Na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Zaidi ya
shilingi 25.9 milioni zimeahidiwa kutolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo katika
halmashauri ya wilaya ya Chunya ili kufanikisha ujenzi wa chumba cha kuhifadhia
maiti(mochwali) katika hospitali ya wilya ya chunya ili kuhakikisha changamoto
hiyo inatoka hospitalini hapo.
Wadau hao wa
maendeleo katika halmshauri ya wilaya ya
Chunya wametoa ahadi hizo katika kikao na mkuu wa wilaya ya Chunya Elias John Tarimo kujadili ujenzi wa Chumba
cha kuhifadhia maiti(Mochwali) katika hospitali ya wilaya ya chunya ili
kuhakikisha miili ya marehemu inasaminiwa.
Tarimo
alisema ameamua kuwaita wadau wa maendeleo katika halmshauri ya wilaya ya
chunya ili kuwahamasisha katika suala zima la kufanikisha mara moja ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya wilaya kutokana na umuhimu wake kwani ni aibu kwa wilaya kongwe
kama Chunya kukosa sehemu ya kuhifadhi maiti.
Alisema
lazima watambue kila mtu ni marehemu mtajiwa hivyo ni wajibu wa kila mmoja
kuona umuhimu wa kuchangia fedha ili kuhakikisha halmashauri inapata jengo la
kuhifadhia maiti.
Aidha wadau
waliohudhuria kikao hicho kwa kuona umuhimu wa jambo hilo wameweza
kujitoa kwa kupeleka mawe na mchanga lori
11,mifuko ya cement 229,na kutengeneza mirango na madirisha kwenye jengo la
hilo kwaajili ya kuanza ujenzi mara moja na kuazimia kwamba ifikapo desemba mwaka huu
wawe wamekamilisha ujezi wa jengo la kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
Mbali na
kutoa michango mbalimbali waliweza kuunda kamati itakayokuwa ikifwatilia kwa
ukaribu ujenzi wa jengo la hilo la kuhifadhia maiti hospitalini hapo ili
kuhakikisha kasi hiyo inaendana na makubaliano hayo.
0 comments:
Post a Comment