Pages


Home » » MJASIRIAMALI AIOMBA SERIKALI KUFUNGUA MADUKA YA KUUZA VIFAA VYA USINDIKAJI - MBEYA

MJASIRIAMALI AIOMBA SERIKALI KUFUNGUA MADUKA YA KUUZA VIFAA VYA USINDIKAJI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:54 | 0 comments
Maboga tayari kwa biashara sokoni.
*****
Na mwandishi wetu
Serikali imeombwa kufungua maduka ya kuuza vifaa vya usindikaji mkoani Mbeya ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo  kupata vifaa kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Ombi hilo limetolewa na Bi.Sarah Mtalemwa ambaye anajihusisha na shughuli za usindikaji na utengenezaji wa waini ya Twinsi amesema kupitia kazi hiyo ya usindikaji wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la upatikanaji wa vifaa vya kusindikia kutokana na vifaa hivyo kupatikana Dar es salaam pekee.

Ameongeza kuwa ili kurahisisha kazi za ujasiriamali ziweze kufanyika kwa urahisi na kuwawezesha wao kupata kipato kutokana na shughuli zao za usindikaji.

Twinsi waini hutengenezwa kwa kutumia maboga na Losera ambapo chupa moja ya waini yenye ujazo milizi 750 huuzwa kwa shilingi 5,000 na yenye ujazo wa milizi 250 huuzwa kwa shilingi 2,500.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger