Mwili wa marehemu amabye jina lake halikuweza kufahamika katika kijiji cha Nsonyanga, wilaya ya Mbarali anadaiwa kuiba baiskeli ya mwananchi wa kijiji hicho.
Mahali ulipokuwa umefukiwa mwili wa marehemu huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, katika kijiji cha Nsonyanga, wilaya ya Mbarali
*****
Na mwandishi wetu.
Mtu mmoja anayedaiwa kuiba baiskeli wiki lililopita katika kijiji cha Nsonyanga wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambaye jina lake halikuweza kufahamika, ameuwawa na wananchi wenye hasira kali katika kijiji hicho.
Baada ya kukuta mwili wa marehemu katika shamba lake, mkulima na mmiliki wa shamba hilo ambaye jina lake aliamuka ewenda kutoa taarifa katika ofisi ya serikali ya kijiji kwa Kaimu mtendaji wa serikali ya kijiji hicho Bwana Pius Malila aliamua alienda kutoa taarifa za tukio hilo katika Kituo cha Polisi cha Igurusi.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na askari polisi wa nne na madaktari wawili kutoka Kituo cha afya cha Igurusi na kuamuru wananchi kuuzika mwili huo ambapo ruhusa hiyo ilitolewa majira ya saa 7 mchana lakini mwili huo haukuzikwa mpaka majira ya saa moja usiku.
Je, kama maiti haikuweza kufahamika kwanini isitanganzwe kama kuna ndugu waweze kujitokeza kuuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika kwani kisheria baada ya siku saba kama mwili wa marehemu haujatambuliwa ndipo serikali huchukua jukumu la kuzika kuna agenda gani kijijini hapo kama mtuhumiwa alikamatwa? Je. Dhana ya jeshi la polisi la ulinzi shirikishi itafanikiwa? Na kwanini kijiji hakikumpeleka mtuhumiwa katika vyombo vya dola, badala ya wao kuamua kujichukulia jukumu la Polisi, mahakama.
Marehemu alivalia mavazi tisheti nyeusi, singleti nyeupe iliyoandikwa michigani na suruali ya rangi nyeusi rangi ya ngozi yake ni maji ya kunde.
0 comments:
Post a Comment