Na mwandishi wetu
Unywaji wa pombe kupindukia umetajwa kuwa moja ya sababu inayochangia baadhi ya wazazi na walezi wa kata ya Igawilo jijini Mbeya kushindwa kutoa huduma muhimu kwa watoto wao hali inayopelekea watoto hao kuishi kwenye mazingira hatarishi.
Akiongea na mwandishi wetu mwenyekiti wa mtaa wa Mwanyanji Bwana Elia Jerema amesema watoto wanao onekana kwenye madampo wakiokota vitu mbalimbali kwa kuwa wamekosa malezi kutoka kwa wazazi ambao muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwenye uuzaji na unywaji wa pombe.
Aidha amewataka wakazi wa mtaa huo kutojihusishwa na vitendo vya unywaji wa pombe muda wa kazi na kwamba mtu atakaye kamatwa akinywa pombe muda huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Naye mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la JOHN amesema analazimika kuokota vitu kwenye madampo ya taka ili aweze kuuza na kujipatia kipato kitakachomsaidia kununua mahitaji mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment