINI wakati kauli mbiu ya kitaifa ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
 Baadhi ya wadau wa mdahalo wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru mkoani Mbeya waliofika kuchangia mada, katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya, ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ni KUKUZA UCHUMI, KILIMO CHENYE TIJA, MATUMIZI YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO NI SILAHA YA KUPAPAMBANA NA UMASIKINI wakati kauli mbiu ya kitaifa ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
Mwenye shati jeupe(wa kwanza kulia), Kamanda wa TAKUKURU mkoani Mbeya Bwana Daniel Mtuka akifuatilia kwa makini Mdahalo wa wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, uliofanyika katika Ukumbi wa Mkapa uliopo jijini Mbeya, ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ni KUKUZA UCHUMI, KILIMO CHENYE TIJA, MATUMIZI YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO NI SILAHA YA KUPAPAMBANA NA UMASIKINI wakati kauli mbiu ya kitaifa ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
Wanafauzi wa Chuo cha Ualimu cha Moravian kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian mkoani Mbeya wakifuatilia kwa makini mdahalo wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, uliofanyika katika Ukumbi wa Mkapa uliopo jijini Mbeya, ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa mkoa wa Mbeya ni KUKUZA UCHUMI, KILIMO CHENYE TIJA, MATUMIZI YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO NI SILAHA YA KUPAPAMBANA NA UMASIKINI wakati kauli mbiu ya kitaifa ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE

WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI

Kamanga na Matukio | 05:57 | 0 comments


Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde
 *****
Watu wa tatu wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya katika kijiji cha Ivuna kata ya Kamsamba wilayani Mbozi, kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule ya sekondari ya Ivuna vikiwemo saruji, rangi na chokaa.

Amewataja watu hao kuwa ni Mkuu wa shule ya sekondari ya Ivuna Bwana Danford Mwakaswaja, Erick Mkamba ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya shule na Magazeti Simfukwe ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Ivuna.

Kwa pamoja watu hawa wanadaiwa Oktoba 18, mwaka huu majira ya saa 11 jioni walikamatwa na wananchi wa kijiji hicho cha Ivuna wakiwa wamebeba katika gari, wakidai wanavipeleka katika shule ya Msingi Itumbula kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi hali iliyopelekea wananchi hao kupinga taarifa hizo na kuamua kuita Jeshi la polisi.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi magharibi Mheshimiwa David Silinde amesema kwamba watu hao walikuwa na nia ya kuiba na sababu ya kuwa vinatumika katika ujenzi wa shule ya msingi si sahihi.

Naye Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa amesema watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha Polisi Vwawa na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger