Bwana Daniel Mtuka(Kulia) Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya akiwa na Bwana Omari Mtimbo wa kitengo cha elimu kwa Umma wakiwa katika ukumbi wa Mount Livingstone jijini Mbeya.
*****
Kamanda wa TAKUKURU mkoani Mbeya Bwana Daniel Mtuka amesema kuwa kuna udhaifu mkubwa umejitokeza ugawaji wa pembejeo za kilimo katika miaka iliyopita na amebainisha kwamba kamati za vocha za wilaya kuwekuwemo na mianya ya upotevu wa vocha za ruzuku ambapo maafisa kilimo na maafisa ugani wa wilaya wamesema chanzo cha tatizo hilo ni uchache na kuchelewa kufika kwa pembejeo.
Ameeongeza sababu nyingine kuwa kutotolewa taarifa sahihi za maeneo husika na posho ndogo kwa kamati za vijiji ambazo hupewa shilingi elfu kumi na maafisa ugani kuwewa shilingi elfu arobaini kwa msimu mzima hali inayowashawishi kujiingiza katika mianya ya rushwa na mawakala kutokuwa waaminifu.
Bwana Mtuka amesema kutokuwa na mikataba baina ya serikali na mawakala, ambapo mawakala wamekuwa wakitumia uthaifu huo kuwarubuni wakuliwa pembejeo, na wananchi kutoshirikishwa katiaka uteuzi wa watu wanaositahiuli kugaiwa pembejeo za kilimo na vocha za ruzuku.
Amesema kuwa wakulima wengi wanakabiliwa nan janga la kukosa elimu ya kutosha kuhusiana na matumizi ya pembejeo za kilimo na vocha za ruzuku hali isayosababisa kurubuniwa na viongozi wao.
Kamanda wa TAKUKURU Bwana Mtuka amehitimishwa kwa kusema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa Maafisa na mawakala watakaohusika na udanyanyifu kwa maslahi yao binafsi, kufuja na kushindwa kuwatendea haki wakulima katika ugawaji wa pembejeo za kilimo na pocha za ruzuku kwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment