Mkuu wa mkoa wa Mbeya mheshimiwa Abbas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu
*****
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Abbas Kandoro amesema kuwa wakati utakapokuwa umefika wa kukusanya maoni ya katiba mpya wananchi wanatakiwa kutotumia jazba, chuki au shinikizo kwani katiba hiyo ni sheria mama inatakiwa kujadiliwa kwa umakini.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema hivi sasa suala la katiba mpya linazungumzia karibu kila kona hivyo kuna umuhimu likapewa umuhimu wa aina yake na likajadiliwa kwa kina na si kujadili wakati wananchi wakiwa na chuki zao au shinikizo.
Alisema kuwa matatizo yaliyopo hivi sasa mkoani hapo ni ya mpito,kwa kuwa hakuna taifa linalojengwa kwa mara moja isipokuwa ni kwa kuunganisha nguvu kama taifa ili kuona ni namna gani matatizo hayo yatakabiliwa.
Bw. Kandoro alisema kuwa suluhisho la matatizo hayo haliwezi kutatuliwa kwa kufanya fujo wala kupiga watu nondo bali huo ni uhalifu ambao haustahili kushabikiwa kamwe.
Aidha Bw.Kandoro alitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi wa Mbeya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba mpya utakapoa anza kwa kutoa mawazo yao ili kuboresha katiba hiyo kwa manufaa ya Taifa ni ya Mtu moja mmoja.
0 comments:
Post a Comment