Nembo ya maadhimiasho ya miaka Hamsini ya toka kupatikana kwa Uhuru wa taifa letu Tanzania Desemba 12, 1961
*****
Na mwandishi wetu.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Jackson Msome, Amezindua maadhimisho ya miaka 50 tangu Uhuru wa Tanganyika, yaliyofanyika katika mji wa Tukuyu mkoani Mbeya, na kuhudha riwa na mamia ya wananchi.
Msome amesema kabla ya Uhuru wa nchi yetu, wilaya hiyo wakati huo ikijumuisha wilaya za Kyela na Ileje, ilikuwa na jumla ya shule za msingi 83, .Vyuo vya Ualimu 11, madarasa ya MEMKWA 10 na MUKEJA 16”
Mkuu huyo wa wilaya alisema:”upande wa sekondari wilaya ilikuwa na sekondari moja tu ya Rungwe, lakini kwa sasa ikiwa ni miaka 50 tangu tupate Uhuru kuna jumla ya sekondari 53, zikiwemo 43 zinazomilikiwa na serikali”.
Ameongeza kwa kusema kwamba wilaya hiyo ina shule moja ya msingi maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu pamoja na shule ya msingi mchepuo wa Kiingereza huku nyingine ikiwa katika hatua za ujenzi.
Vile vile amemaliza kwa kusema kuelezea vyanzo rasmi vya maji 15, ambapo Mamlaka ya maji Mjini ina mtandao wa kilometa 53, tofauti na kilometa saba zilizokuwepo kabla ya Uhuru.
0 comments:
Post a Comment