Pages


Home » » MBUNGE WA JIMBO LA MBARALI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU

MBUNGE WA JIMBO LA MBARALI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU

Kamanga na Matukio | 05:57 | 0 comments
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
*****
Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mwalimu Dickson Kilufi atafikishwa mahakama ya mkoa wa Mbeya siku ya jumatatu tarehe Oktoaba 10, mwaka huu baada ya kudaiwa kutishia kuua kwa maneno Machi 15, mwaka huu katika Ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbarali.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema mbunge huyo amedhaminiwa baada ya kukamatwa juzi na kushikiliwa na Jeshi la polisi ambapo Mwanasheria wa serikali alikubali dhamana iliyotolewa jumamosi ya Oktoba 8, mwaka huu.

Mbunge Kilufi anadaiwa kumtishia kumuua Afisa mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bwana Jordan Masweve mbele ya diwani wa kata hiyo Bwana Alex Mndamlage.

Kwa taarifa zinadai kuwa kumekuwa na mvutano wa muda mrefu wa kiutendaji baina ya Mbunge Kilufi na Afisa mtendaji huyo Bwna Masweve hali iliyopelekea kuamishwa kwa Afisa mtendaji huyo kutoka Kata ya Mawimbi na kupelekwa kituo cha sasa anachoendelea kufanya kazi cha Kata ya Ruiwa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger