Pages


Home » » WANANCHI WAONYWA KUACHA MARA MOJA KUTUMIA VIPODOZI HATARISHI.

WANANCHI WAONYWA KUACHA MARA MOJA KUTUMIA VIPODOZI HATARISHI.

Kamanga na Matukio | 02:35 | 0 comments
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bwana Paul Sonda, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.
 Mmoja kati ya madaktari waliohudhurua mkutano huo akivitambua baadhi ya vipodozi hatarishi na madhara yake, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.
 Baadhi ya aina ya Vipodozi hatarishi kwa binadamu
 Vipodozi hatarishi kwa binadamu
Baadhi ya madaktari waliohudhuria katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dokta Seif Mhina, akizungumza na madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi katika Ukumbi wa Youth Centre uliopo katika Jiji la Mbeya.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wananchi wametakiwa kuacha mara moja matumizi ya vipodozi hatarishi vilivyokatazwa na Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mkuu wa Kanda ya nyanda za Juu kusini Bwana Paul Sonda, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.

Ameviataja baadhi ya vipodozi kuwa ni MISS AFRICA, CITROLIGHT, COCODERM, CAROLIGHT, MAXLIGHT, EXTRA CLAIR, TOP LEMON PLUS, BETA SOL LOTION, LEMONVATE CREAM, JARIBU KWANZA, DIPLOSON, SUPER CLAIR, CLAIR MEN, FAIR AND HANDSOME, BIOCLARE, CAROTONE, MEDICATED FADE CREME, PRINCESS CLAIR, EPIDERM, BETASOL, IVAN HABART na SICAIRE.

Katika mkutano huo Bwana Sonda amesema kuwa watu wanaotumia vipodozi hivyo wanahatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa ya kupoteza fahamu, kansa ya damu, kansa ya ini, ubongo, pia kwa akina mama wajawazito kujifungua watoto wenye mtindio wa ubongo, muwasho mwilini na kunenepa kupita kiasi.

Mbali na athari hizo hudidimiza uchumi kwa waathirika kutokana na gharama kubwa za kutibu na wengine kupoteza maisha au kupata ulemavu na kwamba amesikitishwa na wananchi hao kwa kung'ang'ania kuendelea kutumia vipodozi hivyo na kuvipitisha kwa njia ya panya.

Hivi karibuni Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini waliteketeza vipodozi vyenye thamani ya shilingi milioni 129.

Hata hivyo Bwana Sonda amesikitishwa na kitendo cha wananchi wa Songwe ambapo vipodozi hivyo viliteketezwa baada ya kuchukua masalia ya vipodozi hivyo na kuvitumia.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger