Pages


Home » » Breaking Nuuz: Mwanafunzi mtanzania Afariki kwa ajali mbaya Malaysia

Breaking Nuuz: Mwanafunzi mtanzania Afariki kwa ajali mbaya Malaysia

Kamanga na Matukio | 16:21 | 0 comments
Na ripota wetu kutoka Malaysia
Habari zilizo tufikia katika mtandao huu hivi punde zinasema kwamba Mwanafunzi Mtanzania anae julikana kwa jina la Ally Mfaume Amefariki dunia Leo asubuhi baada ya kuumia vibaya katika ajali iliyo tokea jana usiku.

Habari zaidi zinasema kwamba kijana huyo ambae ndie mmiliki wa Gari hilo na aliye kuwa mwanafunzi wa Help university College kilichopo nchini Malaysia alikuwa na wenzake wanaosemekana wanne walikuwa wakitoka sehemu inaitwa Sun way na walipo fika maeneo ya mbele kidogo waligonga Lori kwa nyuma na Gari lao kuumia vibaya na Marehemu pia kuumia vibaya sana.

Usiku huo huo wasamalia wema waliwakimbiza majeruhi wote mpaka Hospitali lakini Marehemu Ally kutokana na kupata maumivu makali na majeraha makali sana Mwilini mwake aliaga Dunia majila ya asubuhi.

Mpaka muda huu mwili wa marehemu upo Hospitali na taratibu za msiba zinaendelea kufanyika na Msiba upo apartment za Desa Kiara ambapo Marehemu alikua akiishi. Taarifa zaidi tutawaleteeni.

Latest News Tz inawapa pole wafiwa wote na Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger