Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(Kulia) akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi katika Kata ya Itenzi.
Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(pichani kushoto )
akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo
vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi
katika Kata ya Itenzi na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Tambukareli (pichani kulia) .
Machifu wakiingia katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi ya Tambukarelikufanya tambiko la kukemea vitendo viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
Machifu wakiingia katika madarasa na kufanya tambiko la kukemea vitendo
viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za
Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwasikiliza Machifu licha ya mvua kubwa iliyokua ikiendelea kunyesha, katika zoezi la tambiko la kukemea vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
Wananchi waliojitokeza kutoka Kata ya Itenzi katika zoezi la Machifu waliofika katani hapo kutambika kwa lengo la kukemea
vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Machifu wa kabila la Kisafwa Mkoani Mbeya waliamuru
kusitishwa kwa masomo kwa siku moja katika Kata ya Itenzi Jijini Mbeya,
kutokana na wanafunzi wa jinsia ya kike kuanguka, kupoteza fahamu na
kuwanyong’oshesha nguvu.
Tukio hilo
limehusisha Shule za msingi za Gombe, Tambukareli na Mwasote, zoezi lililofanya
na Chifu kiongozi wa kabila hilo
Roketi Mwanshinga, akisaidiana na zaidi ya mchifu 30.
Pia zoezi hilo
limehudhuriwa na Diwani wa Kata ya Itenzi Mheshimiwa Frank Mayemba na Askari wa
Jeshi la Polisi na Ulinzi shirikishi L.M Kiyeyeu Aprili 2 mwaka huu.
Kabla ya kuanza kazi hiyo iliyohudhuriwa na mamia
ya wananchi wanaozizunguka shule hizo, Chifu Mwanshinga alishusha lawama kwa
Wachungaji wa madhehebu na makanisa mbalimbali Mkoani hapa, kutokana na kupokea
waumini kwa kivuli cha kuokoka bila kuwauliza machifu.
Amesema kwani wao wanafahamu hawajaacha tabia zao
za awali ndio maana vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku huku
makanisa hayo yakichipuka kama uyoga.
Chifu Mwanshinga ameenda mbali zaidi kwa kusema
daima maisha yao
ni duni, hivyo hufanya vitendo hivyo kwa nia ya kujipatia pesa wanajidanganya
kwani pesa hupatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.
Mkusanyiko huo umefanyika baada ya watoto wanaosoma
katika shule hiyo hususani wasichana darasa la tano ndio wanaoathirika zaidi na
ugonjwa wa kuanguka na kupoteza fahamu na kuwanyong’onyesha nguvu na hivyo
kushindwa kuendelea na masomo na kuwapeleka nyumbani kwao.
Katika mkutanoi huo Machifu wameagiza yeyote
anyejihusisha na masuala hayo aache mara moja na kutoa onyo yeyote atakayekaidi
agizo hilo
atatembea barabarani akiwa kichaa.
Aidha katika hali ya kusafisha mazingira hayo
machifu wote walipita katika madarasa yote ya shule zote tatu na kwamba kuanzia
sasa watapiga kambi kwa muda wa juma moja hatimaye kukomesha kabisa vitendo
hivyo ambavyo huathiri huduma za maendeleo ya elimu na kiuchumi mkoani hapa.
Kutokana na kukerwa na suala hili machifu wameagiza
wazazi wote wakeshe kwenye shule hizo ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Kwa upande wake pia Afisa Mtendaji wa Kata hiyo
Bwana Deusdedit Maseke amewashukuru wazazi kwa kuitikia wito wa kufika shuleni
hapo na kuonesha jinsi walivyokerwa na jambo hilo.
Shule kadhaa mkoani Mbeya zimekubwa na janga la
ushirikina na kupelekea kufungwa kutokana na vitendo vya kishirikina ikiwemo
Shule ya Juhudi iliyopo kata ya Iganzo ambapo Ofisi ya Mwalimu Mkuu alisilibwa
kinyesi pamoja na ofisi nyingine ya walimu mbali ya kusilibwa kinyesi vyombo
vya chakula vilitapakaa kinyesi.
0 comments:
Post a Comment