Wahitimu wa Cheti Cha Usimamizi wa Kodi,wakifuatilia jambo wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo Cha Usimamizi wa Kodi (TIA).
*****
Na mwandishi wetu
Wahitimu wa vyuo mbalimbali mkoani Mbeya wameshauriwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali badala ya kukaa na kusubiri ajira kutoka Serikali.
Ushauri huo umetolewa na mkurugenzi wa Neema Decoration iliyopo Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini inayojihusisha na upambaji na usindikaji wa Waini aina ya Twinsi Bi.Sarah Mtalemwa.
Bi.Mtalemwa amesema shughuli za ujasiriamali humwezesha mwanachi kupata ajira na kipato kwa urahisi hivyo kuondokana na hali ya kuwa omba omba.
Wakati huo huo amewataka wanawake kujihusisha na biashara ndogondogo zitkazowaingizia kipato badala ya kuendelea na tabia ya kuwategemea waume zao kila kitu.
0 comments:
Post a Comment