Rais wa TFF amewataka wadau wa soka kuwa katika hali ya utulivu.

Kamanga na Matukio | 06:18 | 0 comments


  Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga 
 =====

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga amewataka wadau wa soka kuwa katika hali ya utulivu, katika kipindi hiki cha kuusubiri ujumbe wa shirikisho la soka duniani ambao utakuja nchini mwezi ujao kwa ajili ya kutatua sakata la uchaguzi wa TFF.Tenga ametoa rai hiyo kwa wadau, baada ya hali ya utulivu wa soka kuingia dosari kufuatia kila mtu kusema lake baada ya kamati ya rufa ya uchaguzi inayoongozwa na Iddi Mtiginjola kuliengua jina la aliekua mgombea wa nafasi wa uraisi wa TFF Malali Malizi kwa kigezo cha kukosa sifa za kugombea.Hata hivyo Tenga ametoa msisitizo kwa wadau wa soka nchini kutambua kwamba sakata la uchaguzi wa TFF katu halitochukua mustakabali wa maandalizi ya mchezo wa kuwani nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia ambapo timu ya taifa Taifa Stars itapambana na timu ya taifa ya Morocco mwezi ujao.

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amesema nafasi ya kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger haipaswi kuhojiwa'

Kamanga na Matukio | 06:17 | 0 comments

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amesema nafasi ya kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger haipaswi kuhojiwa na wachezaji wa timu hiyo wanapaswa kuwajibika kwa matokeo mabaya.Matumaini ya Arsenal kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamekuwa finyu baada ya kukubali kipigo nyumbani cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Munich ya Ujerumani.Jumamosi iliyopita Arsenal ilipata pigo lingine baada ya kubanduliwa katika Kombe la FA kwa kufungwa bao 1-0 na Blackburn Rovers.Wilshere amesema Wenger ameifundisha klabu hiyo kwa miaka 16 na amekuwa akifanya kazi nzuri hivyo hauwezi kuhoji kuhusu uwezo wake.Arsenal kwasasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza wakiwa nyuma ya Tottenham Hotspurs kwa alama nne hivyo wana kibarua kingine cha kuhakikisha wanamaliza katika nafasi nne za juu ili waweze kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli unatarajiwa kutumika katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014.

Kamanga na Matukio | 06:16 | 0 comments


Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limethibitisha kuwa mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli unatarajiwa kutumika katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014.Mfumo huo ulitumika kwa mafanikio katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyofanyika Desemba mwaka jana na pia itatumika katika michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika Juni mwaka huu.Rais wa FIFA mara kwa mara amekuwa akipigia debe mfumo huo toka alipoona bao halali alilofunga kiungo wa Uingereza Frank Lampard likikataliwa na kupelekea nchi hiyo kufungwa na Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia 2010.FIFA katika mkutano wake wa mwaka jana ilipitisha mifumo miwili ya Goalref na Hawkeye ambayo yote kwa pamoja ilitumika katika michuano ya klabu bingwa ya dunia.

WINGU ZITO LATANDA VITENDO VYA UJAMBAZI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:36 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtikisiko mkubwa umeukumba Mkoa wa Mbeya kutokana na vitendo vya ujambazi vilivyotokea hivi karibuni, likiwemo la Askari wa Jeshi la Polisi kuawa katika Wilaya ya Chunya mkoani humo.

Mbali na askari polisi kuuawa pia majambazi walimuua kwa kumpiga risasi Mzee Cosmas Kunzugala mkazi wa Airpot, Jijini Mbeya, akiwa nyumbani kwake baada ya kugongewa  mlango na watu wasiofahamika.

Tukio jingine limetokea Mafinga ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Festo Kyando(47), akiwa na msaidizi wake katika gari waliuawa kisha kuzikwa katika msitu wa Mafinga, kabla ya Jeshi la polisi mikoa ya Iringa na Mbeya kugundua na kuifukua Februari 18 na kuisafirisha hadi Mbeya Februari 19 mwaka huu na miili hiyo kuzikwa upya.

Akiongea na mtandao huu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman amesikitishwa na vitendo hivyo na kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi ili kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vinavyofanya wananchi kuishi  kwa hofu pia kuwafanya watu wanaotaka kuwekeza  mkoani hapa kuogopa na kuufanya mkoa kudumaa kiuchumi.

aidha Kamanda huyo wa polisi amesema Jeshi lake linafanya kila jitihada ili kubaini wale wote waliohusika na vitendo hivyo ambavyo vinatia doa Mkoa wa Mbeya.

Katika tukio la dereva na tingo wake kuuawa mali ya zaidi ya shilingi milioni 800 iliporwa na majambazi hayo kisha gari kutelekezwa Makambako.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI MATATANI KWA KUTAKA KUWAHAMISHA WANANCHI.

Kamanga na Matukio | 05:21 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya imeingia matatani kufuatia wananchi zaidi ya 400, wanaoishi eneo la Masaki Kijiji cha Ichenjezya, Kata ya Vwawa lenye chanzo cha maji kutakiwa kuondoka eneo hilo, na wao kupinga agizo hilo wakidai kulipwa fidia za mali zao kutokana na nyumba za watendaji wa Serikali kuachwa.

Wananchi hao walionekana kukasirishwa na Halmashauri hiyo kufuatia nyumba zao kuwekewa alama nyekundu ya X na bango ya kuwataka kutofanya shughuli zozote za kibinadamu kuanzia Februari 18 mwaka huu ikiwa ni pamoja na kusitisha ujenzi.

 Hata hivyo Diwani wa Kata ya Vwawa Richard Kibona amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wake na suala lao kulipeleka katika Ofisi ya Halmashauri ya wilaya hiyo lakini amekuwa akipigwa danadana na maafisa wa halmashauri hiyo.

Aidha, diwani huyo ameeleza kukerwa na kauli za maafisa hao wa halmashauri kwa kutokuwa wakweli na kumbebesha jukumu nzito la lawama kuwa yeye ndiye asuluhishe mgogoro huo, wakati wakifahamu kuwa suala hilo linatakiwa kujibiwa kitaalamu kutokana na wananchi kumiliki kihalali viwanja na nyumba zao.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake na kueleza kuwa yeye ni Daktari alikataa kata kata kuzungumzia suala hilo kuwa hana mamlaka ya kujibu, akidai kuwa Mkurugenzi ndio mwenye uwezo wa kulizungumzia.

Kutokana na bugudha hiyo kutoka kwa wananchi wake Diwani Kibona alisema wananchi wanamhitaji Mkuu wa Wilaya ya Mbozi ili kupata ufumbuzi wa suala hilo ambalo limewafanya waishi kwa hofu.

Kwa uapande wake Mchungaji Zacharia Mwakasala ambaye pia ni mhanga wa kubomolewa amesema halmashauri ya wilaya hiyo inajichanganya katika maamuzi  kwani eneo hilo walipewa kihalali na kuwekewa mawe(Bicons) na maafisa ardhi kuendelea kulipia kila mwaka na kupewa stakabadhi za wilaya.

Hata hivyo Bwana Philemon Mwaisoloka amesikitishwa na kitendo cha watumishi wa halmashauri hiyo kwa kuweka alama za kubomolewa nyumba zao kwa upendeleo kwani baadhi ya nyumba za vigogo na halmashauri hiyo kutowekewa alama na pia zilizo karibu na maafisa hao zimeachwa bila kuwekwa alamayoyote hali inayojenga hofu ya kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

Naye Bi. Happines Mwanijembe ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa baadhi ya nyumba kama vile ya Afisa mipango, Afisa ardhi, Afisa mazingira, Afisa misitu, Afisa utumishi, Askari wa jeshi la Polisi, Afisa wa benki ya NMB na Meneja wa CRDB zimeachwa huku maafisa wanaondesha zoezi la kuweka alama wakijinufaisha kwa pesa kutokana na baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo kutaka wawalinde.

Hata hivyo juhudi za kumpata Mkuu wa wilaya Ndugu Kadege hiyo ziligonga ukuta baada ya kuwa nje ya Ofisi kikazi ambapo Afisa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mpandachombo, kukiri kupokea malalamiko ya wananchi hao na kwamba suala hilo atamfikishia ili atolee maamuzi.

Mama aliyemlisha Kinyesi na kumchoma moto mtoto ahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Kamanga na Matukio | 17:44 | 0 comments
Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha 
Baadhi ya wakazi wa majengo alikokuwa anaishi mtuhumiwa wakimsifu hakimu kwa hukumu aliyotoa kwa mtuhumiwa huyo
Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto
Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini.


Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
WILIVINA MKANDALA mwenye umri wa miaka 24 ameukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlisha mtoto ANETH GASTO mwenye umri wa 5 mitano kinyesi na na kumuunguza kwa maji ya moto

Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali ACHIREY MULISA ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wegine wenye tabia kama hiyo

Akisoma hukumu hiyo kwa muda wa dakika hamsini hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya mbeya GILBERT NDEURUO ameridhishwa na   na ushahidi uliotolewa na upande  wa Jamuhuri kwamba  mshtakiwa amtenda kosa kinyume cha sheria  cha makosa ya jinai namba 222(a)sura  ya kumi na sita ya marekebisho ya mwaka 2002

Hata hivyo ameiomba serikali kutunga sheria ya kumlinda  mtoto kutokana na vitendo vilivyokithiri kwa  watoto ambapo amesema tanzania haina sheria ya kulinda mtoto

Akijitetea mahakamani mtuhumiwa huyo   ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia sababu ambazo zilipingwa na mahakama hiyo

MJANE ADHURUMIWA NYUMBA NA SERIKALI YA KIJIJI

Kamanga na Matukio | 02:45 | 0 comments
Na  Ezekiel Kamanga Mbarali
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Jerumana Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amedhurumiwa nyumba na serikali ya kijiji hicho.
Hii imekuja baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu nyumba yake ya bati ibomolewe ili kupisha shughuli za kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi kwamba angeweza kujengewa nyumba nyingine  ya kuweza kuishi.
Mjane huyo ambaye hana watoto amejikuta akiishi kwa dhiki kwa kipindi chote cha masika  ambapo baadhi ya vitu vimeharibika kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa kulala 
 “Mume wangu alifariki mwaka 2007 na  kuanzia mwaka 2010  serikali ya kijiji imenihamisha  na kunileta hapa bila huduma  za msingi  kama maliwato na bafu ambapo nimekuwa nikijisetiri kwa majirani  na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza “ alisema mjane huyo.
 Kwa upande wake jirani wa mjane huyo  Bwana Mbwiga Mwayila amesema  kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa  adha kwao kwa kuwakatisha usingizi .
 Bi  Salome Mwampashi ni jarani wa mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia haraka mjane huyo ili kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema  ameshuhudia  mama huyo akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba anayoishi kuvuja na moto kuzimika 
 Naye  mwenyekiti wa kijiji  hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwa  Fulugence  Mhegele amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta maendeleo ya kijiji  ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya kulipa fidia  ingawa diwani huyo hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo .

Serikali wilayani Rungwe mkoani Mbeya imesema inatarajia kuanza kutoa vocha za Ruzuku kwa wakulima kupitia vikundi.

Kamanga na Matukio | 02:45 | 0 comments


Mkuu wa wilaya ya Rungwe Crispin Meela
 Na Gabriel Mbwille, Mbeya.
 Serikali wilayani Rungwe mkoani Mbeya imesema inatarajia kuanza kutoa vocha za Ruzuku kwa wakulima kupitia vikundi ili kukabiliana na tatizo la wizi kutoka kwa mawakala na baadhi ya watendaji wa Serikali.Akiongea na Mwandishi wetu Mkuu wa wilaya ya Rungwe Crispin Meela amesema mfumo wa awali ulikuwa ukitoa mwanya kwa mawakala kuwarubuni wakulima kwa kuwapa fedha badala ya pembejeo husika.Kuhusu sababu ya Vocha kuchelewa kutolewa kwa wakati Meela amesema imetokana na mahitaji ya vocha hizo kuongezeka.Wakati huohuo amesema Serikali imedhamiria kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwalaghai wakulima kwa kununua mazao yakiwa mashambani.Aidha amesema ili kukabiliana na tatizo la wakulima kushawishika kuuza mazao yao yakiwa shambani Serikali imeanza kutoa mikopo yenye masharti nafuu.

Frank Lampard amesema anafurahishwa na kiwango chake.

Kamanga na Matukio | 02:44 | 0 comments

Kiungo kutoka nchini Uingereza Frank Lampard amesema anafurahishwa na kiwango chake ambacho kimekua chachu ya kuiwezesha klabu ay Chelsea kuhitimisha suala la ushindi pale inapohitajika.


Frank Lampard, ambae ataondoka mwishoni mwa msimu huu kufuatia mkataba wake wa sasa kufikia kikomo wakati huo, amezungumzo furaha hiyo baada ya kuwa sehemu ya mafabnikio yaliyopatikana mwishoni mwa juma lililopita ya kuibanjua Wigan kwa idadi ya mabao manne kwa moja.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, amesema kujituma kwake na kumini bado ana uwezo wa kufanya makubwa zaidi ndio siri ya mafanikio aliyonayo kwa sasa hivyo anaamini bado mengi mazuri yanakuja kutoka kwake, licha ya majeraha kumuweka nje kwa kipindi kirefu mwanzoni mwa msimu huu.Nae meneja wa muda wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez ameungana na Frank Lampard kwa kusema bado anaamini mazuri yanakuja kutoka kwa kiungo huyo ambae anajipigia upatu wa kuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.


Benitez amesema kiwango cha Lampard kimekua kikibadilika siku hadi siku, hivyo haamini kama kitarejea nyuma zaidi ya kusonge mbele kwa ajili ya kusaka mafanikio zaidi.

Aliekua kocha mkuu wa klabu ya Simba Milovan Circovic, amesema asingependa kuifikisha klabu hiyo mbele ya FIFA, kwa kigezo cha kushindwa kumlipa malipo anayodai

Kamanga na Matukio | 02:43 | 0 comments
Aliekua kocha mkuu wa klabu ya Simba Milovan Circovic, amesema asingependa kuifikisha klabu hiyo mbele ya shirikisho la soka duniani FIFA, kwa kigezo cha kushindwa kumlipa malipo anayoudai uongozi wa klabu hiyo baada ya kusitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2012.


Milovan Circovic, ambae yupo nchini tangu juma lililopita kwa ajili ya kusaka haki yake ambayo aliahidiwa angelipwa mara baada ya fedha za usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi zitakapowasili kutoka nchini Tunisia, lakini amesema amekua akizunguushwa kila anapohitaji msaada wa kukutana na viongozi wa klabu hiyo kongwe hapa nchini.


Katika hatua nyingine kocha huyo kutoka nchini Serbia ameonyesha kusikitishwa na mwenendo wa kikosi cha simba tangu alipoondoka nchini kwa kusema, viongozi wa klabu hiyo wamefanya makosa makubwa kuharibu mipango aliyokua amejiwekea ndani ya timu hiyo, na matokeo yake hali imeendelea kuwa mbaya zaidi ya alivyoiacha.

 

Wakati Milovan Circovic, akidai kilicho halali kwake kutokana na kusitishiwa mkataba uongozi wa klabu ya simba umekiri ni kweli unadaiwa na kocha huyo aliewapa ubingwa msimu wa mwaka 2011-12, lakini wameukana ujio wake kwa kusema hawakumuarifu aje nchini kwa ajili ya kulipwa pesa zake kwa sasa.


Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema suala la kocha huyo lipo wazi na kila siku amekua akielezwa kwamba pesa za usajili wa Emmanuel Okwi zitakapowasili kutoka nchini Tunisia atalipwa stahiki zake.

 Wakati huohuo Uongozi wa klabu ya Simba umekanusha taarifa za kuwa na mifarakano na baadhi ya wachezaji kama inavyoelezwa katika vyombo mbalimbali vya habari, hatua mbayo inachukuliwa kama chanzo cha kuendelea kufanya vibaya katika michezo ya ligi inayowakabili kwa sasa. 


Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema hakuna ukweli wa jambo hilo ambalo limechukua nafasi kubwa katia vyombo vya habari tangu mwishoni mwa juma lililopita na badala yake kikosi chao kipo katika hali nzuri baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Oljoro JKT ulioshuhudia wakilazimishwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Wananchi waiomba Serikali iwalipe fidia yao ya miti kabla ya kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo itokanayo Ilomba hadi Machinjioni.

Kamanga na Matukio | 16:01 | 0 comments
 Wananchi wa mtaa wa Veta kata ya Ilemi jijini Mbeya wametishia kumzuia mkandarasi anayeendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa lengo la kuishinikiza Serikali iwalipe fidia yao ya miti kabla ya kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo itokanayo Ilomba hadi Machinjioni.
Wananchi hao wamesema wameshangazwa na kitendo cha mkandarasi kuanza upembuzi yakinifu wa barabara hiyo wakati fedha zao hazijalipwa licha ya maofisa kadhaa kutembelea eneo hilo na kuahidi kuwalipa fidia.
Baadhi ya wananchi wanaodai kulipwa fidia ya miti kabla ya kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo itokanayo Ilomba hadi Machinjioni.
Kisiki cha baadhi ya miti iliyokatwa katika eneo hilo.
 Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la miti iliyokatwa.
Nao wananchi hao wamesema miti hiyo ilikuwa tegemezi kubwa kwao na familia…

Zaidi ya wanafunzi 70 wa Kidato cha Sita wamehitimu elimu ya juu ya Sekondari katika shule ya WENDA HIGH SCHOOL.

Kamanga na Matukio | 18:53 | 0 comments
Picha na Habari na Yustina David, Mbeya..
Zaidi ya wanafunzi 70 wa Kidato cha Sita wamehitimu elimu ya juu  ya Sekondari katika shule ya WENDA HIGH SCHOOL ambapo katika mahafari hayo wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali.

Akiongea na wazazi pamoja na wahitimu mgeni rasmi wa mahafari hayo Padre Bazile Mzena amewahasa wanafunzi hao kumkumbuka Mungu katika masomo yao ili waweze kufikia malengo yao.

Sherehe za mahafali ya 4 ya Kidato cha sita shule ya Sekondari Wenda iliyopo Mbalizi zafana viongozi wa dini wahimiza wanafunzi kujituma katika masomo ya Sayansi.

Wanafunzi wa Wenda High School wakionesha umahili wao katika somo la Sayansi ambapo hapa wanaonesha namana walivyobobea katika uchanganyaji wa kemikamikali.

Mgeni Rasmi Padre Bazil Mzena ambaye ni mkuu wa Seminary ya Mafinga, akimsikiliza mwanafunzi wa Wenda High School aliyekuwa akimweleza umuhimu wa kujifunza masomo ya Sayansi na matarajio yake mara baada ya kuhitimu Kidato cha sita.


Hapa wanafunzi wakionesha mafanikio yaliyopatikana katika jaribio la kumpasua Panya.

Mtu mmoja auawa kwa wivu wa kimapenzi mkoani Mbeya.

Kamanga na Matukio | 18:52 | 0 comments
MWILI WA MAREHEMU DANIEL MWASALEMBA 30 UKIWA UMELALA KWENYE MAJANI BAADA YA KUCHOMWA KISU NA KUANGUKA MITA CHACHE KUTOKA NYUMBANI KWA ELIZABETH MICHAEL (18) KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI WA KUMGOMBANIA ELIZABETH MICHAEL.
ANAYEDHANIWA KUSABABISHA KIFO  CHA DANIEL  AMEJULIKANA KWA JINA MOJA TU PETER YEYE NI MWENYEJI WA SUMBAWANGA NA NA NIMWOSHA MAGARI YA KAMPUNI YA MABASI YA SUMRY JIJINI MBEYA AKIWA AMEPATA KIPIGO TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI
HAPA PETER AKIOKOLEWA NA WANAUSALAMA WALIOWAHI ENEO HILI LA TUKIO ASUBUHI HII
MWENYEKITI WA MTAA WA ITIJI EZEKIEL KING ALIYESIMAMA MLANGONI AKINESHA MICHILIZI YA DAMU KUTOKA KATIKA CHUMBA ALICHOMWA KISU MAREHEMU DANIEL KINACHOMILIKIWA NA ELIZABETH.
NDUGU WA MAREHEMU WAKIANGUA KILIO MARA BAADA YA KUONA MWILI WA NDUGU YAO DANIEL
HAKIKA ILIKUWA KAZI KUBWA SANA KWA POLISI KUMUOKOA PETER ANAEDHANIWA KUMUUA DANIEL KUMUOKOA KATIKA MIKONO YA WANANCHI WENYE HASIRA KALI
ANAEDHANIWA KUMUUA DANIEL AKIWA AMELALA CHINI BAADA YA KIPIGO KIKALI TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI

POLISI TAYARI WAMEUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU DANIEL  HABARI KAMILI MBEYA YETU ITAZIDI KUKUJUZA KWANI BADO TUPO ENEO LA TUKIO 

HABARI NA PICHA NA EZEKIEL KAMANGA, MBEYA.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Mwasalemba  mwenye umri wa miaka  30  mkazi wa Itiji  jijini Mbeya amefariki dunia baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenziAkizungumza na mtandao huu mwanamke aliyesababisha ugomvi huo Elizabeth Michael mwenye umri wa miaka 18  amesema marehemu alikuwa na ugomvi na mtu alifahamika kwa jina moja la Peter mkazi wa eneo hilo. Amesema ugomvi huo ulianzia katika kilabu cha pombe za kienyeji ambapo marehemu  alimsindikiza Elizabeth nyumbani kwake ndipo mtuhumiwa alipofuatilia na kumkuta nyumbani kwa Elizabeth na ugomvi kuanza saa nane usiku hali iliyopelekea mtuhumiwa kumchoma marehemu kisu na kumsababishia kifo chakeAkithibitisha kutokea kwa tukio hilo Balozi wa Mtaa huo Dotto Mwakasagule amesema baada ya kupata taarifa za marehemu kuuwawa kaika eneo lake alianza kufuatilia damu kutoka katika eneo la tukio hadi kwa Elizabeth na kumkamata Elizabeth wakati alipokuwa akipiga deki kuondoa damu.  Hata hivyo mtuhumiwa alinusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa muda mfupi katika makaburi ya Nonde ambapo aliweza kuokolewa na jeshi la polisi baada ya kufyatua risasi hewani.

Kesi inayomkabili Wilvina Mkandara kutokana na kitendo cha kumlisha mtoto kinyesi na kumuunguza mtoto hali iliyomsababishia ulemavu wa mkono ilisikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya .

Kamanga na Matukio | 18:51 | 0 comments
WILVINA MKANDARA  AKIWASONYA NA KUWAKEJELI WAKAZI WA MAJENGO MBEYA WALIOKUJA KUSIKILIZA KESI YAKE KWA KUWAAMBIA MMEACHA KUKAA MAJUMBANI MWENU MMEKUJA KUFUATA UMBEYA TU NIACHENI KUNIFUATAFUATA HUKUMU YA WIL VINA MKANDARA ITATOLEWA  TAREHE 18/2/2013

NA EZEKIEL KAMANGA MBEYA
Kesi inayomkabili Wilvina Mkandara kutokana na kitendo cha kumlisha mtoto kinyesi na kumuunguza mtoto hali iliyomsababishia ulemavu wa mkono ilisikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya
 
Akitoa ushahidi  wake mahakamani mtuhumiwa huyo alikana kuhusika na vitendo hivyo na kudai kuwa mtoto huyo alivunjika alipokuwa akicheza na wenzake na kumpeleka katika hospitali ya Ifisi  ambapo alipewa dawa za kuchua
 
Ushahidi wa  mtuhumiwa huyo ulipingwa na wakili wa serikali Achirey Mulisa na kuitaka mahakama kutupilia mbali vielelezo hivyo vilivyowasilishwa na mtuhumiwa huyo zikiwemo picha na vyeti vya hospitali ya ifisi
 
Hakimu wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo alimuonesha  mtuhumiwa picha za mtoto Aneth baada ya kukatwa mkono na kumuliza anavyojisikia kama mzazi baada ya kuziona picha hizo hali iliyopelekea mtuhumiwa kukaa kimya mahakamani
 
Hata hivyo Kesi hiyo imeahirishwa hadi February 18 mwaka huu  itakapotolewa hukumu 

Kesi inayomkabili Mchungaji Daniel Mwasumbi imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya.

Kamanga na Matukio | 18:49 | 0 comments
Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi anaetuhumiwa kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi akitoka mahakamanibaada ya kudhaminiwa

 Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Kesi inayomkabili Mchungaji Daniel Mwasumbi imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya ambapo utatuzi wa  kisheria  ulifanyika na hakimu wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo anyesikiliza kesi hiyo alitoa ufafanuzi wa kisheria

Ndeuruo amesema mahakamani hapo kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea mahakama kukataa  kupokea sampuli ya vinasaba DNA  ni pamoja na mtuhumiwa kutosaini katika barua ya mrakibu wa polisi , mshtakiwa kutosomewa  haki zake  kabla ya kuchukuliwa vipimo ,mshtakiwa kutokupewa nakala ya majibu kwa mujibu kifungu cha vinasaba kifungu cha 25 kifungu kidogo na cha pili  (c) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Pamoja na  Mlalaikaji Neema Ben  kutoa vielezo mahakamani ambavyo ni watoto wake Irene na  Johnson mahakama imesema haiko tayari kupokea vina saba kutokana na kutokukamilika  kwa taratibu za kisheria

Wakili wa serikali Achirey Mulisa  na wakili wa utetezi Mkumbe wamekubaliana  na hatua iliyofikiwa na hakimu wa mahakama hiyo ambapo kesi hiyo itatajwa tena march 7 mwaka huu.

Siku ya jana, sakata hilo la mchungaji DANIEL MWASUMBI limeingia katika sura mpaya baada ya mchungaji huyo kutokufika mahakani kwa kusingizia ugonjwa
akisoma hati ya  ya mashtaka mwendesha mastaka  wa mahakama hiyo ACHIREI MULISA mbele ya hakimu GILBERT NDEURUO amesema hakubaliani na hoja ya wakili wa mtuhumiwa wakili MKUMBE  kuwa mtuhumiwa ni mgonjwa licha ya kuwasilishwa cheti cha zahanati ya ebeneza  iliyoko kabwe jijini mbeya
Kufuatia taarifa hiyo wakili huyo aliiomba mahakama kuahirisha kesi  hiyo kwa muda na kuamua kufuatilia hadi katika zahanati hiyo ambapo dactari  YUSUFU YASINI SENTI alikiri kutoa cheti bila kuonana na mgonjwa ambapo hata jina halikuorodheshwa katika vitabu vya zahanati
Baada ya dactari  kukiri wakili alimuomba wakili wake pamoja na mdhamini  kumleta mtuhumiwa mahakamani mara moja ambapo aliletwa na  kesi kuendelea katika mahakama ya siri na ushaidi kuanza kutolewa
Miongoni mwa waliotoa ushaidi ni pamoja daktari aliyepima vinasaba  FIDELIS SEGUMBA  na mwanafunzi wa shule ya sekondari ITENDE ambaye anadaiwa kuzaa na mchungaji huyo  na kuleta vielelezo wakiwemo watoto wawili wa kike na wa kiume ambao  inadaiwa kuzaa na mchungaji MWASUMBI
 Hata hivyo kulizuka ubishani wa kisheria ambapo wakili  wa mtuhumiwa alipinga kupokelewa kwa vipimo hivyo mbele ya mahakama na kudai kuwa taratibu za kisheria hazikufuatwa hali iliyosababisha kuairishwa kwa kesi hiyo  ambapo kesi hiyo itasomwa tena leo na hakimu  kuwagiza upande wa serikali kuleta barua ya uthibitisho
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger