Uongozi wa chuo cha Ualimu Moroviani Mbeya kilichopo eneo la Kadege umelazimika kubadilisha muhula wa masomo kwa kuongeza muda wa mapumziko kwa wanafunzi wa chuo hicho ili kutoa nafasi ya ukarabati wa miundombinu ya maji chuoni hapo.
Akiongea na chanzo chetu mkuu wa chuo hicho Eliakimu Mtawa amesema chuo kinakabiliwa na tatizo la mfumo wa kupitisha maji safi na taka hali iliyowapelekea kuongeza muda wa lizikizo kwa wanafunzi wake.
Chuo hicho kilifungwa septemba 26 mwaka huu baada ya kuwepo kwa hatari ya kuibuka kwa magonjwa ya miripuko kutokana na mfumo mbovu wa maji safi na maji taka.
Naye afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amesema uamuzi uliofikiwa na uongozi wa chuo hicho umelenga kulinda afya za wanafunzi na sio kama chuo hicho kimefungwa kutoa huduma za kielimu.
0 comments:
Post a Comment