MBEYA CITY YAITANDIKA RUVU SHOOTING BAO 2--1

Kamanga na Matukio | 04:50 | 0 comments
Mgeni rasmi meya wa jiji laMbeya Athanas Kapunga  akisalimiana na wachezaji wa Mbeya city kabla ya mechi kuanza

Meya wa jiji la Mbeya akiongea na timu zote mbili


Wachezaji wa timu ya Mbeya city wakishangilia ushindi baadya ya kuitandika Ruvu shootingKocha wa timu ya Ruvu shooting Charles Boniface Mkwasa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mpira kwisha

Kocha wa timu ya Mbeya city Mwambusi akiongea na waandishi wa habari

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Musa akimtania kocha wa timu ya Ruvu Charles Mkwasa 


TIMU YA MBEYA CITY IMEISHINDA KWA MAGOLI MAWILI DHIDI YA MOJA YA ROVU SHOOTING WAFUNGAJI WA MBEYA CITY NI PAUL NONGA DK 7 NA STEVEN MAZANDA DAKIKA YA 90 NA GOLI LA KUFUTIA MACHOZI LA RUVU LIMEFUNGWA NA AYUBU KITALA DK 25

Na Mbeya yetu

MBUNGE WA JIMBO LA RUNGWE MAGHARIBI, PROFESA DAVID MWAKYUSA ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 40 KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA LA SABATO LA SWEBO- NTOKELA WILAYANI RUNGWE.

Kamanga na Matukio | 04:49 | 0 comments
Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akizungumza na waumini wa kanisa la Wasabato wa Swebo Ntokela kuashiria ufunguzi wa harambee ya ujenzi wa kanisa.

Watoto wakiingia kanisani kwa ukakamavu mkubwa kushiriki harambee hiyo.
Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa akiwa meza kuu pamoja na viongozi wa Kanisa la Sabato siku ya harambee.
Kwaya ya Kanisa hilo ikitumbuiza kanisa hapo siku hiyo ya harambee.
Katibu mkuu wa kanisa la Sabato Jimbo la Nyanda za juu kusini Mchungaji Steven Letter akisoma neno la Mungu kuashiria ufunguzi wa Harambee hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na waumini wakifuatilia kwa makini zoezi la Harambee lililokuwa likiendelea kanisani hapo.
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee hiyo, Award Mpandilah  na Jose Mwapamba wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Award Mpandila akisimamia zoezi la uchangiaji wa harambee lilipokuwa likiendelea.
Kamati ya maandalizi ya harambee hiyo ikiwa katika picha ya pamoja.
Award Mpandila akimkabidhi hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee hiyo Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa.
Mwonekano wa jengo la kanisa hilo lilipoishia na kulazimu kufanya harambee ili kumalizia ujenzi wake.

Profesa David Mwakyusa Waziri wa Afya wa Zamani  na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Rungwe Magharibi(CCM) amefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milion 40 katika harambee ya uchangiaji ujenzi wa kanisa la Sabato la Swebo lililopo Ntokela Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Katika Harambee hiyo  Profesa Mwakyusa ambaye alikuwa Mgeni rasmi, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo aliwasihi waumini  wa kanisa hilo kuacha tabia ya kunung’unika pale wanapojitoa kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali za kikanisa ambazo zinafanywa na makanisa hayo  ili kusaidia jamii.

Imeelezwa kuwa baadhi ya waumini wamekuwa na moyo wa kujitolea pindi misaada mbali mbali inapohitajika katika makanisa, badala yake huanza kuumia  katika mioyo yao kwa kile walichotoa kwa kuona wametoa kiasi kingi.

Prof. Mwakyusa alisema  kama waumini wameamua kujitoa kwa ajili ya shughuli  za kanisa  hawana budi kunung’unika ndani ya nafsi zao kwani kazi ya mungu ni kujitolea si busara muumini kutoa msaada halafu ujutie baadaye.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi  mmoja wa wajumbe wa kamati  ya maandalizi  ya harambee hiyo  Bw.Awadi Mpandila  alisema kuwa lengo la kuanzisha ujenzi huo wa kanisa kulitokana na wingi wa waumini katika  kanisa hilo ambao wanafikia 835.

Award alisema kuwa ujenzi huo ulianza  mwaka 2002 na kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa ni mil.279 na zinazohitajika ili kuweza kukamilisha jengo
hilo ni sh. Mil.90.

Mbali na kukamilika kwa Harambee hiyo Mpandila anatoa wito kwa wadau na marafiki wa karibu ambao walipewa kadi za mwaliko lakini walikwama kufika kuendelea kuchangia kutokana na fedha zilizopatikana kutokidhi kiwango.

Alisema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kupaua na kumalizia jengo la kanisa hilo ambalo hatua za ujenzi wa awali umekamilika hivyo Wadau na marafiki wamekumbushwa kumtolea Mungu kupitia ujenzi wa kanisa hilo.

Hata hivyo katika harambee hiyo jumla ya sh. Mil.46 zilipatikana huku fedha iliyochangwa papo kwa papo ni sh. Mil.23 huku ahadi zikiwa mil.23 .

Aidha katika harambee hiyo ,Prof. Mwakyusa alichangia zaidi ya mil.2 pamoja na familia yake.

Na Mbeya yetu

Mama Pinda awashukia mafataki

Kamanga na Matukio | 04:56 | 0 comments
·         Ataka watoto wa kike wapewe kipaumbele katika elimu
·         Ni wale wanao walaghai wanafunzi

Mke wa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Tunu Pinda, amewakemea baadhi ya wanaume wanaotumia matatizo waliyonayo wanafunzi wa kike na kuwalaghai ili watimize haja zao kwa kuwarubuni kuwahudumia huku akiitaka jamii ya Watanzania kuwapa watoto wa kike kipaumbele katika elimu.
Mama pinda ameyasema hayo katika uzinduzi wa mradi wa Msichana kwanza uliofanyika mkoani Mtwara huku akitanabaisha kuwa watoto wengi wa kike wanashindwa kuhudhuria masomo pale wanapokuwa kwenye hedhi.
Alisema, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba wasichana wanaotoka kwenye familia zinazoishi katika hali duni hukosa haki ya kimsingi ya kuweza kumudu usafi wao na kushindwa kuhudhuria masomo yao huku akiwakemea wanaume “Mafataki” wanaowalaghai mabinti kwa kuwahaidi kuwahudumia.
“Baadhi ya wasichana, kwa kukosa mahitaji muhimu zikiwemo pedi, wamejiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na ’mafataki’ ambao huwaahidi kushugulikia mahitaji yao. Hali hii haikubaliki”
“Tatizo la hedhi limekuwa likiwasumbua mabinti wetu hasa walioko katika maeneo ya vijijini na wengine walioko katika mazingira duni, alisema Mama pinda.
Mradi huo ambao umeandaliwa na TMARC na USAID kwa ufadhili wa Vodacom Foundation umelenga kuwakomboa wasichana wanaokosa kuhudhuria masomo mashuleni wakati  wakiwa kwenye hedhi umelenga kuwa endelevu na wa gharama nafuu kwa kuwawezesha wasicha zaidi ya 10,535 waliopo ndani na nje ya shule kwa kuanzia mikoa ya Lindi na Mtwara.
Pamoja na kuishukuru Vodacom, T -MARC na USAID, Mama Pinda ameongeza kuwa ni vyema sasa jamii ikaliona tatizo hilo na kulipa kipaumbele haina haja ya kufumbia macho tatizo hili ili kuwawezesha watoto wa kike kutimiza malengo yao na ndoto zao huku akitoa wito kwa viongozi wa serikali hasa katika ngazi za mikoa kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na kuwa endelevu kwa kutoa ushirikiano unaofaa kwa wahusika na kuhakikisha waalimu wanahusishwa kwa ukaribu zaidi.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Jamii (Vodacom Foundation), Yessaya Mwakifulefule, alisema kuwa “Tunaamini kwamba mradi huu utabadilisha tabia na hivyo kupunguza tabia hatarishi za ngono miongoni mwa vijana sambamba na kujikinga na kuanza kushiriki ngono mapema kama njia ya kupunguza mimba kwa wasicha wadogo mashuleni, kuepusha maambukizi ya magonjwa yanayoambukiza kama vile UKIMWI na pia kupunguza utoro mashuleni.” 
Aidha, Mwakifulefule alisema kuwa baada ya kipindi cha miaka miwili, mradi huo unapaswa kutoa mafunzo ya jinsi ya kujitunza na kufanya usafi na hivyo kuwapatia manufaa endelevu na stahiki kwa jamii katika mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara.
“Tunaamini kwamba mradi huu utafika mbali katika suala zima la usafi kwa wasichana mashuleni sambamba na kudumisha heshima yao binafsi,” alisema Mwakifulefule, akiongeza kuwa, “Vodacom Foundation imewekeza kiasi cha shilingi milioni 160.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa T - MARC Diana kisaka, alisema kuwa mradi huo wa majaribio wa miaka miwili unalenga kuwafikia mabinti wote wanaoishi katika mazingira duni.
“Lengo la mradi huu ni kuwasaidia wasichana hawa ambao wamekuwa hawaudhurii masomo kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama za mataulo maalum kwa ajili kuwasitiri wakati wanapokuwa kwenye hedhi kitu ambacho kimechangia kufanya vibaya mashuleni. Hivyo, tunaamini kwa kuanzisha mradi huu utawasaidia kuboresha mahudhurio yao mashuleni sambamba na matokeo yao kuwa mazuri,” alisema Kisaka.

Vodacom yakabidhi vifaa ligi kuu.

Kamanga na Matukio | 04:55 | 0 comments
 Wawakilishi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom tayari kwa ajili ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu 2013/2014. Pamoja nao katika picha ni Mkuu  wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni  hiyo Kelvin Twisa,(Aliyeshikilia mpira) na Mkurugenzi  wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
 Wawakilishi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom tayari kwa ajili ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu 2013/2014. Pamoja nao katika picha ni Mkuu  wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni  hiyo Kelvin Twisa, na Mkurugenzi  wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.

*******

Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom leo imekabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi hiyo vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh 400 Milioni.


Akizungumza kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo kuanza, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba pamoja na kuishukuru Vodacom kwa kutekeleza majukumu yake ya kimkataba amevitaka vilabu vya ligi kuu kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechu za ligi.


“Ninatoa wito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini kama kanuni zinavyo sema, pia ninawaomba viongozi wote tuwe na Ushirikiano katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”

 
Kama mzazi tusingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume tunapenda kuona kila mmoja akimtendea haki mdhamini kama ambavyo nay eye anavyotimiza haki yake ya kutupatia vifaa hivi.”Aliongeza Saad


Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema kuwa vifaa hivyo viko tayari na anaamini timu zote zimejiandaa vya kutosha na tayari kuingia katika mtanange wa ligi.


“Tunajisikia furaha sana kufikia hapa leo na kukabidhi vifaa hivi tukitekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zineshajiandaa vizuri na sasa tupo tayari kuanza msimu mpya wa 2013/2014.’Alisema Twissa


Twissa aliongeza kuwa vifaa vipya vilivyo kabidhiwa ni pamoja na seti za jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko (shin guards), nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine.  


Aidha, Pamoja na kukabidhi vifaa hivyo wao kama wadhamini wa ligi kuu pia wamefarijika kuona timu zote zimefanya maandalizi ya kutosha.


 “Hii ni  ishara tosha kuwa siku hadi siku ligi yetu imeendelea kuimarika na kuwa na ushindani mkubwa zaidi hakika tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya soka nchini,” alisema.


Twissa alihitimisha kwa kutoa wito kwa wadau wengine wenye malengo ya kukuza soka la Tanzania kujitokeza na kuongeza udhamini katika ligi ili kuleta tija zaidi huku akiendelea kuwakumbusha wanahabari wajibu wao wa kuitangaza ligi hususan vipaji.


Hatudhamini kwa sababu ya viongozi wala jambo jengine lolote, Vodacom inadhamini ligi kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa na ndio wenye washabiki wengi na hatimae kukuza vipaji.”Alisema Twissa na kuongeza.

 “Vyombo vya habari mnanafasi kubwa sana ya kutangaza vipaji na ligi yetu na sio kuandika habari hasi ambazo hazijengi tungepeda kuona wachezaji wetu wanakuwa maarufu kama wanavyojulikana kina Ronaldo, Rooney na wengine wa nje.”

INAUMA SANAAAA!!!!! TANESCO WAONDOKA NA UHAI WA BINTI HUYU HUKO MBEYA,PICHA ZA ENEO LA TUKIO HIZI HAPA

Kamanga na Matukio | 01:12 | 0 comments
 HAPA NDIPO MAREHEMU ALIPOGUSA NA KUKUTWA NA MAUTI

NYAYA ZA UMEME AMBAZO ZIMENING'INIA MITA MOJA KUTOKA USAWA WA ARDHI ZIMESABABISHA KIFO CHA NEEMA B. KIPENYA (26) ALIPOTELEZA NA KUKAMATA NYAYA HIZO KISHA KUFARIKI PAPO HAPO.
 KATI YA NGUZO HADI NGUZO NI UMBALI WA ZAIDI YA MITA 75 MAHALI AMBAPO PALIPASWA KUWA NA NGUZO TATU LAKINI IKAWEKWA NGUZO MOJA , HALI MTEJA WA ENEO HILO ALIKUWA AMELIPIA NGOZO TATU ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA .
 HAPA NDIPO ALIPO TELEZA MAREHEMU NEEMA NA KUANGUKIA NGUZO HIZO
 ASKARI AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MASHUHUDA 
 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO BWANA KISMAN MWANGOMALE AMBAYE NDIYE MTEJA WA KWANZA KULIPIA TANESCO NGUZO TATU  NA KUFUNGWA NGUZO MOJA , NA AMETOA TAARIFA MARA KADHAA TANESCO NA HATA KUANDIKA BARUA KWA NIABA YA KIJIJI LAKINI HAKUNA UTEKELEZAJI ULIOFANYIKA HADI MADHARA YAMETOKEA NDIPO TANESCO WAMEFIKA.

MMOJA KATI YA WATUMISHI WA TANESCO AMBAYE ALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUKATA UMEME USILETE MADHARA ENEO HILO , HATA HIVYO ALINUSURIKA KUPIGWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI AMBAO WALIKERWA NA TUKIO HILO.

 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO WA KWANZA KUSHOTO NA WATUMISHI WA TANESCO WAKIANGALIA NGUZO ZILIZO ELEMEWA NA UZITO WA NYAYA HIZO NA KUSABABISHA NGUZO KUSHINDWA KUHIMILI UZITO WA NYAYA HIZO. 
 WAOMBOLEZAJI WAKILIA KWA UCHUNGU KWANI MUDA MFUPI ULIOPITA WALIKUWA NA MAREHEMU NYUMBANI HAPO.
 MOJA KATI YA NDUGU AMBAYE ALIZIRAI KATIKA ENEO LA TUKIO
MWILI WA MAREHEMU UKIWA KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA IFISI ILIYOKO WILAYA YA MBEYA UKISUBIRI UCHUNGUZI ZAIDI WA KITABIBU.

PICHA NA EZEKIEL KAMANGA


FUATILIA KESHO JE TANESCO WATAREKEBISHA NGUZO HIZO? HII NI SINTO FAHAMU .. NB: TATIZO KAMA HILI LIPO WILAYANI CHUNYA NI MIEZI MITATU TANGU LITOLEWE TAARIFA TANESCO WILAYA YA CHUNYA NA MKOANI, LAKINI HADI LEO HAKUNA KILICHOFANYIKA NA NYAYA HIZO HAZINA GAMBA LA PLASTIC(INSULATOR). MENEJA AKILI KUPOKEA TAARIFA HIZO NA KUAHIDI KUFANYIA KAZI.

NJEMBA YA MIAKA 50 ADAIWA KUWADHALILISHA NA KUWABAKA WATOTO WAWILI.

Kamanga na Matukio | 00:53 | 0 comments
MBAKAJI ERASTO MWAKYOMO (50) ANAYETUHUMIWA KWA UBAKAJI AKIWA KATIKA OFISI YA MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE KABLA YA KUCHUKULIWA NA MWENYEKITI WA DAWATI LA WATOTO NA UKATILI WA KIJINSIA MARY GUMBO.
WATOTO WALIOKUWA WAKIBAKWA WAKITOA MAELEZO JINSI WALIVYOKUWA WAKITENDEWA
 MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE CHRISTOPHER MWAKIBETE AKIANDIKA BARUA KWA WAZAZI NA MTUHUMIWA KUPELEKWA POLISI 
 BAADHI YA WAZAZI NA NDUGU WA WATOTO WAKIWA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA MTAA.

***************

Ezekiel Kamanga

ERASTO MWAKYOMA mwenye umri wa miaka 50. Mkazi wa mtaa wa Mapelele Kata ya ILEMI jijini Mbeya anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwadhalilisha watoto wawili wa kike wote wakazi wa Mapelele.

Wazazi wa watoto hao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watoto hao ambao mmoja ana umri wa miaka minne na mwingine mitano walitoa taarifa kwa Balozi wa mtaa Bwana CASIAN MWEZIMPYA ambapo baada ya kutafakari kwa kina aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa.


Mwenyekiti wa mtaa Bwana CHRISTOPHER MWAKIBETE Aliamua kuwaita wazazi na mtuhumiwa kuwahoji yaliyotukia ambapo nao watoto walipewa nafasi ya kueleza ambao walieza kuwa ERASTO Alikuwa akiwashika sehemu za siri na kuwapaka mafuta kabla ya kufanya nao mapenzi.


Baada ya kusikiliza kwa makini MWAKIBETE aliamuru kuwa suala hilo ni la kisheria na kitaalamu hivyo hawezi kuchukua hatua zozote bali suala hilo analazimika kulipeleka Polisi ambapo Mwenyekiti wa Dawati la watoto na jinsia MARY GUMBO Alimchukua mtuhumiwa hadi kituo cha Polisi kati.


Baada ya mahojiano ya awali GUMBO aliwachuchukua watoto hadi Hospitali ya Rufaa kwa uchunguzi na mtuhumiwa kubaki kituo cha kati kwa mahojiano zaidi,hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya watoto mtaani hapo wamekuwa wakitendewa vitendo vya ukatili lakini vimekuwa vikifumbiwa macho na baadhi ya wazazi wakihisi ni aibu kwa watoto wao.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger