Pages


Home » » WANANCHI WAUOKOA KWA ASILIMIA FULANI MNARA WA KAMPUNI YA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA VODACOM BAADA YA KUANZA KUTEKETEA KWA MOTO WILAYANI MBARALI - MBEYA

WANANCHI WAUOKOA KWA ASILIMIA FULANI MNARA WA KAMPUNI YA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA VODACOM BAADA YA KUANZA KUTEKETEA KWA MOTO WILAYANI MBARALI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:48 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbarali.
Mnara wa simu za mkononi unaomilikiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania, uliopo eneo la Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya umeokolewa kwa kiasi fulani na wananchi wakati unaanza kuteketea kwa moto baada ya jenereta kulipuka.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8:00 mchana Mei 14 mwaka huu katika Jenereta la kampuni hiyo kulipuka na hivyo kusababisha moto mkubwa ambapo wasamaria wema walivunja uzio wa mnara huo na kisha kufanikiwa kuuzima moto huo.

Aidha gari la zimamoto la Halmashauri ya wilaya hiyo halikuweza kufanikiwa kukabiliana na moto huo na hivyo kubaki watazamaji wa tukio hilo.

Hata hivyo Jeshi la polisi halikuweza kupatikama mara moja mpaka tunaingiza habari hii mtandaoni ili kuweza kudhibitisha uwepo wa taarifa hili.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger