Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Raia 6 wa
nchi ya Somalia wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kuacha njia na kisha kupinduka katika Kijiji cha Luswiswi, Wilaya ya
Kyela, Mkoani Mbeya.
Tukio
hilo limetokea mei 7 mwaka huu majira ya saa nne usiku ambapo gari lenye
nambari T 934 AAR aina ya Fuso linalomilikiwa na Msuya mkazi wa Arusha
lililokuwa na wasomalia hao ambayo idadi yake haijafahamika walipokuwa
wakipita njia za panya kwa nia ya kwenda nchi ya Malawi kupitia wilaya
ya Ileje.
Dereva wa
gari hilo hakuweza kupatikana baada ya kutoroka mara baada ya ajali
hiyo kutokea na kwamba lori hilo lilikuwa katika mwendokasi dereva huyo
alishindwa kulimudu katika kona hali iliyopelekea gari kupinduka na
kuingia korongoni.
Baada ya
ajali hiyo waliojeruhiwa walijikongoja mpaka barabarani na wanakijiji wa
kijiji cha Luswiswi kutoa msaada wa hali na mali ambapo walitoa taarifa
kwa Afisa mtendaji wa kijiji Bwana Eliki Kibona.
Bwana
Kibona alitoa taarifa kwa Halmashauri ya wilaya na Ofisi ya Mkuu wa
wilaya ya Ileje ambapo walituma gari kwa ajili ya kuwachukua majeruhi
wapatao tisa ambao wamelazwa katika Hospitali ya wilaya hiyo iliyopo
Itumba Ileje.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Ileje Mheshimiwa Aliko Kibona alifika
eneo la tukio na kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa moyo wa upendo
wa huruma kwa ajili ya kutoa msaada wa hali na mali.
Miili ya raia hao wa Somalia imehifadhiwa katika hospitali hiyo, huku jeshi la polisi likifanya uchunguzi wa tukio hilo.
Aidha Idara ya uhamiaji mkoani hapa ilituma maafisa wake eneo la tukio ili kubaini uhalali wa kuwepo nchini wasomali hao.
Hata
hivyo Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa Barakiel Masaki,
amethibitisha kupata taarifa kuhusiana na tukio hilo na kwamba amemtuma
Afisa wake na kwamba atatoa taarifa mara baada ya kurejea.
Wimbi
la raia wa Ethiopia na Somalia kupitia nchini kwa njia haramu limezidi
kukua huku baadhi ya wananchi kushindwa kutoa taarifa kwa idara ya
uhamiaji na Polisi.
0 comments:
Post a Comment