Pages

Home » » MTO LUPA - CHUNYA - MBEYA AMBAO NI TEGEMEZI KWA WANANCHI HATARINI KUKAUKA

MTO LUPA - CHUNYA - MBEYA AMBAO NI TEGEMEZI KWA WANANCHI HATARINI KUKAUKA

Kamanga na Matukio | 05:04 | 0 comments

Mto Lupa uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya.
 *****
Na mwandishi wetu.
Mto Lupa ambao ni tegemezi kwa huduma ya maji katika kijiji cha Lupa wilayani Chunya mkoani Mbeya upo hatarini kukauka endapo hatua za haraka za kudhibiti uharibifu wa mazingira hazitochukuliwa na uongozi wa Wilaya hiyo.

Kwa sasa mto huo unaonekana mithiri ya bwawa kutokana na maji yake kutuama ikiwa ni pamoja sehemu nyingine za mto huo kuwa kavu kabisa.

Mwandishi wa mtandao huu ameshuhudia baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Lupa wakichimba mashimo ndani ya mto huo ili waweze kupata maji safi kutokana na mto huo kukauka maji.

Mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na utunzaji wa misitu ya asili ya Kaeya bwana Lukasi Malangalila ameitaja sababu ya mto huo kukauka kuwa ni kilimo holela pembezoni mwa mto pamoja na ukatwaji wa misitu ya asili ambayo imekuwa ikihifadhi maji.

Share this article :

0 comments:

Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger