Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. Abbas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu.
Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Sange iliyopo kata ya Sange wilayani Ileje wameacha masomo na kuamua kuoana ambapo hadi sasa wanaishi kama mume na mke.
Hayo yamebainika baada ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kufanya ziara maalumu ya kujitambulisha wilayani humo ambapo pia alitembelea kujionea hali ya ujenzi wa shule ya msingi Sange.
Akiwa shuleni hapo Kandoro alielezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Lugano Mwambuja kuwa wanafunzi Joshua Kijalo na Acheni Tete waliacha masomo mwezi Julai mwaka huu na kuamua kuishi maisha ya ndoa.

Mratibu Elimu wa kata hiyo, Joseph Mwanzela amesema wanafunzi wameacha masomo kwa sababu za kiuchumi, ambapo watoto wa kike huamua kuacha shule na kwenda kufanya kazi za ndani mijini wakati wavulana hukimbilia kufanya kazi za mashambani.
Kutokana na taarifa hizo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro ametoa agizo kwa viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha watoto hao wanapatikana na kurejeshwa masomo pamoja na wazazi wa watoto hao kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kushindwa kuwadhibiti watoto wao kufuata masomo.