MADAKTARI 72 WA HOSPITALI YA RUFAA WALIOGOMA WATIMULIWA KAZI -MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:21 | 0 comments
 Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari,wakifuatilia taarifa kamili za madaktari waliofukuzwa kazi Mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr  E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya
*******
Habari na Godfrey Kahango,Mbeya.
Sakata la mgomo wa Madaktari  katika hospitali ya Rufaa Mbeya, limeendelea kuingia katika sura mpya baada ya Madaktari 72, waliogoma kutimuliwa na bodi ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya.

Hatua ya kutimuliwa  kwa madaktari hao imekuja baada ya bodi hiyo kuwaandikia barua ya kuwataka  kukaa meza moja na kujadili mstakabali mzima wa madai yao ambapo wadaktari hao kukaidi wito huo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Mkuu wa Mkoa  wa Mbeya ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dr. Norman Sigalla, alisema kuwa wameamua kusitisha Mkataba wa madaktari hao na kuwarudisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

”Madaktari 54  ni wale walioko kwenye mafunzo ya vitendo kwa mkataba wa miaka miwili  na hospitali ya Rufaa  na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya” alisema Sigalla na kuwataka wale wote wanaoishi bwenini hospitalini hapo kuwa ifakapo saa 11:00 jioni ya leo(jana) wawe wameondoka katika eneo hilo la hospitali”alisema.

Alisema kuwa wamefikia hatua hiyo kwa kuwa madaktari hao wamekiuka , kuvunja mkataba wawalioingia  na hospitali hiyo pia kukiuka kanuni za kudumu za Umma na toleo la 2009, kifungu namba F16- F. 17 na F27.

 Alisema kuwa madaktari hao waliandikiwa barua ya mara ya kwanza ya kuwaita ili wakutane na Mwenyekiti wa bodi hiyo ya rufaa mbeya lakini walikaidi na kuandikiwa barua ya pili ya kuwataka waeleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kutofika kazini kwa siku tano lakini nayo waliikaidi.

Dr. Sigalla akizungumzia kuhusu madaktari  18 ambao ni waajiriwa pia wamo katika mgomo huo alisema kuwa nao wanakabidhiwa barua zao za kusimamishwa ajira zao hospitalini hapo na kuwarudisha Wizarani kwa katibu Mkuu  Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa hatua  stahiki za kinidhamu.

“Madaktari waajiriwa wanakabidhiwa barua zao za kusimamishwa ajira yao hospitalini hapa na kuwarudisha Wizarani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi  wa Jamii kwa hatua stahiki za kinidhamu” alisema Dr. Sigalla.

Hata hivyo gazeti hili lilishuhudia baadhi ya  madaktari hao wakiondoka kwenye mabweni yao huku madaktari hao wakisikika wakisema wapo tayari kurudi walikotoka na kwamba hawapo kuvumilia kile kinachoendelea hivi sasa.

“Tupo tayari kuondoka hospitalini hapa na kurudi tuliko toka wala hatutishiki hata kidogo” walisikika wakisema huku wakiwa wanapakia mabegi yao kwenye tax walizokodi. 

Wakati huohuo Jeshi la Polisi mkoania hapa lilizingira eneo la Hospitali ya Rufaa kuimarisha ulinzi na usalama.

AGOMA NDUGUYE KUZIKWA KATIKA JENEZA.

Kamanga na Matukio | 05:19 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkazi wa Kitongoji cha Mayewa,Kijiji cha Masanyila,Kata ya Igamba,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amegoma mwili wa nduguye  marehemu Onesha Nkota(Shilomanda) mwenye umri kati ya miaka 75 mpaka 80 kuzikwa katika jeneza.

Sakata hilo lililotokea Juni 27 mwaka huu majira ya saa nane mchana baada ya marehemu kufariki na Serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti  wake Bwana Nelson Mgode ulifanya jitihada za kuchonga jeneza lilogharimu shilingi 40,000 na kuliwasilisha nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya maziko.

Lakini badala ya kushukuru kwa wanakijiji kwa msaada huo,ndugu huyo wa marehemu alilikataa akidai kuwa kutokana na umri mkubwa marehemu alikula madawa mengi,hivyo yataidhuru familia yake na kwamba juyo tayari nduguye kuzikwa kwa jeneza.

Aidha siku hiyo hiyo,baada ya familia kutafakarei kwa yote yaliyotokea waliamua kumuomba radhi mwennyekiti wa kijiji lakini alikataa,bali mwenyekiti alidai uitishwe mkutano wa hadhara aombwe mbele ya wananchi.

Kufutia hatua hiyo majira ya saa nane mchana mkutano uliitishwa na Bwana Mgode kuomba radhi na kutakiwa kulipa gharama zilizotumika kutengenezea jeneza na ng'ombe mmoka kama adhabu ya kuwadharau wanakijiji.

Hata hivyo Bwana Mgode alilipa gharama hizo na ng'ombe mmoja aliyechinjwa siku hiyo hiyo na jeneza kukabidhiwa katika uongozi wa machifu kwa ajili ya taratibu nyingine za kimila huku ndugu zake wakimlaumu kwa kuendekeza imani za kishirikina.

WANANCHI WA KIJIJI CHA ISYONJE WAUVUA UONGOZI MADARAKANI,KUTOKANA NA KUIKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI.

Kamanga na Matukio | 05:19 | 0 comments
Hii ni barua ya kukiri ufujaji wa pesa.
*Mtunza hazina akiri kufuja fedha za kijiji.
*Mkutano wavurugika.
*Waunda kamati ya kusimia kijiji hicho.
*Diwani afunga mkutano.
 *******
Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe.
Wananchi wa Kijiji cha Isyonje,Kata ya Isongole,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wamemvua uongozi,mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Venance Daima na halmashauri ya kijiji kizima kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali na kutosimamia ipasanyo rasilimali za kijiji ikiwemo mianzi ya asili na mashamba ya kijiji.

Tuhuma hizo zimetolewa katika mkutano maalumu wa kijiji hicho uliofanyika Juni 28 mwaka huu mbele ya Diwani wa kata hiyo mheshimiwa Laurence Nyasa Mfwango,ambapo baada ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Ambokile Kinjisi na kubaini kuwa jumla ya shilingi 1,118,000 kufunjwa na mhasibu wa kijiji Bwana Michael Mbilinyi.

Aidha mhasibu huyo alipotakiwa kuonyeshwa pesa hizo zilipo alishindwa hali iliyompelekea kukiri kosa hilo na kuahidi kuzilipa Juni 29 mwaka huu baada ya kujiwekea dhamana ya shamba la miti.

Hata hivyo wananchi hao waliutupia lawama uongozi wa kijiji kwa kutosimamia mali ikiwa ni pamoja na uuzaji holela wa mianzi na ukodishwaji wa mashamba bila ridhaa ya wananchio na kutoitisha mikutano ya hadhara ikiwa ni kinyume na kanuni za Serikali ya kijiji.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya tuhuma hizo wananchi walimtaka mwenyekiti huyo na halmashauri yake kujiuzuru,ambapo walikubaliana na kijiji hicho kusimamiwa na kamati ya mpito,chini ya Afisa mtendaji wa kijiji Bwana Kinjisi.

Kutokana na wananchi kuchoshwa na uongozi  huo baadhi yao waliondoka mkutanoni kwa hasira  na viongozi wa kijiji kuacha viti vyao na kumuacha Diwani,ambaye alilazimika kufunga mkutano.baada ya mwenyekiti aliyeufungua mkutano huo na wananchi wakaridhia Kamati ya watu 10 kusimamia shughuli za kimaendeleo hadi uongozi mwingine utakapochaguliwa kwa mujibu wa kanuni za kijiji.

NYUMBA YA KULALA WAGENI YATEKETEA KWA MOTO - CHUNYA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:18 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Half London,inayomilikiwa na Bwana Raphael Mwasongole,mkazi wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku Juni 28 mwaka huu na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza vyumba zaidi ya 20 na kila kitu kilichokuwemo ndani yakiwemo magodoro na samani huku watu walikuwemo wamelala kunusurika kifo,baada ya kuvunja milango na madirisha na kubeba mizigo yao.

Kwa mujibu wa mmiliki wa nyumba hiyo Bwana Mwasongole,amesema ameshindwa kumudu kuuzima moto huo kutokana na uhaba wa maji na gari ya Zimamoto wilayani humo,ambapo moto huo uliendelea mpaka majira ya saa 12 asubuhi.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa,uliowaka katika moja ya vyumba na kuendelea katika vyumba vingine.

Wameongeza kuwa umeme katika nyumba hiyo haukuwepo kutokana na Luku kuisha,hali iliyopelekea kuwashwa kwa mishumaa katika vyumba.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea na pia thamani ya vyombo vilivyoteketea haijajulikana.

AFA BAADA YA KUJIFUNGIA NDANI NA KUJICHOMA KWA MOTO.

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Iziwa Wilaya ya Mbeya Vijijini Bi.Eva Tume(38),amefariki dunia baada ya kukusanya nguo zote na vyombo vyote ndani ya nyumba kisha kufunga mlango na kujichoma moto na kuteketea mwili wote.

Tukio hilo limetrokea Juni 26 mwaka huu,majira ya saa 12 jioni mara baada ya mumewe aitwaye Tume Mwalingo,ambaye ni mlinzi kuondoka nyumbani hapo na kuelekea kazini.

Aidha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Iwambala Bwana Asikile Mtafya,amesema siku hiyo majira ya mchana marehemu alionekana maeneo kadhaa akiwa mwenye hasira.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa pia na ugonjwa wa akili ambapo alikuwa akihudhuria kliniki katika Hospitali ya Rufaa kwa jalada namba 30/33/26.

Ametoa wito kwa wananchi walio na wagonjwa wenye matatizo ya akili kuwa nao karibu zaidi na uangalizi mzuri ili kuokoa maisha yao badala ya kuwaacha wao wenyewe.

Hata hivyo,Kamanda Diwani amesema uchunguzi umefanikiwa na mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa nfugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika Juni 17 mwaka huu..

HUKU NA KULE NA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:35 | 0 comments
  Mkazi wa Ilolo Jijini Mbeya,akiwa kwenye bustani ya mboga akifanya maboresho ya mboga kwa kupapalia,eneo hilo ni maarufu kwa kilimo cha mboga mboga ambapo kwa asilimia kubwa wakazi wa jiji la Mbeya hupata mahitaji ya mboga kutoka eneo hilo.
Watoto wakiwa wamebeba miwa kama walivyokutwa,umri wa watoto hao wanatakiwa kuwepo shule lakini wengi wao hawaendi shule na kuwa watoto wa mitaani,kutokana na ugumu wa maisha wazazi kukosa ada,yatima na waishio katika mazingira hatarishi..
Wanafunzi wa shule ya msingi Sinde ya Jijini Mbeya, wakiwa wanateka maji mtoni,ambayo si salama kwa afya zao kutokana na wakazi wa eneo hilo hutupia kila aina ya takataka(uchafu) huku wakiendelea kutumia maji hayo kwa kufulia nguo.(picha na Godfrey Kahango).

MFUME DUME WAATHIRI HALI YA UCHUMI KWA WANAWAKE.

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Habari na Ester Macha,Mbeya.
Kushamiri kwa mfumo dume katika wilaya ya Mbeya kunaathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi kwa wanawake ambao ndio nguvu kazi kubwa katika kilimo, kipato wanmachopata baada ya mavuno huishia mikononi mwa wanaume wanaojihusiusha na vitendo vya starehe na kusahau malezi ya familia zao.

Uchunguzi uliofanywa na Majira kwa takribani wiki moja  kwa msaada wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP)umegundua kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanavyofanyiwa wanawake wa vijiji vya Ifiga,Iwalanje na Nsongwi juu  Kata ya Ijombe vinavyotokana na nguvu ya wanaume ya kuhodhi mali zilizopatikana kwa kuwashirikisha wanawake.

Mmoja wa awanawake wa Kijiji cha Ifiga Bi Salah Jailos alisema kuwa wakati wa  msimu wa kilimo unapowadia  hushirikiana na waume zao kwa karibu bila kuwepo ugomvi wowote ndani ya familia zao mpaka  mazao yanapokomaa.

Alisema kuwa inapofika kipindi cha kuvuna wanaume  huanza kubadilika kwa kutafuta sababu mbali mbali  za kuonyesha chuki ndani ya nyumba ili aweze kupata sababu za kuvuna peke yake mazao na kuuza pepe yake bila kumshirikisha mke wake.

“Hali hii inatusikitisha sana kwani akishauza mazao haya huondoka nyumbani na kwenda kufanya starehe zake na wanawake wengine, lakini fedha baada ya kuisha hurudi nyumbani na kuanza kutafuta visababu vidogo vidogo kwa kuanza kudai chakula na kutoa sababu mbali mbali ikiwa  ni pamoja  na kudai kuwa chakula kibichi mara hufai kuishi na mimi mara nataka kuoa mke mwingine maadamu tu apate sababu za kujitetea ili mwanamke nionekane mbaya”alisema mwanamke huyo.

Mwanamke mwingine mkazi wa Usongwe Juu Bi.Benadeta Hamisi alisema kufutia vitendo hivyo vya wanaume tunaomba waache kwani iweje wakati wa kilimo  tulime wote lakini inapofika wakati wa mavuno wawe wababe wa kuuza mazao9 peke yao kwa ujumla huu ni ukatili wa kijinsia kwa sisi wanawake wa Kata ya Ijombe.

“Tunaomba waume zetu waache tabia hii kwani mazao haya tunalima sote hivyo hata wakati wa kuvuna inatakiwa tuwe pamoja na hata kuuza vile vile inatakiwa kusimama kwa pamoja kama mke na mume ioli fedha hizo zitakapopatikana mazao  na kuuza yaweze kusaidia kulea familia zetu pamoja na kusomesha”alisema Bi. Hamis.

Hata hivyo mwanamke huyo alisema athari ambazo wanapata baada ya kuachiwa familia ni kupata shida ya  kuhudumia familia ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto namahitaji mengine ya nyumbani ambayo ni muhimu.

Akizungumzia malalamiko hayo kwa Wanawake wa vijiji hivyo, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ifiga Bw.Raphael  Siyejele alisema hana taarifa za kiofisi za wanaume kuwanyanyasa wake zao labda kama zipo ngazi zingine.

KIONGOZI WA SERIKALI AONDOLEWA MADARAKANI KWA UBADHILIFU WA MALI ZA KIJIJI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:33 | 0 comments
Habari na Bosco Nyambege,Rungwe.
Wananchi wa kijiji cha Bumbiji kata ya Isange Mwakaleli wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamejikuta wakimwondoa mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya kujihusisha na ubatilifu wa mali za kijiji hicho.

Akizungumza na kituo hiki afisa mtendaji wa kijiji hicho ASWILE MWALUKASYA amesema wananchi hao wameamua kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na imani na kiongozi huyo kutokana na ufujaji wa fedha za kijiji kiasi cha shilingi laki tano.

Mwalukasya ameongeza kuwa mwenyekiti huyo anagubikwa na tuhuma za uharibifu wa mali ya kijiji kama simenti yenye thamani ya shilingi laki mbili pamoja nauuzaji wa miti ya kijiji hicho yenye thamani ya shilingi laki tatu ambayo ilikuwa itumike katika ujenzi wa nyumba za walimu kijijini hapo.

Wananchi wa kijiji hicho wamemtaka mwenyekiti huyo arejeshe fedha hizo ili ujenzi wa nyumba za walimu iweze kukamilika na kuondoa uhaba wa nyumba za walimu kijijini hapo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya isanga amethibitisha kutukia kwa tukio hilo na kuwasihi wananchi hao kuwa na subira kwani sheria itachukua mkondo wake.

SIKU 4 BAADA YA KITUO CHA AFYA KUZINDULIWA KWA MBIO ZA MWENGE WAUGUZI WATOWEKA - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:40 | 0 comments
 
Baadhi ya dawa zilizotelekezwa na wauguzi baada ya kukiacha kituo cha kazi,siku nne baada ya mwenge wa uhuru kukizindua kituo hicho(Picha na Ezekiel Kamanga).. 

*Dawa zakabidhiwa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kijiji.
*Wanawake wawili ambao ni wajawazito wajifungulia njiani.
 ******
Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Wakati Serikali ikiendelea na mchakato wa kuhakikisha huduma za kijamii zinasogezwa jirani zaidi na makazi ya watu,Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mpona,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,kimeachwa bila watumishi baada ya waliokuwa wamefikishwa kutoweka hali iliyochangia akina mama wawili wajawazito kujifungulia njiani.

Kituo hicho kimeachwa mikononi mwa Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Bahati Mwanguku na Mwenyekiti wake Bwana Nestory Mwashadewa.

Kittuo hicho cha Afya kilizinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Kepteni Honest Ernest Mwanossa,Mei 12 mwaka huu ambapo watumishi wawili wa afya walipelekwa kwa ajili ya kutoa huduma ambao ni Tabibu,msaidizi Bwana Manase Sinkamba na Muuguzi msaidizi Bi F. Mwaisakilaambao walitipoti kituoni hapo Mei 10 na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa kijiji hicho Mei 11 mwaka huu.

Aidha kituo hicho kilifunguliwa kwa furaha kubwa kutoka kwa wananchi wakati wa mbio za Mwenge wa uhuru,wakiamini kuwa ni ukombozi na changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwa sekta ya afya zimeisha.

Katika hali ya kushangaza wahudumu hao walitoka  kituoni Mei 16 mwaka huu wakidai kuwa wao waliazimwa tu kwa muda na kwamba walipewa siku 4 za kutoa huduma katika kijiji hicho hivyo hadi sasa kituo hicho hakifanyiwi kazi kufuatia adha kubwa kwa wananchi zaidi ya 2000,ambao walijenga kituo hicho kwa jitihada kubwa ambapo kiligharimu zaidi ya shilingi milioni 4.

Wananchi wameiomba Serikali kufanya haraka iwezekanavyo kuwaleta wahudummu wengi,ambapo akina mama wajawazito kujifungulia njiani kutokana na kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 8 kwani baadhi yao wamekuwa wakipanda mikokoteni na wengine kutembea kwa miguu.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba si muda mrefu waganga wa kituo hicho watapelekwa kijijini humo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Deodatus Kinawiro,amekiri kupokea taarifa za tatizo hilo ingawa amewataka viongozi wa kijiji hicho kuwasilisha malalamiko yao rasmi kwa barua ili aweze kuchukua hatua za haraka kukabiliana na adha hiyo kwa wananchi.

Kituo hicho cha afya mbali na kutoa huduma kwa wakazi wa kijiji hicho,ilikuwa isaidie vijiji vya jirani kutokana na Jografia ya wilaya hiyo kuzungukwa na makabila ya Maasai,Wasukuma na Wamang'ati ambao wamehamia wakiwa na mifugo.

DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO

Kamanga na Matukio | 03:40 | 0 comments
Pichani aliyesimama mwenye shirt jeupe ndie Dr Ulimboka wakati amabaye ni Kiongozi wa chama cha madaktari Tanzania Dk. Steven Ulimboka amefikishwa MOI baada ya kuokotwa akiwa mahututi eneo la Mabwepande. Picha za majeruhi yake ndio hiyo hapo chini. 
Mweneyikiti wa Jumuia ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka, amepigwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika.
 Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
********
Akisimulia tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa juzi usiku alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders Kinondoni.

Dk Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.

Alisema baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.

Dkt Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.

MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu na kumfahamisha tukio hilo.

Alisema alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.

Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.

"Hali yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli tumemleta hapa hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara ya kwanza nilishindwa hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa ameumizwa"alisema Dkt Deo

Alisema kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga walikuwa na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.

Aliongeza kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa akisikia mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga risasi.

Alisema wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na lengo la kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na kuangua chini.

Kwa upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba wanajitahidi kumpatia huduma za haraka.

Alisema kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.

POLISI
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo

MUHIMBILI
Wakati hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.

Pia inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.

Pia baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima miongoni mwao.
Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo [truncated by WhatsApp]

Kwa hisani ya http://tina-sweethome.blogspot.com

CCM:- WANACHAMA WENYE TUHUMA ZA UFISADI WATAENDELEA KUTOLEWA MADARAKANI.

Kamanga na Matukio | 05:24 | 0 comments

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),alipokuwa ametembelea Chuo Kikuu Cha Teofilo Kisanji(TEKU).
*******
 Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema bado kinaendelea na mchakato wa kuwaondoa madarakani wanachama wake wenye tuhuma za ufisadi na wale wasiokuwa na maadili mazuri kwa jamii, maarufu kwa jina la kuvua gamba.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye Jijini Mbeya alipozungumza na waandishi wa habari Jijini hapa.

Nape amesema kuwa dhana ya kujivua gamba ilipangwa kuwa na awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza ya kuwataka wahusika wawajibike wenyewe na imepita ingawa ilikuwa na mwitikio mdogo.

Kwa mujibu wa Nape awamu ya pili ya kujivua gamba ilipangwa kufanyika kupitia uchaguzi wa ndani ya chama hicho, na kuwa awamu hiyo ndio sasa inaendelea.

Amesema awamu ya tatu ni ya kuwawajibisha wahusika kupitia vikao vya chama, ambapo mpaka sasa tayari vikao vya kuwajadili viongozi wa juu wa chama hicho wenye tuhuma za ufisadi vimeanza na vitakapokamilika umma utashuhudia mageuzi makubwa ya uongozi wa chama hicho kikongwe nchini.

Aidha, Nape amesema katika awamu ya pili ya kujivua gamba ambayo inahusisha wanachama wote kutoa maamuzi kupitia uchaguzi, mchujo mkali utapitishwa kwa watakaoomba kugomea nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo wale wenye tuhuma majina yao hayatarudi.

MGOMO WA MADAKTARI KUTISHIA KUSITISHA MIKATABA YAO HUSUSANI WALIOPO KWENYE MAFUNZO - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:22 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Sakata la Mgomo wa Madaktari limeingia katika sura mpya Mkoani Mbeya baada ya Bodi ya Hospitali ya Rufaa Mbeya ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kutishia kusitisha mikataba ya madaktari waliogoma hasa wale ambao wako kwenye mafunzo ya vitendo.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Norman Sigalla amewaambia waandishi wa habari leo kuwa Bodi imefikia uamuzi huo baada ya kuona  madaktari hao wamevunja mkataba wao na hospitali hiyo ambao unawataka kufanya kazi bila kugoma.

Aidha, amesema kabla ya kuwaandikia barua hiyo, juzi bodi ya Hospitali ilikutana na kuwaita madaktari wote kwa barua ili wakae nao na kuwasikiliza madai yao lakini hakuna daktari hata mmoja aliyejitokeza kwenye kikao hicho.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria za kazi mtumishi asipofika kazini kwa muda wa siku tato mfululizo anakuwa amejifuta kazi mwenyewe, hivyo kama madaktari hao hawataripoti kazini kufikia leo, watalazimika kuwaondoa na kuwarejesha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ndiye aliwatuma kwenda kufanya mazoezi ya vitendo hospitalini hapo.

Akizungumzia madaktari waliosajiliwa ambao wanashiriki mgomo huo, Dk. Sigalla amesema  na wao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ndiye mwajiri wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk. Eliuter Samky amezungumzia madhara yaliyosababishwa na mgomo huo kwa wagonjwa, kuwa tangu madaktari hao kugoma kuwa wagonjwa waliofika hospitalini hapo kwa matibabu wameathirika kwa namna moja ama nyingine kwa kuwa hakukuwa na huduma ya kuridhisha.

WAUGUZI WAINGIA MITINI BAADA YA MBIO ZA MWENGE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:16 | 0 comments
 Zahanati ya Kijiji cha Mponwa,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya iliyofunguliwa katika mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa,imetelekezwa baada ya Wauguzi wawili kuondoka siku nne baada ya kituo hicho kuzinduliwa Mei 12,Mwaka huu na Kiongozi wa mbio za Mwenge Keptani Honest Erenest Mwanossa.
Aidha,madawa mbalimbali ya afya za binadamu yamefungiwa ndani na funguo kukabidhiwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wake,ambapo dawa hizo zipo hatarini kuharibika baada ya popo na bundi kuvamia jengo hilo kwa ajili ya makazi.
Jiwe la msingi la ufunguzi wa Zahanati hiyo kama kinavyoonekana.
Baadhi ya dawa zilizotelekezwa na wauguzi baada ya kukiacha kituo cha kazi,siku nne baada ya mwenge wa uhuru kukizindua kituo hicho.
 Kwa habari zaidi endelea kufuatilia matandao huu(Picha na Ezekiel Kamanga)..

KESI YA MWANAFUNZI WA TEKU ALIYEUAWA NA POLISI KUANZA KUSIKIKA MAHAKAMA KUU HIVI KARIBUNI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:23 | 0 comments
 Baadhi ya majeraha yaliyotokana na kipigo kwenye mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye alikuwa mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU),Mbeya aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi mkoani hapa tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
******
Habari na Mwandishi wetu.
Kesi ya mwanafunzi anayedaiwa kuuawa na Polisi Mkoani Mbeya,itaanza kusikika Juni 27 mwaka huu katika Mahakama Kuu,jijini Mbeya.

Mwanachuo huyo anayedaiwa kuuawa na Polisi marehemu Daniel Mwakyusa,aliyekuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) kilichopo jijini hapa,tukio lililotokea Februari 14 mwaka huu.

Imedaiwa marehemu na wenzake walikuwa katika sherehe ya Siku ya wapendanao duniani,ambapo marehemu aliuawa mita kadhaa kadhaa kutoka eneo la Grocery,huku ndugu wakisema marehemu aliuawa kwa sime na risasi kama inavyodaiwa na Jeshi la Polisi.

Kesi hiyo ambayo wananchi wengi walikuwa wakifuatilia inahusisha Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa kutumia Askari wake ambao ndio wanaodaiwa kusababisha kifo hicho.

Asasi mbalimbali zimekuwa zikilalamikia Polisi kujichukulia sheria mmkononi na kufanya vitendo vya unyanyasaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia badala ya kufuata majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana na jamii.

Kwa upande wake Mzazi wa marehemu,Bwana Godluck Mwakyusa amesema mwanae alimtegemea sana na tukio hilo limemfanya mara kadhaa kukosa amani,kufuatia majeraha ambayo mwanae alisababishiwa na Askari waliokuwa doria siku hiyo.

KIGANJA CHA MFANYABIASHARA KILICHOKATWA CHAMSABABISHIA KIFO MWENYEJI.

Kamanga na Matukio | 03:23 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mkazi wa Kijiji cha Mpona Malanfali,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mwile Hassan(23),ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kumkata kiganja mfanyabiashara Bi.Judith Mpamba(47),mkazi wa Kijiji cha Iwindi,Kata ya Iwindi Wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa.

Marehemu alikamatwa usiku Juni 21 mwaka huu,akidaiwa kumkata kiganja mfanyabiashara huyo wa ufuta aliyefika kijijini hapo akiwa na mwenzie Bwana Helman Mwalindu(37) ambao walifika kijijini hapo kwa lengo la kununua ufuta.

Marehemu Mwile akiwa na mtuhumiwa mwenzake Bwana Frank Nzovu(Tembo) ambaye alitokomea kusikojulikana na ni mwenyeji wa Kijiji cha Ikonya,Wilaya ya Mbozi,walifika nyumbani kwa Bwana Shigela ambapo waliwachukua wafanyabiashara hao hadi eneo la shamba walikodai kuwepo kwa ufuta.

Baada ya kufika eneo hilo hali ilikuwa ndovyo sivyo baada ya vijana hao kugeukia wafanyabiashara hao na kuwatishia mapanga wakidai wapewe pesa,ambapo Bwana Mwalindu alitoa pesa taslimu shilingi 860,000 na Bi.Mpamba alitoa shilingi 700,000 baada ya kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto na wahalifu kutokomea kusikojulikana.

Kufuatia tukio hilo majeruhi walitoa taarifa katika Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Bahati Mwanguku na Mwenyekiti Bwana Nestory Mwashadema,ambao nao walitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Galula na walifika eneo la tukio na kuwa tafuta watuhumiwa bila mafanikio.

Polisi walirudi siku ya pili kwa ajili ya kukitafuta kiganja cha mkono cha Bi Mpamba ambapo walifanikiwa kukikuta na majeruhi kukiwakilisha kituoni hapo na kukimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi May 26 mwaka huu,siku moja baada ya tukio hilo majira ya saa sita mchana.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Mwanguku,amewataja watuhumiwa wanaodaiwa kumkata kiganja mwanamke huyo kuwa ni pamoja na Karim(anayedaiwa kushika kisu),Frank Nzovu(alishika panga),Shigela na Mwile Hassan.

Watuhumiwa hao baada ya kutoroka ndipo wananchi walianza msako mkali na kufanikiwa kumkamata Shigela na Mwile Hassan,ambaye alikamatwa Juni 21 mwaka huu usiku akiwa amejificha kichakani baada ya kutoroka kwa baba yake Bwana Hassan Mwahasanga(60) kilometa 8 kutoka eneo la tukio kijiji cha Masalamba,Chunya.

Katika mapambano wananchi wenye hasira kali walimkamata mtuhumiwa hadi Ofisi ya kijiji na baada ya kupishana na Afisa Mtendaji wa kijiji,waliamua kuchukua matita ya ufuta na petroli ndipo walipoamua kuwasha moto na kumteketeza mtuhumiwa ambapo kifua ba kichwa ndivyo vilisalia.

Polisi walifika eneo la tukio saa moja baada ya tukio kufanyika majira ya saa 5 asubuhi na kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na mara baada ya kukamilika ndugu wa marehemu walikabidhiwa kwa ajili ya masomo.

Baba wa mtuhumiwa Bwna Hassan Mwahasanga,amethibitisha kuwa mwanae ndiye aliyeuawa ingawa ameeleza kuwa hajui chanzo cha tukio.

Aidha wananchi wa kijiji hicho,ambao hawakupenda majina yao kutajwa,wamesema wamechoshwa na tabia za vijana wa hao kijijini hapo na wao wameamua kufanya hivyo ili iwe onyo kwa vijana wengine kujihusisha na vitendo vya uporaji.

Mazishi ya marehemu yamefanyika katika Kijiji cha Totowe Juni 22 mwaka huu.

Wimbi la nwananchi kujichukulia sheria mkononi limekithiri ingawa lawama hutupiwa Polisi na mahakama kwa kuwaachia huru watuhumiwa  na wanachi wamekuwa hawapo tayari kutoa ushahidi hivyo mahakama huwaachia huru kwa kukosa ushahidi.

BREAKING NEWS:-MAFUTA AINA YA DIESEL ZAIDI YA LITA 3,500 YAIBIWA.

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
*Madumu 211 yakamatwa na mapipa 16 katika nyumba za makazi, mtaa wa Mwaka,Mji mdogo wa Tunduma na Jeshi la polisi lashindwa kuyatolea maamuzi. Vijana wafanya vurugu wakitaka kuyateka wakati mafuta hayo yakirudishwa kambini.

*Vijana wapangwa na kiongozi wa Chama pinzani ilikuvunja vibanda zaidi ya 30 vya biashara vilivyopo karibu na eneo la makaburini Tunduma.Mkuu wa Wilaya ya Momba aingilia kati.

*Uongozi wa serikali ya kijiji wauza miazi ya kijiji kwa shilingi 1,600,000 wananchi wazuia gari la mteja wadai ni hujuma,viongozi wa kijiji watokomea kusikojulikana.


Ronaldo aipeleka Portuguese nusu fainali

Kamanga na Matukio | 05:01 | 0 comments
Mchezaji wa Czech Republic's Theodor Gebre Selassie (shoto) wakigombania mpira na mchezaji wa Portugal's Cristiano Ronaldo kipindi cha kwanza katika ya robo fainali ya Uefa Euro 2012,

Bao la ushindi lilipatikana katika dakika ya 79 kwa kicha kikali alichofunga Cristiano Ronaldo dhidi ya Czech Republic, na kusabisha  ushindi wa 1-0 huku wakiwa wanasubiri, fahari wawili kati ya Spain na France, katika mechi ya robo fainali itakayochezwa siku ya jumamosi  Juni 23, 2012. Matokeo ya mchezo huu Czech Republic 0-1 Portuguese.

MWENYEKITI WA KIJIJI ATAFUNA PESA ZA ZAHANATI YA KIJIJI.

Kamanga na Matukio | 05:00 | 0 comments
*Afisa mtendaji wa Kata akaa kwenye kituo zaidi ya miaka 20.
*Afisa Mtendaji wa Kijiji naye ajimegea shilingi 380,000.

Mkataba wa ahadi ya kulipa fedha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Masanyila,anaedaiwa kufuja pesa taslimu shilingi 2,350,000 za zahanati ya kijiji.
******

Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Masanyila,Kata ya Igamba,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bwana Chepson Mkanjilwa,anatuhumiwa kuiba pesa taslimu 2,350,000,kati ya shilingi milioni 12 zilizotolewa na Halmshauri ya Mbozi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho iliyogharimu zaisi ya miliozi 24 lakini mpaka sasa haija kamilika.

Katika katika mkutano uliofanyiaka Julai 21 mwaka 2011 mwenyekiti huyo,alikirikutumia pesa hizo kwa matumizi yake binafsi na alipobanwa siku hiyo alitoa shilingi laki mbili na salio la 2,150,000 kuahidi mbele ya mkutano huo wa hadhara kwa uthibitisho wa kuweka saini kwenye barua ya mkataba mbele ya Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Justin Mgala lakini hajazirejesha.

Kufuatia hatua hiyo Wenyeviti wa vitongoji 6 vya Kijiji hicho walikutana na kumwalika Diwani wa Kata hiyo mheshimiwa Amos Kalonge,lakini hali ilikuwa ndivyo sivyo kutokana na mwenyekiti na afisa mtendaji wa kijiji kuingia mitini.

Katika hali hiyo isiyokuwa ya kawaida Afisa mtendaji Bwana Mgala,anatuhumiwa kwa kufuja shilingi 380,000 alizokabidhiwa na Mkandarasi kwa ajili ya kununulia mchanga wa kujengea nyumba ya Daktari wa zahanati ya kijiji na mpaka sasa haonekani ofisini kwake,licha ya kupewa uhamisho kwenda kijiji kingine huku wananchi wakiwa hawajui la kufanya.

Kwa upande wake Mheshimiwa Kalonge,aliwataka viongozi hao na wananchi kuahirisha mkutano huo hadi Juni 27 mwaka huu na atamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ili waweze kusikiliza kero za wananchi wa kijiji hicho.

Aidha,wananchi hao wamemtupia lawama Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bwana Ambakisye Waya,,ambaye amedumu katika kata hiyo kwa takribani miaka 20 sasa na kudai kuwa amekifanya kijiji kama mradi wake wa kufuja fedha kupitia watendaji wa vijiji na akishatimiza azma yake huwahamisha watendaji hao vituo vya kazi hali inayopelekeza pesa za wananchi kupotea ovyo.

Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bwana Levson Chilewa,amekiri kupokea malalamiko ya kijiji hicho na kwamba ofisi yake ilituma mkaguzi hivyo taarifa yake ataitoa siku za hivi karibuni.

YACHEKESHA LAKINI PIA YASIKITISHA,UBISHI WACHANGIA PIA AJALI YA CANTER - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:58 | 0 comments

 Gari aina ya Canter Toyota ikiwa imetumbukia katika mto Jianga maeneo ya Ilolo Jijini Mbeya,  baada ya kuvunjika kwa daraja na katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa. Lakini wakazi wa eneo hilo walieleza kwamba daraja hilo ni bovu toka muda mrefu na viongozi wao hawajafanya jitihada zozote juu ya ubovu huo.( picha na Godfrey Kahango).
 Mmmh jamani hatari
Wakazi wa eneo la jirani na tukio la ajali waliofika kudhuhudia tukio hilo.

Hata hivyo kufuatia tukio hili,Kata za Ilemi,Sinde na Isanga zinapaswa kukutana katika meza moja ya mazungumzo kwa ajili ya kujenga daraja hilo ambalo ni kiunganishi cha kila pande na mara nyingi limekuwa likitumiwa na wagonjwa kwenda Kituo cha Afya cha Mwanjelwa na katika shughuli mbalimbali za kitaifa za kimaendeleo.

CHUPUCHUPU DIWANI WA UPINZANI KUPATA KIPIGO MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:57 | 0 comments
Na. Shomi Mtaki, Tunduma
Tabia ya viongozi wa Chadema kuchanganya masualaya yaushabiki wa kisiasa na kufitinisha wananchi na viongozi wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) katika mikutano yake vya hadhara pamoja na vikao vya baraza la halmashauri ya mji wa Tunduma wlayani Momba, nusura kiongozi mmoja wa chama apate kipigo.

Kiongozi huyoi Frank Mwakajoka ambaye ni diwani wa kata ya Tunduma (Chadema), alinusulika kipigo hichojana  kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Mji huo baada ya kuwatukana wajumbe katika kikao hicho kilichafanyikia ndani ya ukumbi wa hoteli ya Flamingo mjini hapa.

Tukio hilo lilitokea katika kikao hicho kufuatia hoja ya mwenyekiti wa mtaa wa Tukuyu Kenneth Mwankuga, kutaka ufafanuzi wa kauli za viongozi wa Chadema, kudai katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivikaribuni katika mtaa wake kuwazushia uongo viongozi wa  CCM kuwa wameuza soko la Majengo.

 Mwankugha alisema viongozi hao akiwemo diwani huyo walifanya mkutano wa hadhara, katika eneo hilo na kuenezauzushi huo na kudai kuwa uongozi wa Chadema umepinga hatua hiyo jambo ambalo halikuwa sahihi.

Hivyo kupitia Baraza hili naomba nipate ufafanuzi ili zaidi ili niwapelekee wananchi majibu sahihi maana viongozi hao tunao katika kikao hiki,” alisema Mwankuga.

Hoa hiyo iliungwa mkono na wajumbe wengine wanaotokana na   CCM na kumtaja diwani huyo kuwa ndiye aliyetamka maneno hayo na kuwa amekuwa na tabia ya kutengeneza uchochezi kila mara   anapofanya mikutano ya hadhara mjni hapa.
 
Wajumbe hao walisema diwani huyo akishirikiana na viongozi wa chama chake, amekuwa mstari wa mbele kusababisha kutoweka kwa amani na kuzusha vurugu zisizo za msingi zinazojitokeza mara kwa mara katika mji huo

Hata hivyo maneno hayo yalimfanya diwani huyo asimame na kuanza kukanusha taarifa hiyo kwa madai kuwa yeye ndiye aliyekuwa akitetea kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo.

Hata hivyuo diweani huyo alianza kutoa lugha chafu dhidi ya wajumbe wa mkutano huo akisema,“acheni ujinga wenu,hakuna mnachosali mtaendelea kubaki hivyo hivyo na tena nawaambieni kesho (leo) nitaitisha mkutano mwingine niwaambie wananchi ujinga wenu” alisema.

Wakati diwani huyo akiendelea kuongea, kelele za wajumbe hao na baadhi ya wa Chadema walianza mzozo huku wajumbe wengine wakiwa wamemzonga diwani huyo kwa lengo la kumpa kipigo kufuatia kauli zake hizo,ambazo hazikuwaridhisha baadhi ya  wajumbe wa baraza hilo.

Mzozo huo uliochukua takribani dakika 20, ulifanya hali ya kikao kutoeleweka ambapo baadhi ya wajumbe walitaharuki na kuwaondolea utulivu kufuatia kuendelea kulizungumzia jambo hilo badala ya kujadili agenda zilizo mbele yao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga alikanusha kuwapo kwa jambo hilo na kuwataka wajumbe wasiingize mambo ya mtaani kwenye vikao badala yake wawe makini kujadili mambo ya msingi.
 
Akizungumzia suala hilo Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),ta ya Tunduma Hemed Steven aliwataka wajumbe hao kuacha kuingiza Siasa kwenye vikao vya maendeleo badala yake wafanye majukumu waliyotumwa na wananchi.

“Tujue siasa inatumika wapi na wapi ni masuala ya maendeleo haya yaliyotokea mimi nasema wajumbe watambue majukumu waliyotumwa na wananchi huo ndiyo ujumbe wangu sina zaidi I have no comment ”alisema Steven.

Naye Mwenyekiti wa Jimbo la Magharibi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Joseph Mwachembe alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema CCM watambue kuwa chadema hakiwezi kuwasifia bali kitaendelea kuwafitinisha na wananchi.

KIONGOZI WA SERIKALI ATUHUMIWA KWA KOSA LA KUFANYA UDANGANYIFU BENKI NA KUJICHUKULIA MAMILIONI YA PESA.

Kamanga na Matukio | 04:01 | 0 comments
Habari na Gabriel Mbwille,Mbeya.
Ofisa mtendaji wa Kata ya Nsalaga Bwana Cyprian Matola anatuhumiwa kuwadanganya watia saini benki na kuchukuwa shilingi milioni 2 na laki 8 za ujenzi wa sekondari ya kata kinyume cha taratibu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Kamati teule iliyoundwa kufuatilia ujenzi wa shule ya sekondari Uyole, Jelly Mwakipesile wakati akitoa taarifa ya kamati kwenye kikao cha Maendeleo cha kata hiyo.

Kamati hiyo iliundwa kutokana na kuwepo kwa taarifa, juu ya utaratibu mzima ambao haukuwa sahihi wa utoaji wa fedha benki na kupelekea kukwama kwa kazi hiyo ya ujenzi wa shule ya sekondari Uyole wakati fedha za ujenzi zilikuwa zimetolewa.

Aidha amesema fedha iliyokuwa ikichukuliwa benki na Ofisa Mtendaji Matola, ilikuwa inatunzwa UWAMU Saccos katika akaunti ya mtu binafsi hali iliyomfanya m,tendaji huyo awe anaizalisha fedha hiyo ya serikali kwa manufaa yake.

Nao wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya kata hiyo, walimtaka mtendaji Matola arudishe fedha hizo zilizotumika kinyume na taratibu na pia taarifa ifikishwe kwa Mkurugenzi wa jiji la Mbeya.

Jitihada za kumtafuta Mkurugenzi wa jiji, Juma Idd kuzungumzia suala hilo zimeshindikana kutokana na simu zake za kiganjani kutopatikana sanjari na kuwa nje ya ofisi kikazi.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger