Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu watatu wakazi wa Tuduma Kati, Wilaya mpya ya Momba, Mkoani Mbeya wameshtakiwa kwa tuhuma za kujeruhi.
Watuhumiwa
hao ni pamoja na Martha Ndabila(30),Gibe Prosper(37) na Victor
Haonga(37) ambapo wote kwa pamoja walifikishwa katika Mahakama ya mwanzo
Tunduma Mei 29 mwaka huu.
Watuhumiwa
hao walifikishwa mbele ya Hakimu Leonard Kazimzuri wa mahakama hiyo,
wakidaiwa kumjeruhi Bwana Elias Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Mamlaka ya Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma, Mei 28 mwaka huu majira
ya saa 5:30 asubuhi.
Akisoma
mashtaka mbele ya mahakama hiyo PP Nathani amesema kuwa watu hai
wametenda kosa la jinai kifungu cha 241 sura ya 16 ya marekebisho ya
sheria ya nchi ambapo kesi hiyo imesajiliwa kwa namba ya 236 ya mwaka
2012.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo watuhumiwa walikana kutenda kosa hilo na kesi
hiyo kupigwa kalenda mpaka June 11 mwaka huu,na Hakimu kuweka bayana
dhamana kwa washtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambapo wote
walidhaminiwa.
Aidha
sababu za wananchi hao na kufikishwa mahakamani ni kutokana na
kutokubaliana na taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa katika mkutano
wa mtaa,ambapo wananchi hao hawakutaka kukubaliana na taarifa ya
Mwenyekiti huyo wa halmashauri wakidai si sahihi na kwamba amefuja pesa za wananchi zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Kufuati
hali hiyo walimtaka mwenyekiti huyo Bwana Cheyo kujiuzuru kwa kutia
saini kwenye karatasi jambo ambalo kiongozi huyo alilikataa na kuuvunja
mkutano majira ya saa 6:30 mchana na wananchi kutawanyika.
Sakata
hilo halikuishia hapo majira ya saa 5:00 usiku, Jeshi la polisi
liliwakamata watuhumiwa hao kwa mahojiano katika Kituo cha Polisi
Tunduma, hali iliyowatia hasira wananchi hao na kusababisha taflani
kituoni hapo baada ya wananchi wengine kutaka kuvamia ili kuwatoa
watuhumiwa.
Hata
hivyo baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu Jeshi la Polisi Mei 29
mwaka huu majira ya saa nne asubuhi, lililazimika kuandaa hati ya
mashtaka kwa watuhumiwa na kuwafikisha mahakama ya mwanzo, hivyo
kushusha hasira ya wananchi hao.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Tunduma mheshimiwa Frank Mwakajoka
Mwesa,ambaye alikuwa mmoja wa waalikwa kwenye mkutano huo amesema
amesikitishwa na kitendo cha wananchi hao kushtakiwa mahakamani kwani
hakuona kitendo chochote cha sambulio na kwamba hawezi kuingilia uhuru
wa mahakama anaiachia itende haki.
Wakati
kesi hiyo ikitajwa mahakamani hapo mlalamikaji Bwana Cheyo,hakuwepo
mahakamani na pia hakuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na kesi
hiyo.
Kata
hiyo imekuwa na migogoro ya mara kwa mara hivyo kufanya eneo hilo kuwa
tete huku wanafunzi wakijazana katika vyumba vya madarasa na wengine
wakisoma kwa kuchuchumaa madarasani.
0 comments:
Post a Comment