Msongamano wa magari ya mizigo katika parking mji mdogo wa tunduma
Mwenyekiti wa mji mdogo wa Tunduma Bwana Elias Cheyo akiwa na katibu wake Bwana Godness Mwaipula
*****
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa mji Tunduma na vitongoji vyake mkoani Mbeya,wameitaka serikali kuchukua hatua za makusudi za kuondoa msongamano wa magari,unaojitokeza kila mara katika barabara na viunga vya mji huo.
Imeelezwa kuwa hali hiyo imesabababishwa na kuwepo kwa ongezeko la idadi kubwa ya magari ya mizigo na mengine madogo yanayosubiri foleni ya kuvuka mpaka wa nchi za Tanzania na Zambia kwenda nchini za kusini mwa Afrika.
Baadhi ya wakazi hao Juma Rashidi na Alex Ngole walisema kuwa serikali inapaswa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kuweka maegesho ya magari makubwa ya mizigo na yaliyobeba nishati ya mafuta gesi.
Wakazi hao walziitaka mamlaka za Serikali zenye dhamana, kuweka utaratibu wa kudumu ili kuruhusu magari hayo kuondoka katika maegesho yao baada ya kupatikana mawasiliano kati ya madereva na maofisa wa mpaka huo
Walisema abiria wa mabasi i makubwa na madogo ,wamekuwa wakipata usumbufu ya kushushwa umbali wa km 5 huku wakitembea kwa miguu wakiwa wamebrba baadhi ya mizigo yao kichwani.
Walisema ili kutatua tatizo hilo pia serikali ipanue barabara za mji huo ikiwemo barabara kuu inayokwenda kusini, kuondoa magari makubwa katikati ya mji na kuweka vituo vingine vya kubeba abiria na mizigo nje kidogo ya mji huo.
Akizungumza na “Uhuru”jana ,mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma Elias Cheyo alisema kuwa wananchi wanapata usumbufu mkubwa wakati wa kutoka na kuingia katika mji huo, hatua ambayo huchangia kupunguza ufanisi wa kazi za utendaji na uzalishaji mali.
Alisema suala hilo linafahamika na lipo katika ngazi mbalimbali za serikali ambalo limekuwa likijadiliwa katika vikao mbalimbali lakini halionyeshi kuwepo kwa dalili za kukabiliana nalo.
Alisema kufuatyia hali hiyo ajali nyingi zimekuwa zikijitokeza na kugharimu maisha ya wananchi baaada ya kuanza kutumia njia zingine za usafiri zisizo rasmi ikiwa ni pamoja na pikipiki zisizosajiliwa..
Kwa upande wake Afisa mfawidhi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kituo cha Tunduma Rogasian Shirima,alikiri kuwepo kwa msongamano huo ambao alisema unasababishwa na kuwepo kwa miundo mbinu duni kwa wamiliki wa mpaka huo nchi za Tanzania na Zambia.
Alisema kuna barabara moja inayoruhusu magari ya kutoka na kuingia katika mpaka huo, tofauti na maeneo mengine ya mipaka hapa nchini pamoja na kuwepo na eneo dogo la kuegesha magari.
Alisema hali kama hiyo imejitokeza upande wa pili wa mpaka ambako Serikali ya Zambia iko katika hatua za kujenga kituo maalumu (One Stop Boder) mahali patakapo kuwa pakifanyika ukaguzi na uchunguzi wa mara moja wa mizigo na abiria, utakaokuwa ukifanywa na maofisa wa idara na taasisi za Serikali wa nchi mbil hizo.
Aidhaa alitaja sababu za mawakala wa forodhawa Zambia kuwa na uwezo mdogo wa fedha ya dhamana katika mashirika ya bima na mabenki hivyo kusababisha kushindwa kuhudumia magari mengi kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa Shirima mpaka huo umekuwa ukipokea zaidi ya malori 213 ya mizigo kwa siku pamoja na idadi nyingine ya malori 150 ya mafuta,magari ya kupita zaidi ya 300 na mabasi manne ya abria wa kutoka nchi za maziwa makubwa wanaoingia nchini,
0 comments:
Post a Comment