Wamzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mwenzao Mkoani Mbeya.

Kamanga na Matukio | 03:18 | 0 comments
KWANZA KABISA WANAANZA TOA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA NA KUZANIWA AMEROGWA NA ALIYEZIKWA AKIWA HAI MAANA KATIKA KABURI HILO WALIZIWA WATU WAWILI KATIKA KABURI MOJA  ALIE HAI NA MFU
JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA TAYARI LIMETOLEWA HILO PEMBENI SASA ANAFUKULIWAALIEZIKWA HAI
HII MITI NDIYO ILIYOTENGANISHA JENEZA NA ALIEZIKWA AKIWA HAI KWANZA ALIANZA ALIE HAI KUZIKWA IKAFUATIA MITI HIYO NDIYO LIKAFUATA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA
MDOGO WA MAREHEMU ALIEZIKWA AKIWA HAI
MWILI WA ALIEKUFA KWA UGONJWA ULIZIKWA TENA NA WANAUSALAMA KUONDOKA NA MWILI ALIEZIKWA AKIWA HAI
WANANCHI HAO HAIKUTOSHA BAADA YA KUMZIKA MWENZAO AKIWA HAI WALIKWENDA KUCHOMA NYUMBA YAKE
NA KUHARIBU MAZAO YAKE SHAMBANI

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
 
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail alisema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
 
Alisema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.
 
Aliongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika  marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
 
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu.
 
Baada ya Mzee huyo  kupoteza fahamu Vijana hao walianza kutandika fito ndani ya kaburi kisha kufukia kwa udongo kiasi kwa lengo la kutenganisha na Mwili wa Marehemu Pita uliokuwa kwenye jeneza baada ya kuwazika kwenye kaburi moja.
 
Baada ya kukamilika kwa zoezi la mazishi kundi la vijana lilielekea hadi nyumbani kwa Mzee aliyezikwa akiwa hai na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kutotoa siri wakidai Siri ya Jeshi.
 
Hata hivyo baadhi ya wananchi walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Credo Kayanza ambaye pia alitoa taarifa kwa Diwani wa Kata hiyo Chesco Ngairo ambao kwa pamoja walitoa taarifa Jeshi la Polisi ambao baada ya taarifa hiyo walifika eneo la tukio huku wakidhani lililotokea ni kuchomwa kwa nyumba pekee.
 
Jeshi la Polisi baada ya kufanya upelelezi na kubaini kitendo hicho waliwaamuru baadhi ya Vijana kufukua kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya Vijana hao kulipwa.
 
Baada ya kufukuliwa kwa kaburi hilo Mwili wa Marehemu Mzee Mwachirui ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya Uchunguzi huku Mwili wa Pita ukizikwa upya palepale.
 
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo Marehemu alizikwa katika eneo tofauti na alipokuwa amefukiwa awali.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo pia ametoa wito na kuwaasa  wananchi na jamii kuacha tabia  ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi kwa madai kuwa hauna faida kwao bali huchochea migogoro katika jamii zao.
 
Aidha ameongeza kuwa wakumbuke kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria ambapo pia  amewaomba wenye taarifa za walipo waliohusika na mauaji hayo kuzifikisha polisi haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao ingawa hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

KANDORO ATEMA CHECHE KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO RUNGWE.

Kamanga na Matukio | 03:17 | 0 comments
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi wa habari ofisini kwake

 Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi wa dini kutoa ushauri kwa waumini pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya mauji ya kikatili vivavyo endelea kujitokeza siku hadi siku katika maeneo yote Mkoani hapa yanayo hatarisha uvunjifu wa amani na kuliletea sifa mbaya jiji la Mbeya,

Kandoro aliyasema hayo jana  wakati wa sherehe za maadhimisho  ya sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kimkoa yalifanyika Wilayani Rungwe na kuhudhuria na viongozi mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya,baada ya kutokea matukio mfululizo ya mauaji ya kinyama yanayohusishwa na imani za kishirikina,

Baada ya kutoa ushauri huo kwa viongozi wa dini,Mh,Kandoro pia alizungumzia mfumo wa serikali mbili Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo yenye dola inayo shughulikia  Utawala,Ulinzi na usalama na masuala yote ya muungano na mambo ya Tanzania Bara yasiyo ya muungano,

Alisema kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina mamlaka juu ya mambo yasiyo ya muungano yanayohusu Zanzibar  tu kama ilivyoainishwa katika sehemu ya kwanza ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake,

Aliongeza kuwa Kila mmoja wetu anao wajibu wa kudumisha umoja,mshikamano na muungano wetu kwa kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwl ,Julius Nyerere pamoja na Hayati  Sheikh Abed  Karume ambao walipiga vita udini,ukabila, Rushwa na aina zote za ukiukwaji wa haki za binadamu,

‘’Ndugu zangu wana Rungwe na wana Mbeya wote tunatakiwa tuuenzi Muungano wetu pamoja na kudumisha Amani,Utulivu,Upendo na mshikamano  miungoni mwa watanzania na majirani zetu,kupiga vita umasikini,ujinga na maradhi, kuimarisha misingi ya Utawara bora na Demokrasia’’,alisema Kandoro,

Aidha Kanoro aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kupambana kikamilifu na maambukizi  mapya ya UKIMWI,kupinga  vitendo vya Rushwa,na  imani za Kishirikina zinazopelekea mauaji ya wananchi wasio na hatia,na kuwataka kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kunufaika na huduma bora za Afya kwa kuchangia fedha mara moja tu kwa mwaka,

Pia  ailiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuri  mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za waalimu pamoja na ununuzi wa madawati ili kupunguza changamoto katika shule zetu na vijana wetu waliopo katika shule za msingi na sekondari waweze kusoma vizuri  na kupata matokeo mazuri pindi wamalizapo masomo yao.

BABU WA MIAKA 86 KYELA AMBAKA MTOTO WA MIAKA 6

Kamanga na Matukio | 03:16 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Kyela

KATIKA  hali isiyokuwa  ya kawaida iliyowashangaza wengi ni baada ya babu aliyefahamika kwa jina la Edward  Mwakalebela (86) ambaye ni mganga wa tiba za jadi mkazi  wa kijiji cha Ndwanga  kata ya Katumbasongwe wilayani Kyela Mkoani Mbeya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 6 Anjela kifoji,


Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Sioni Ijuni  aliiambia Tanzania Daima kuwa ilikuwa saa 8 usiku wa kuamkia j,mosi  mtoto wake alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo ambapo aliamua kumpa huduma ya kwanza kwa kumkanda na maji ya moto na ndipo alipoona damu zikitoka sehemu za siri,


Alisema alipomhoji zaidi ndipo mtoto huyo alipomtaja babu huyo kuwa alimuingilia kimwili na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama na kuwa mzee huyo ambaye ni jirani yao alikuwa na mazoea ya kumtuma mtoto kana kwamba ni mjukuu wake kumbe alikuwa anatengeneza mazingira ya kumfanyia unyama huo,


Kutokana na hali hiyo mama huyo alidai kuwa aliamua kupeleka taarifa hiyo kwa mwenyekiti wa kijiji akiwa na mumewe Kifoji  Mwabusila waliye tengana naye ambaye wanaishi  jirani,ambapo mwenyekiti baada ya kuandika maelezo aliwaamuru waende polisi ili wapatiwe kibali cha kwenda kutibiwa hospitalini na wao kufanya hivyo,na polisi walimkamata mtuhumiwa na kumtia hatiani,


‘’Tulipokuwa kwa mwenyekiti wa kijiji babu huyo alikili kutenda kosa hilo na aliomba msamaha akidai ni shetani tu alimpitia huku akiomba mambo hayo wamalizwe kimya kimya bila kwenda polisi jambo ambalo lilikuwa gumu wao kulikubali na ndipo  taarifa ilipo pelekwa polisi ambao walikuja kumkamata’’alisema mama mzazi wa mtoto huyo,


Mwenyekiti  wa kijiji  hicho Dickson Mwakasinga alikili kuwepo na tukio hilo na kuwa baada ya kuletewa taarifa ya uwepo wa tukio hilo alifuata taratibu zote  na kumkabidhi  mtuhumiwa huyo mikononi  mwa polisi wilaya kwa hatua zaidi za kisheria,


Mganga  wa  zamu aliyemtibu mtoto huyo Tabu Mwakalundwa alikili  kumpokea mgonjwa huyo na kudai kuwa mtoto huyo aliingiliwa na kuharibiwa vibaya na wao wanafanya jitihada za haraka za kumtibu mtoto huyo ili arudi katika hali yake ya kawaida,


Wananchi  wa kijij hicho kwa upande wao wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa kuwa mzee huyo ni mganga wa tiba za kienyeji(asili) na kuwa umri alionao na kitendo alicho mfanyia mtoto huyo wa umri wa miaka 6 ni kinyume na maadili ya mtanzania,

Cristiano Ronaldo amekanusha vikali tuhuma za kumsaliti rafiki yake wa kike Irina Shayk .

Kamanga na Matukio | 03:15 | 0 comments
Irina Shayk
 Mwanamitindo wa Brazil Andressa Urach ‘Miss BumBum’.


 Irina Shayk na Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo amekanusha vikali tuhuma za kumsaliti rafiki yake wa kike Irina Shayk kwa kutembea na mwanamitindo wa Brazil Andressa Urach ambaye anajulikana pia kwa jina ya ‘Miss BumBum’.


Urach alikaririwa na gazeti la The Sun akidai kuwa alilala na nyota huyo wa Madrid katika hoteli ya Villa Magna saa 48 kabla ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund lakini nyota huyo amesisitiza kuwa hakuna ukweli katika hilo.


Ronaldo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa twitter akilalamikia kitendo cha mwanamitindo huyo kutaka kumchafua kwa kile kilichoandikwa katika gazeti hilo.


Ronaldo aliendelea kuandika kuwa ni kweli alifikia katika hoteli hiyo Aprili 22 kwa ajili ya mahojiano lakini mengine yote yaliyozungumza baada ya hapo ni uongo na uzushi mtupu

ome » BURUDANI NA MICHEZO. » Barcelona haitasita kutumia mbinu chafu - Franz Beckenbauer Barcelona haitasita kutumia mbinu chafu - Franz Beckenbauer

Kamanga na Matukio | 03:14 | 0 comments

Mchezaji nyota wa zamani wa Ujerumani Magharibi, Franz Beckenbauer ameionya klabu ya Bayern Munich kuwa Barcelona haitasita kutumia mbinu chafu katika mchezo wa marudiano ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano.


Barcelona walibamizwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Allianz Arena wiki iliyopita na Beckenbauer ana wasiwasi kuwa Barcelona watatumia mbinu zote kuhakikisha wanageuza ametokeo hayo.


Amesema katika mchezo huo Barcelona itatumia mbinu zote katika kitabu kujaribu kuitoa Bayern mchezoni na kama wakishindwa hawatasita kutumia mbinu chafu mradi wafanikiwe lengo lao.


Lakini pamoja na yote hayo Beckenbauer hadhani kama Bayern wataifanya kazi ya Barcelona kugeuza matokeo kuwa rahisi sana kutokana na kikosi bora walichonacho hivi sasa.

HAKI YA NANI VILE, WANANCHI MBOZI WALIZWA NA MBOLEA FEKI

Kamanga na Matukio | 02:32 | 0 comments
 Sehemu ya Mifuko ya Mbolea kimeo ikisogezwa pembeni na vijana wa kazi baada ya kufunguliwa kwa dula la Mbolea la STACO LTD na kusafishwa kwamba mbolea nyingine haina matatizo

 Mbolea yenye alama ya kampuni ya YALA aina ya DAP ambayo pia imekutwa ikiwa chini ya kiwango

ofisa wa Upelelezi Mbozi akionyesha sehemu ya Mbolea mbovu ambayo imefumbiwa macho na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania na kuitakatisha kama haina matatizo wala madhara kwa wakulima


Katika hali inayoonyesha kuna mchezo mchafu wa kuendelea kuwamaliza wakulima wilayani Mbozi, shehena ya Mbolea mbovu iliyozuiwa  kuuzwa mwaka jana hatimaye “upepo umepita” na kuruhusu iendelee kuuzwa kwamba ipo juu kiviwango!

Katika hali hiyo wakulima wamekuja juu jana wakati wakishuhudia ufunguzi wa duka la STACCO ambalo miezi kadhaa lilishuhudiwa likiwa limepigwa makufuli na kwa mbwembwe nyingi ikiwemo msururu wa vyombo vya habari, lakini kwa jana ilikuwa kimya kimya kufuli la kwanza likafunguliwa, likafuata la pili na hatimaye la tatu!

Wakati wananchi kwa macho yao meupe wakishuhudia mifuko iliyoganda ya Mbolea za UREA, DAP, CAN na SA taarifa iliyotolewa kuruhusu kufunguliwa kwa duka hilo inatoa maelezo kuwa ni Mbolea ya SA peke yake  ndiyo iliyobainika kuwa na ubora hafifu! ambayo ni mifuko 11 tu.

Hata hivyo afisa anayesimamia ubora wa Mbolea katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi Bi Shonyela amesema licha ya maelekezo kutoka juu mengine hayatatekelezeka kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwamaliza wakuliwa wa wilaya yake kwakuzingatia kuwa Mbolea iliyoganda kuto kufaa tena mashambani.

“nimeandikiwa Mbolea aina ya SA pekee ndiyo isafirishwe chini ya usimamizi wa polisi kwenda Dar es Salaam lakini ni mifuko 11tu! Wakati kuna mbolea aina nyingine ambazo ni zaidi ya mifuko 50 hazina viwango vya ubora na taarifa imekuwa kimya” alifafanua

Uchunguzi wa haraka kwenye duka hilo unaonyesha kuwa mifuko16 ya DAP ilikuwa imeganda wakati wa kufunga duka hilo mwezi September mwaka jana, UREA mifuko 16, CAN 11 na SA 11.

Ingawa katika maelezo ya mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA ilionyesha kuwa wangeshirikiana bega kwa bega na TBS katika kuhakikisha viwango vya bidhaa hiyo vinasimamiwa, maamuzi ya kuruhusu uuzwaji wa mbolea aina ya DAP, CAN na UREA iliyoharibika kwenye ghala la STACO wilayani Mbozi yanajenga mawimbi na mashaka kwa wananchi kuwa mamlaka imelainishwa na ama wamefumbishwa macho!

Tanzania hutegemea maabara yake ya Mbolea iliyopo Mlingano mkoani Tanga kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo hata hivyo kumekuwepo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya maofisa wa serikali na kuwasaliti wakulima kutokana na makampuni yanayofanya shughuli za usambazaji wa pembejeo na hasa Mbolea kushika keki kubwa katika mzunguko wa fedha nchini

Wakati pia chuo cha kilimo SUA kimekuwa kikitumika katika tafiti na uchunguzi wa Mbolea, mwaka jana Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika Dr Adam Malima alikataa matokeo ya uchunguzi wa mbolea yaliyotolewa na SUA na kuahidi sampuli za Mbolea iliyokamatwa RUVUMA kupelekwa nchini Afrika kusini kujiridhisha na uchuguzi wa maabara za huko baada ya kulalamikiwa na wakulima

Aidha naibu waziri alisitisha leseni za makampuni ya STACO na Mohamed Enterpries mnamo August 07 mwaka jana, ambapo baada ya siku kadhaa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania Suzana Ikelya alitua Mbozi na kukamata Mbolea kwenye duka la STACO

“Maamuzi ya mamlaka ya ukaguzi wa ubora wa Mbolea yanawaacha wananchi wilayani Mbozi wakikosa imani kutokana na namna maamuzi yanavyofikiwa hata katika mambo ambayo hayahitaji utaalamu kuthibitisha ubora kama suala la Mbolea iliyoganda” anaeleza bwana Keneth Mwazembe mmoja wa wakulima wakubwa wilayani Mbozi.

Msimamizi wa duka la STACO bwana Julius Masai licha ya kufurahia kufunguliwa kwa ofisi yake ya chakula, amesema ni kweli kwamba kuna mbolea ambayo haimo kwenye barua ya kuruhusu uuzwaji ambayo haifai kwa matumizi lakini wanatumia busara kuitenga licha ya kutoelezwa kwenye barua hiyo

Ni kweli kuna mifuko kama 37 hivi ya mbolea mchanganyiko ambayo ni mbovu na tumeitenga pembeni na hatutaiuza” alisema meneja huyo bwana Julius Masai

Duka hilo limefunguliwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wawili wa idara ya upelelezi ya jeshi la polisi na ofisa anayesimamia ubora wa MBOLEA wilaya ya Mbozi, na shughuli hiyo imefanyika kimya kimya tofauti na mbwembwe zilizofanyika wakati wa kufunga duka hilo ambapo wananchi waliokuwa wakipita barabarani waliitwa kushuhudia namna wanavyotendwa!

Kwahisani ya Indaba Africa

Wito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala ya kukubali kupandikizwa chuki na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa na Taifa kwa ujumla.

Kamanga na Matukio | 02:31 | 0 commentsWito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala  ya kukubali kupandikizwa chuki  na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa  na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa  Scourt Mkoa wa mbeya Ndugu Pablo Sanga akizungumza na waandishi wa habari jijini humo amesema kuwa kuna kila sababu ya wananchi mkoani humo kuilinda amani ya mkoa huo ilikuvutia shughuli za kimaaendeleo .

Amesema katika kipindi cha hivi karibuni  kumekuwepo na matukio mbalimbali yanayoashiria kuvuruga amani ya mkoa huo hivyo nivema wananchi wa mkoa huo wakawa makini na baadhi ya watu wanaopandikiza chuki  zidi ya viongozi wao na serikali yao kwa ujumla.

Pablo amesema siasa chafu zinazo enezwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini ndizo zitakazo weza kusababisha madhara ambayo ndiyo yatakayo changia kuvuruga kwa amani ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.
Kauli hiyo ya kiongozi wa scourt mkoani humo imekuja kufuatia kuwepo kwa ujio wa kiongozi wa kitaifa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kufanya ziara ikiwa ni pamoja na kuzungumza katika sherehe ya mei mosi kitaifa ambayo itafanyika mkoani hapa.

Hata hivyo Kiongozi huyo wa Scourt amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanampokea vyema Raisi Kikwete katika kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anafanya ziara yake  kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa vitendo viovu.

MICHEZO YA MEI MOSI KITAIFA YAZINDULIWA MBEYA

Kamanga na Matukio | 01:43 | 0 comments

Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu   Costantine Mushi.
mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu   Costantine Mushi. akizindua michuano hiyo

Na Mbeya Yetu Blog
Michuano ya Mei mosi kitaifa katika uwanja wa kumbukumbu sokoine jijini mbeya imeendela kushika ambapo michezo mbalimbali imefanyika uwanjani hapo  baada ya kufunguliwa rasmi na mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu   Costantine Mushi.

Katika michezo ya awali kwa upande wa wanaume ilikuwa ni kati ya Wizara ya Mambo ya ndani pamoja na Wizara ya Mali asili.
Matokeo ya mchezo huo Timu ya Mambo ya Ndni imefanikiwa kuibuka kidedea kwa kuicharanga goli 3 kwa mbili timu pinzani.
Katika dk ya 22 maliasili walifanikiwa kuandika bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Hamisi Changánda mara baada ya kupkea pasi kutoka wingi ya kulia.

 Katika kpindi hicho cha kwanza wapinzani wao ambao ni Mambo ya ndani walisawazisha bao hili katika dk 38 kwa mchezaji westoni mwanjala kwa kichwa ambapo mpaka mchezo huo unakamilika katika kipindi cha kwanza  timu zote zilikwenda suruhu.

Hata hivyo kipindi cha pili mpambano ulikuwa mkali kwani timu zote zilikuwa na kasi kubwa kwani dk ya .47 Andrew Bundara wa mambo ya nadani aliandikia timu yake bao la pili ambapo katika dk ya 60  Hamisi Nyagawa aliipachikia timu yake ya Maliasili bao la kusawazisha.

Mambo ya ndani waliendela kulindama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la 3 na la ushindi kupitia kwa mchezaji wao hatari Westoni Mwanjala ambaye nfdite aliyekuwa kinara wa mapmbano huo kwa kuiandikia timu yake ya mambo ya ndani bao 3 katika kipindi chote cha dk 90 za mchezo.
Michezo mwingi ne wa pete kati ya CDA ya Dodoma pamoja Hazina Dar es salaam matokeo ni ,,,,,,,,,,,,CDA 31 Hazina 12…………Ulinzi ya Dar 38 Uhamiaji 17 .

Katika mchezo wa kuvuta kamba Hazina wanaume walishindwa nguvu na Uhamiaji.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger