Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya mheshimiwa Jackson Msome.
*****
Na mwandishi wetu.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya Jackson Msome, amepiga marufuku michango inayochangishwa na wanasiasa pasipo kufuata sheria za nchi kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa.
Agizo hilo amelitoa alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tukuyu alipokuwa akizindua maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Amesema hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya viongozi hususan viongozi wa vyama vya siasa kufanya kazi zao za kisiasa na kuitisha mikutano huku wakiwachangisha wananchi fedha pasipo kutoa stakabadhi kwa madai kuwa ziwasaidie kwenda Serikalini kuwatetea.
Akizungumzia malalamiko ya wananchi dhidi ya gharama mpya za maji zilizopandishwa na EWURA hivi karibuni kwa kiwango cha asilimia 125 kutoka Shilingi 2,000 mpaka 4,500 na gharama za matengenezo kutoka 500 mpaka 2,000, amesema viwango hivyo vinawaongezea ugumu wa maisha wananchi na kwamba alisema kuwa Serikali ya wilaya hiyo inalifanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment