Msaidizi wa Mgana Mzungu Dokta
Pondanga kutoka Kijiji cha Manienga Wilaya ya Mbrali Mkoni Mbeya
akiteketeza matunguli kwa kutumia kuni na mafuta ya taa (picha ya
kushoto). Mganga wa Jadi Mzungu Dokta Pondanga akiwa ameshika moja kati
ya majini yaliyokuwa yakitumiwa kwenda kunyonya damu za wananchi wa
Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya.
Mganga wa Jadi Mzungu Dokta Pondanga
kutoka Kijiji cha Manienga, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya akiwa
ameshika moja kati ya pembe iliyokuwa ikitumika kama usafiri na
mchawi/wachawi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya.
Mganga wa Jadi Mzungu Dokta Pondanga
kutoka Kijiji cha Manienga, Wilaya
ya Mbarali Mkoani Mbeya akionesha Pembe ambayo huuzwa zaidi ya shilingi
400,000 kwa ajili ya kusafiria mchawi/wachawi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata
ya
Iganzo Jijini Mbeya. (Picha ya kushoto). Matunguli yakiwa yamekusanywa
kabla ya kuteketezwa kwa moto(Picha ya kulia).
Askari akihakikisha Amani, usalama na ulinzi unaimarika eneo hilo.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mganga
wa Jadi Bwana Mzungu Dokta Pondanga (49) kutoka Kijiji cha Manienga,
Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amewasili Kata ya Iganzo Jijini Mbeya kwa
lengo la kuondoa matunguli na majini yanayodaiwa kuharibu amani katika
kata hiyo.
Ujio
wa Mganga huyo umetokana na ombi la wananchi na viongozi wa kata hiyo
baada ya kuchoshwa na vitendo vya kishirikina vinavyofanywa katika kata
hiyo, ikiwa ni pamoja na kufa kwa ng'ombe zaidi ya 14 kwa muda wa mwezi
mmoja, watoto kuanguka mashuleni, pesa kutoweka katika mazingira ya
kutatanisha na vinyeshi kutapakaa kwenye Ofisi za walimu.
Mganga
huyo Pondanga amepata kibali kutoka Serikalini na katani na kuhakikisha
hakuna uvunjifu wa amani ambapo Serikali imetoa Askari wawili
kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama katika zoezi hilo unahimarika.
Siku
ya kwanza ya ujio wake Aprili 29 mwaka huu ameweza kuibua matunguli,
majini na madawa mbalimbali katika kaya nne za balozi moja kati ya tano
ambazo zitatembelewa na Mganga huyo, baada ya kuibuliwa kwa vitu hivyo
katika nyumba hizo vilichomwa moto.
Baada
ya kumaliza kazi hiyo ya kuibua na kuchoma, Mganga huyo alitoa somo kwa
wachawi na wanaojihusisha na imani hizo kuacha mara moja kwani hazita
wasaidia katika maendeleo kwani hata wao waisha yao ni duni, licha ya
kununua kwa gharama kubwa ushirikina huo ambapo unadiawa hugharimu
shilingi 400,000.
Aidha
alienda mbali kwa kusema kuwa baadhi ya matunguli hayo hutumiwa na
wachawi hao kusafiria angani matharani kutoka Mbeya umbali wa Kilometa
800, hutumia nusu saa huku wakitumia damu za watu kama petroli ndio
maana hutokea vifo vya ghafla na wengine upungufu wa damu jijini hapa.
Kwa
uapnde wao wananchi walimshukuru Mganga Pondanga kwa kuwaondolea adha
hiyo ambapo baadhi yao wanaojihusisha na imani za kishirikina
wamezikimbia nyumba zao na wengine kutupia matunguli mtoni.
Hata
hivyo ameongeza kuwa kwa wale waliokimbia matunguli yao hayatafanya
kazi na yatateketezwa huko huko walipo na zoezi hilo linaendela mpaka
hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment