Na mwandishi wetu
Ukosefu wa elimu ya ujasiriamali kwa baadhi ya wakazi wilayani Ileje mkoani Mbeya umetajwa kuwa chanzo cha umasikini wilayani humo.
Hayo yamebainika kwenye kikao cha umoja wa wakazi wa Ileje waishio Tunduma kilichofanyika hivi karibuni wilaya mpya ya Momba mji wa Tunduma.
Washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa umasikini kwa baadhi ya wananchi wilayani Ileje unatokana na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali pamoja na msukumo wa kujituma katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Madhumuni ya kuanzishwa kwa umoja huo ni kujengeana uwezo wa kujishughulisha kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, Biashara na Kilimo.
0 comments:
Post a Comment