*****
Na mwandishi wetu
Na mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abassi Kandoro amesema katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa waalimu kwenye shule za sekondari na msingi Serikali inatarajia kuajiri waalimu 6,662 kufikia mwezi January mwakani.
Ameyasema hayo wakati akifungua maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yanayoendela katika viwanja vya Raunda Nzovwe vilivyopo kata ya Ilomba jijini Mbeya.
Amesema kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru mkoa wa Mbeya umefanikiwa kuwa shule za msingi 1165, Sekondari 268, za sekondari ambazo zina kidato cha tano zipo 19 ambapo wakati tunapata uhuru mkoa wa Mbeya ulikuwa na shule nne za sekondari ambazo ni Sangu, Loleza, Rungwe na Iyunga.
Aidha Kandoro amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni ili waweze kuondokana na ujinga ikiwa ni pamoja na kuongezewa uwezo wa kujitegemea.
0 comments:
Post a Comment