Pages


Home » » ASASI BINAFSI MKOANI MBEYA YATHAMINI MWANAFUNZI

ASASI BINAFSI MKOANI MBEYA YATHAMINI MWANAFUNZI

Kamanga na Matukio | 04:53 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Asasi isiyo ya kiserikali ya GOOD SERVANTS ASSOSIATION FOR THE DEVELOPMENT OF FAMILY imempatia msaada wa baiskeli Samweli Mwang’ata ili kumrahisishia usafiri wa kwenda shule ambapo awali alikuwa akilazimika kutembea kwa masaa mawili hadi shuleni.

 Akitoa msaada huo mkurugenzi wa kituo hicho Raphael Kajange amesema watoto yatima wanakabiliwa na wakati mgumu katika masomo yao kutokana na kutokuwa na wafadhili wa kuwapatia mahitji yao muhimu yakiwemo ya kielimu.

Ameongeza kuwa msaada kama huo utaendelea kutolewa na asasi hiyo kwa watoto 30 yatima inayowahudumia katika vijiji vya Mshewe, Ikukwa, Idumbi na Ihombe.

Aidha amesema kuwa asasi yake inakabiliwa na changamoto za rasilimali vitu, chakula, vitanda, magodoro na mashuka hali inayowawia vigumu kutoa huduma za malazi kwa watoto wote

Naye mwanafunzi Samweli Mwakang’ata akitoa shukrani mara baada ya kupata msaada huo amesema kuwa baiskeli aliyoipata itamrahisishia katika usafiri ambapo alikuwa akilazimika kutembea kwa zaidi ya masaa mawili kutoka kijiji cha Ihombe hadi kijiji cha Ilunga ambapo shule ilipo ya Ilunga sekondari.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger